Unafanya uamuzi mzuri na muhimu kwa maisha yako. Kila la kheri mkuu.
Ushauri:
1. Kuwa makini sana kwenye zoezi la uchaguzi. Sio kila king'aacho ni dhahabu.
2. Huna sababu ya kuwa na presha za kuoa. Uko kwenye age inayofaa kuoa lakini kwa miaka hiyo yako bado una muda wa kutosha wa kumtafuta mtu sahihi. Nakuomba usiwe desperate utaumia mbaya. Ukiwa desperate uwezo wako wa kufanya maamuzi unavurugika.
3. Wanawake wana uwezo mkubwa sana wa ku-fake ili ampate mwanaume anayemtaka. Tumia akili kufanya maamuzi.
4. Usifumbie macho baadhi ya vigezo vyako vya msingi in a woman. Ukiona mtarajiwa ana upungufu (tatizo kubwa la kitabia) usikubali ahadi ya kubadilika baada ya ukishamuoa. Mambo hayo yana tendency ya kujirudia at a certain point in time kwa watu wengi na bahati mbaya ni kuwa kama ushamuoa tayari unapoteza power ya kutosha kumbadilisha (hasa km alikupa ahadi ya kubadilika ili usimbwage). At that time hashindwi kukuambia ulinikuta niko hivi....kumbuka anakuwa hana vya kupoteza vingi. Yeah...ashaolewa. Ha ha ha