Changamoto na uzembe wa wahusika wa DSE mobile APP

ruukada

Member
Feb 24, 2014
33
125
Kama mmoja wawatumiaji wa Mobile Trading iliyoanzishwa na Dar es salaam Stock Exchange siku za husoni napenda kuzungumzia yafuatayo kwa kuwasadia watumiaji wa sasa na wajao pamoja na kuwajibishwa na wanaosimamia hiyo DSE mobile Application.

1. Kwa uwelewa wangu mdogo , Mobile App yoyote kabla haijawekwa sokoni lazima ifanyiwe majaribio na wahusika kutatua changamoto zake na kujihaminisha utayari wake kwa matumizi. DSE mobile App ilikuwa inatakiwa ifanywe hivyo ndio tuwekewe sokoni tena ukizingatia inahusika na FEDHA. changamoto zake ni kama zifuatazo;

i. Ukinunua Share kuna kisehemu cha My holdings, iki kinatakiwa kionyesha shares ulizokuwa nazo, lakini kinaonyesha 0 ( Hii sehemu ni muhimu na rahisi kumkatisha mtu tamaa kuendelea kununua shares kama hawezi kuziona, anaweza hisi ni utapeli)

ii. kuna wakati unakuwa umelipia shares lakini zinakuwa pending haziwi confirmed kama ni za kwako tayari na haziwi canceled mda ukipita. Inamaanisha hizi shares sio zako bado na hela kurudishiwa ni mtiani.

2.
DSE wametoa whatsapp numbers ili wateja waitumia wakiwa wanashida ama kutaka msaada wa matumizi ya mobile trading (DSE Mobile App) , cha kuchekesha ukituma ujumbe wakuuliza kitu ama kueleweshwa kitu kwenye hiyo whatsapp number, Wahusika wanasoma alafu wanapotezea ( Sasa sijuwi hawaelewi kwamba mtu anaona ukisoma ujumbe wa whatsapp)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom