Changamoto mnazozipata mlioa au kuolewa na wenza wenye watoto

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,790
Habari za J5 wakuu,

Kuna umri ukifika kumpata mtu ambae hajaanza maisha kabla ni nadra. Nilitaka tufahamishane changamoto unazopata pale unaokuta watoto kwenye uhusiano.
 
1. Watoto wale hata ukiwa unaonya kama mzazi bado wanakuwa na hisia kuwa unawanyanyasa.
2. Pale mwenza wako anapotaka kuwasiliana na mzazi mwenzie
3. Pale mwenza wako anapojisahau kwa bahati akakuambia, "lakini wewe hapa unakosea mwenzio alikuwa anafanya..."
 
Kuonyesha upendo kwa watoto wasiokuwa wako na wenyewe wakuelewe kuwa unawapenda kweli,hili lina wezekana iwapo huyo mwenzako atatengeneza mazingira kwa wale watoto kuwa huyu ndio baba/mama ili watoto wakukubali,lakini utakuta kutwa amekazana kuonyesha kuwa wewe sio baba/mama yao hilo ni tatizo sana,na kingine ni pale unapojitahidi kutoa ushauri wa malezi kwa yule mtoto asiekuwa wako mwenzako anaona kuwa unavyofanya sio sahihi ila yeye ndio anayeweza kumuongoza mtoto,kiukweli matatizo ni mengi sana.ndio maana Mungu hakupenda kuona wanadamu wanazini nje ya ndoa au ndoa kuvunjika kwani alijua shida ni nyingi kuliko furaha.
 
Ninadhani ni rahisi pia kuwafahamisha watoto kuwa wewe si mama Yao wala hutakaa uwe . Hii ni hasa kama amefariki ni muhimu kuwasaidia jinsi ya kuenzi siku mama Yao anafariki.
 
hakyanani nawaogopa kama ukoma sio kwa roho mbaya niliyo nayo!!!
hapana...
ila tu ukiolewa ujue upo ndani ya gereza na nilivo na machozi ya karibu hata mtoto akikaidi huwa naliaaaa balaaa sembuse haoo!!!!!! hapanaaaaaaaaaaaaaa....
 
Shost alikutana na single daddy analea watoto watatu mama Yao alishatimua. Wamekutana mwanaume pombe mtu, shost alianza mapenzi mwisho jamaa akawa baa ni weekend tu tena wanakwenda wote baada ya bia mbili wanarudi nyimbani, balanced diet kwa kwenda mbele. Bwana akapata ubunge mambo yamekuwa super si watoto wasianze kupigania mama yao arudi.
 
Habari za J5 wakuu,
Kuna umri ukifika kumpata mtu ambae hajaanza maisha kabla ni nadra. Nilitaka tufahamishane changamoto unazopata pale unaokuta watoto kwenye uhusiano.

We endelea tu na Uliyempata ukianza kutafuta huku utaishia njiani Mama .. Kama umependa na umemkuta na Mtoto wa Mwanamke mwenzio wewe endelea ila usiwe katili kwa watoto
 
Ninadhani ni rahisi pia kuwafahamisha watoto kuwa wewe si mama Yao wala hutakaa uwe . Hii ni hasa kama amefariki ni muhimu kuwasaidia jinsi ya kuenzi siku mama Yao anafariki.
Wakiienzi siku ya kufariki kwa mama/baba yao huku wakimdharau anayewatunza kwa sasa
itawasaidia nini? Ni vyema kwa gharama yoyote kuwafundisha watoto hao kumtii
na kumheshimu baba/mama aliyepo.Na hapo hutakuta matukio ya ajabu ajabu yakitokea.
 
1. Watoto wale hata ukiwa unaonya kama mzazi bado wanakuwa na hisia kuwa unawanyanyasa.
2. Pale mwenza wako anapotaka kuwasiliana na mzazi mwenzie
3. Pale mwenza wako anapojisahau kwa bahati akakuambia, "lakini wewe hapa unakosea mwenzio alikuwa anafanya..."
namba moja ndo ngumu kupita hata uwe na roho nzuri vipi hutaeleweka. watakuambia mama wa kambo sio mama mzazi .utadhani uliomba kuwa mama wa kambo
 
Back
Top Bottom