Changamoto kwenye mfumo cloud

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Miaka michache iliyopita watu wengi waliokuwa wanatumia teknohama kwenye shuguli zao za kila siku
walikuwa na tatizo sugu la kuhifadhi taarifa na nyaraka zao mbalimbali
wanazofanyia kazi wakati huo watu wengi walikuwa wananunua vifaa vyenye nafasi
kubwa kwa ajili ya kuhifadhi taarifa hizo na mengineyo .





Ushahidi uliowazi ni jinsi kampuni Fulani ilivyokuwa inahaha kuongeza ukubwa wa HDD na kila
mfanyakazi kwenye kampuni hiyo kununuliwa flashdisk yake au chombo chake cha
kuhifadhia mali zake ili aweze kuwa nazo popote anapoenda kwenye shuguli mbalimbali
.





Lakini kukawa na tatizo lingine pia kwamba mfanyakazi anaweza
kuwa yuko mtwara na komputa yake ikaharibika au hicho kifaa cha kuhifadhia
taarifa zake kikaharibika au kuibiwa au hata vyote kifaa hicho , komputa na
mengine yote yakaibiwa au kuharibika tu kampuni inakuwa imepata pigo la
kiutendaji .





Huo ni mfano mdogo wa jinsi watu na kampuni zilivyokuwa na
hofu sana na taarifa zao wakati huo .





Hofu hii kwa sasa imepungua kwa kiasi kikubwa au kama sio
kuisha kabisa lakini ujio wa tovuti kama wikileaks pia umeleta hofu kwa
teknologia zingine za kuhifadhi taarifa au kushirikiana taarifa na wengine
wanaofanya kazi kwa vikundi .





Kuja kwa mifumo mbalimbali ya mawasiliano kwa njia ya Mtandao
Maarufu kama CLOUD kumebadilisha kwa kiasi kikubwa hofu na mashaka mengi ambayo
watu wengi waliokuwa nayo wakati huo ambapo kila mtu alipenda kununua kifaa
chake kwa ajili ya kuhifadhia taarifa .





Hofu ya hufadhi na kutumia taarifa imepungua kwa kiasi
kikubwa sana kwa sababu kwenye mfumo wa CLOUD unaweza kuhifadhi taarifa na
mambo yako mengine kwa njia ya mtandao na kuweza kuchukuwa taarifa hizo ukiwa
sehemu nyingine yoyote duniani yenye huduma ya mtandao na hata unaweza kumpa
ruhusa mwingine aliyopo popote duniani kuangalia au kufanyia kazi taarifa hizo
kutoka popote duniani .





Kampuni kubwa ya masuala ya teknohama duniani iliyowekeza
kwenye mfumo wa CLOUD kwa kiasi kikubwa ni IBM mbayo ina Vituo vya kuhifadhia
Taarifa ( DATA CENTRES ) sehemu kadhaa duniani na inatoa huduma za kuhifadhi
taarifa kwa kampuni nyingine kubwa kama mabenki , mashirika ya umma na taasisi
zingine za umoja wa kimataifa .





Kampuni lingine ni GOOGLE ambalo lina programu nyingi
zinazotumika kwenye mfumo huu kama GOOGLE DOCS , Microsoft Nao wana programu
kadhaa ambazo ziko kwenye mfumo huu .





Kwa kutumia programu hizo kuna watu sasa hivi wanaweza
kufungulia barua pepe za maofusini kwao toka popote duniani kujibu na kufanya
shuguli zingine kwa ruhusa tu .





FAIDA ZA CLOUD.


1 – Faida yake kuu ni kwamba kampuni ni ndogo na kubwa
zinazotumia teknohama zinaweza kutumia aina moja ya program na vitu vingine kwa
faida bila ya kuwa na miundombinu ya ziada kama ikiwepo basi ni ya gharama
ndogo sana .





2 – Mtu mmoja anaweza kutembelea Sehemu za kuhifadhia taarifa
( DATA CENTRES ) nyingi kwa wakati mmoja duniani kwa mguso mchache wa Kipanya
chache cha komputa na kutokea popote .





3 – Pia kampuni au watu wanaweza kuongeza vitu na mengine
mengi bila ya kulipiga gharama za ziada lakini hii inategemeana na aina ya
huduma ambayo inatolewa kwa wakati Fulani .





4 – Mfumo huu uko salama na masuala ya uchafuzi wa mazingira
kwa sababu si vitu vingi vinatumika lakini hakujawa na utafiti zaidi wa adhari
zake za kiafya kwa watumiaji wa huduma hizi .





Kwa siku za mbeleni mfumo wa CLOUD utakuruhusu kununua
komputa ndogo , bei nafuu na monitor yako , hautohitaji vitu kama CDROM Au Hard
Disk Lakini utatakiwa kuwa Umeunganishwa na mtandao tu kuweza kufanya shuguli
zako za kila siku .





Pamoja na mazuri hayo niliyoyataja hapo juu pia kuna athari
zake kwa baadhi ya vitu endapo mfumo huu utafanikiwa kupenya na kutumika kwa
wingi zaidi duniani .





ATHARI ZA CLOUD


1 – Kunaweza Kuwa na ongezeko la Gharama za kusafirisha
Taarifa kwa njia ya mtandao kutokana na ukubwa wa taarifa hizo .





2 – Kwenye mfumo huu ni kampuni zingine ndio zinahifadhi
taarifa zako yaani zinazotoa huduma za kuhifadhi taarifa zako kwahiyo hautokuwa
na uwezo wa kutembelea komputa hizo au program zake kinachokuhusu wewe ni
taarifa zako tu .





3 – Inaweza kuwa
vigumu kuhamisha taarifa nyingi na kubwa kwa wakati mmoja endapo tatizo
limetokea sehemu Fulani labda Mtandao ukiwa taratibu na matatizo mengine mengi
.





4 – Taarifa zinazohifadhiwa zinaweza kuwa si salama sana na
zinaweza kupotea kwa njia nyingine au kutembelewa na wahalifu popote walipo
duniani tofauti na vile unavyohifadhi kwenye flashdisk yako .





5 – Programu zinazotumika kwenye mfumo wa CLOUD hazina vitu
vingi kama zilivyo programu zingine za kufanyia kazi zinazoingizwa kwenye
komputa za kawaida .





CHANGAMOTO MPYA ZA CLOUD


Sheria za mitandao ( cyberlaw ) za nchi nyingi haziendI
sambasamba na mfumo wa CLOUD lakini wananchi wake na mashirika yake labda
yanatumia mfumo huu kuna haja sasa ya kwa nchi nyingi kutambua rasmi mfumo huu
na kuweza kutengeneza sheria za mitandao zinazoendana na mfumo huu .





Suala la mwisho ni leseni kwa program zinazotumika kwenye
mfumo huu , mfano zamani hata sasa hivi unaweza kuuziwa leseni kwa ajili ya
komputa moja au kumi na leseni hiyo ikawa ni kwa ajili ya nchi za asia tu
lakini ukija kwenye mfumo huu leseni ya program inaweza kutumika na mtu popote
duniani na ndio shida inaanzia hapo .





Hayo ni mambo machache kuhusu mfumo wa CLOUD naamini serikali
yetu imeshaona hii pamoja na wataalamu kadhaa ma masuala ya teknohama kusoma na
kufanyia utafiti tuone nchi yetu inaweza kufaidika vipi na mfumo huu kwa siku
zijazo kutokana na gharama zake .





Jambo la msingi la kuzingatia ni kwamba faida zake na athari
zinaweza kutofautiana kutegemeana na kampuni zinazotoa huduma hizo na sehemu
ambayo mtu Fulani yupo .





YONA FARES MARO


Sunday, December 19, 2010


www.ictpub.blogspot.com
 
Many thanks for this important info. the first time I heard about cloud was tis year, september at a workshop in Bagamoyo...thanks dude.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom