Changamoto kwa ITV na Azam News: Badilisheni muonekano wa studio ya habari

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Miongoni mwa vituo vikubwa vya runinga hapa kwetu Tanzania katika kuhabarisha bila longolongo na angalau kwa ubora wenye nafuu japo sio 100% ni hivi vituo viwili vya ITV na Azam.

Kwa kweli studio zenu za kusomea taarifa za habari ziko old fashioned sana.

Nawaomba kwa niaba ya watazamaji wenzetu wekezeni ktk maboresho angalau ya hizo studio ili ziwe na muonekano wa kisasa japo kufikia kiwango cha studio za Citizen TV ya Kenya.

Tungetamani kuona movement za camera ndani ya studio kv tilts,pan nk sasa tukitazama idhaa kama BBC wana movements ya picture implements ndani ya studio kiasi kwamba habari haiboi.

Wekeni studio zenye viwango tuwe na habari ya kiwango tofauti na ilivyo sasa.

Azam mnajitahidi sana kwenye quality ya picha zote zikiwemo za regional reporters...kwa upande wa ITV bado baadhi ya waandishi wenu wanaleta picha duni.

Tafadhalini tupeni kitu bora. Ninyi wote mna muscles tupeni kitu kizuri kinachoendana na wakati tuliopo.
 
"Mimi ni Audas Mtiganzi Aitiivii, Biharamulo"..hahah jamaa hana mvuto wa utangazaji kabisaa!
 
Mbona umewasahau Aridhio Mkuu??
Hawa nimewaweka kiporo aliewajengea kale kastudio hajawatendea haki hakana viwango vya Televisheni ya Taifa. TBC 1 waangalie studio ya KBC tu hapo wajilinganishe kale kastudio kamebuniwa kinyonge sana...Tanzania fedha tunazo waombe pesa wajenge studio ya nguvu ambayo hata Rais wa nchi anaweza kuzungumza na wananchi wake moja kwa moja kwenye studio ya namna hiyo.
 
Ila mtoa uzi, studio ya azam na citizen tofauti yao ni ukubwa tu chumba lkn citizen meza zao kusomea habar ni ile ile tu,
Tusitake kushindana na bbc, cnn, aljazeera hawa majamaa yana studio kama 20 ivi na kumbuka wana vituo vidogo vya kurushia matangazo na utangazaj ktk miji mingine pia,
Hapa Tv ukenge li studio kama la al jazeera kwanza wadhamini wenyewe tu wale wale kila siku
 
Miongoni mwa vituo vikubwa vya runinga hapa kwetu Tanzania katika kuhabarisha bila longolongo na angalau kwa ubora wenye nafuu japo sio 100% ni hivi vituo viwili vya ITV na Azam.

Kwa kweli studio zenu za kusomea taarifa za habari ziko old fashioned sana.

Nawaomba kwa niaba ya watazamaji wenzetu wekezeni ktk maboresho angalau ya hizo studio ili ziwe na muonekano wa kisasa japo kufikia kiwango cha studio za Citizen TV ya Kenya.

Tungetamani kuona movement za camera ndani ya studio kv tilts,pan nk sasa tukitazama idhaa kama BBC wana movements ya picture implements ndani ya studio kiasi kwamba habari haiboi.

Wekeni studio zenye viwango tuwe na habari ya kiwango tofauti na ilivyo sasa.

Azam mnajitahidi sana kwenye quality ya picha zote zikiwemo za regional reporters...kwa upande wa ITV bado baadhi ya waandishi wenu wanaleta picha duni.

Tafadhalini tupeni kitu bora. Ninyi wote mna muscles tupeni kitu kizuri kinachoendana na wakati tuliopo.
Uwekezaji ni pesa. Kaa ukijua tangu mtawala aliyepita aingie madarakani, aliharibu sana sekta ya habari na hivyo kupoteza mvuto. Watu wakaacha kuangalia taarifa za hapa kwetu, hivyo kupoteza watazamaji. Hata watangazaji wa BIASHARA wakaacha kutangaza matangazo yao kwenye TV na kutapelwka kwenye platforms zingine. Fedha ikakata, Mengi akafa, Mali zikagombaniwa.
Bora Azam wanaweza kuchukua hela za lambalamba
 
Itv maripota Ni Kama wanaongea kilugha Ni Mimi stiviniiiii mutinganziiiiii
 
Back
Top Bottom