Chanel Ten sa mbili unusu leo LHRC, Na mkurugezi wa SSRA kuhusu Mifuko ya kijamii

SSRA Ilikuwa haina umuhimu wa kuundwa labda kama walitumia kigezo cha kutoa ajira kwa akina IS.Inakula pesa za watanzania sioni kazi yake haswa. Tungeondoa uchafu wa hizi Agency zinamaliza kodi zetu tuu. Magari ,wafanyakazi,safari, fedha ya kuendeshea na kodi ya jengo wanayompati mheshimiwa mwenye jengo ni kuliibia taifa tuu.
 
This is ridiculous! Vijana wa sasa tunaishi leo siyo kesho. Wengi hutuna mpango wa kufanya kazi za kuajiriwa hadi kustaafu bali tunatafuta mitaji tujiajiri. Hivi serikali inapopiga kelele watu wajiajiri bila kuwapa mitaji wanategemea nini?Sisi wengine tunategemea michango yetu iwe mitaji mambo ya kufikisha miaka 60 ni mawazo mufilisi kabisa na haikubaliki! Kama serikali inajali wastaafu ingeonesha mfano kwa wazee wa Africa masharika wanaopuliziwa maji ya kuwasha kila siku. Kwa hili serikali ya CCM iwe makini kama inataka kuendelea kututawala. Hivi inawezekana kukopeshwa nyumba ya m.60 au 80 wakati umechangia m. 10 au 15 tu? Kwa wale wanaocha kazi na kujiunga na mashirika ya kimataifa yenye mifumo yao ya pension kama UN, AfDB,WB na mengineyo au kupata kazi nje ya nchi inakuwaje? Hii SSRA naona inajitahidi kuiondoa CCM madarakani!!! Kwa hili wafanyakazi tupo pamoja!!!!! CHADEMA semeni neno, CUF tayari.
 
wasiwasi wangu na hii hasira niliyonayo line itapatikana kweli?wadau tukomae kupinga hii dhuluma!!!
Yaani ukisikia watu waliolaaniwa ni haya magamba,afadhali hata line ya simu isingepatikana wamekata umeme wenyewe toka saa nane mpaka saa tano usikU!!!!!Wacha nimezee maana nikifunguka hadharani hiki kitukano chake BAN itanipitia kama kimbunga!!!!!
 
hii nchi ya ajabu sana. hivi inakuwaje hawa watu wanakaa wanatoa maamuzi kuhusu pesa zetu bila hata ya kutu consult. ipo haja kubwa sana kuipinga kwa nguvu zote sheria hii kandamizi na ya kinyonyaji. through pesa zetu kila siku wanaanzisha miradi ambayo haitunufaishi sisi moja kwa moja bali kujaza matumbo yao tu! cha ajabu wabunge wetu tunaotegemea watutetee wao wamejitoa kwenye suala hili! hii ni dhulma kubwa na wadau tuipinge kwa nguvu zetu zote. hakuna mwenye uhakika wa kufika miaka 55 na pia kazi zenyewe hazieleweki siku hizi.
 
Naona mkurugenzi wa SSRA ameingia mitini,mpaka saa hii hajaonekana...
Nakumbuka Mh. Rais ali- emphasis hizi taasisi za serikali na wizara ziwe na maofisa habari na nilitumaini kuwa ingesaidia lakini kumbe ilikuwa ni janja yao kuwaweka front watu ambao wako trained 'kuficha ukweli' na naona mpaka sasa hakuna wanachosaidia.
 
Back
Top Bottom