Chanel Ten sa mbili unusu leo LHRC, Na mkurugezi wa SSRA kuhusu Mifuko ya kijamii

Janja PORI

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
825
246
kwa taarifa nlizo nazo leo kipindi cha sa mbili na nusu watakuwepo wadau wakichambua sheria mpya inayokataka withdraw benefit, wadau mpige simu kuchangia
source Chanel Ten.
 
kwa taarifa nlizo nazo
leo kipindi cha sa mbili na nusu watakuwepo wadau wakichambua sheria
mpya inayokataka withdraw benefit, wadau mpige simu kuchangia
source Chanel Ten.
wakuu tupige simu leo kutoa machungu yetu...tusiishie kwenye keybord tu....
 
kwa taarifa nlizo nazo leo kipindi cha sa mbili na nusu watakuwepo wadau wakichambua sheria mpya inayokataka withdraw benefit, wadau mpige simu kuchangia
source Chanel Ten.


na namba yao ya simu ni 2116348, nitahakikisha napiga kuchangia, wacha nijipange
 
Kwa taarifa nilizo nazo, mkuu/mkurugenzi wa SSRA mama Irene Isaka yupo Geita, mgodi wa Geita, na nasikia alikuwa na wakati mgumu sana na wafanyakazi wa huko, ameahidi anaenda kujipanga upya while wafanyakazi wa mgodi huo (wenyewe huwa wajiita watingaji) wamemwambia kama atakuja na story zake hizo bora asirudi.
 
kwa taarifa nilizo nazo, mkuu/mkurugenzi wa ssra mama irene isaka yupo geita, mgodi wa geita, na nasikia alikuwa na wakati mgumu sana na wafanyakazi wa huko, ameahidi anaenda kujipanga upya while wafanyakazi wa mgodi huo (wenyewe huwa wajiita watingaji) wamemwambia kama atakuja na story zake hizo bora asirudi.

alituma mwakilishi yupo ofisini hata sasa namzoom kabisa
 
LHRC walisema wanakwenda mahakamani. Sasa wanajadili nini na hawa wezi?
 
aa bana liwalo na liwe.
Hata wakitaka waninyime mshahara wangu wanipe nikifikika miaka 55 poa tu.
 
naweza vunja screen kwa hasira! maamuzi ya kipuuzi, ingejadiliwa kabla, sio wanajadili wakati maamuzi wameshafanya!
 
  • Thanks
Reactions: ram
siolewi job description ya mkurugenzi wa SSRA. Yeye yupo kulinda maslahi ya mifuko badala ya kubalance walaji na watoa huduma?
 
wasiwasi wangu na hii hasira niliyonayo line itapatikana kweli?wadau tukomae kupinga hii dhuluma!!!
 
  • Thanks
Reactions: rom
Ni kawaida. Halufu ya kinyesi huanzia kwa mwenyewe kabla ya wengne.

Huyu Mkurugenzi wa SSRA nasikia alikuwa huko huko kwenye hii mifuko. Sijui aliokotwa na nani maana naona kama anafanya kazi na wakurugenzi wa hii mifuko badala ya kuwadhibiti. amekuwa kama wabunge wa CCM wanavyowapigia makofi mawaziri badala ya kuwadhibiti.
 
Huyu mama hakuna kipya atakachosema. Hiyo ni SHERIA TAYARI imeshapitishwa na BUNGE na kusainia na RAIS.

Yeye atakachofanya leo ni kuitetea hiyo sheria BY HOOKS AND CROCKS. Mark my word, do not expect anything NEW. Kumsikiliza Irene ni kupoteza mda.

Kinachotakiwa ni SISI WAFANYAKAZI kUUNGANA na kuilazimisha SERIKALI kuifanyia tena marekebisho SHERIA hii OVU. Kumsikiliza Irene is wasting our precious time. Irene is a party of the problem.
 
Wafanyakazi wote wenye maslahi na hili tuungane pamoja kuwaeleza watawala kuwa wanayotaka kututendea ni unyama wenye dhulma nyingi zinazo mchukiza Mungu. Wao wanapanga kutumia jasho letu lakini wao hawataki sisi kufaidika na pesa zetu? eti mpaka miaka 55! Nani anaye jua kuwa ataifikisha miaka hiyo wakati vibarua/kazi zenyewe hazieleweki kila siku ni afadhari ya jana?
 
Leo nilikuwa pale PPF ARUSHA, Kuna kijana mmoja kaja anasema yeye amefanya kazi kwa mhindi na ameachishwa anadai PPF yake ya Tsh.80,000/. sasa je asubiri mpaka afikie miaka 55, na sasa anamiaka 18?....... serikali ijibu na hapa..... Nyambafu zao....... hivi hao CHANEL 10 Hawana line za sms sisi wengine tutume walau sms tu... simu najua zitaharibika leo...
 
Wafanyakazi wote tuwe kitu kimoja katika hili nasi huku geita tumeamua kuwa jumamosi tutakuwa na maandamano ya kuipinga hii sheria kandamizi kwa wafanyakazi.Sisi huku tumewapa muda mpaka jumatatu wawe wameiondoa hiyo sheria kandamizi hivyo tuungane pamoja kuipinga na hata ikiwezekana kugomea sensa sisi na familia zetu.
 
Miye nashangaa sana hawa wabunge wanapitisha sheria ambazo wao haziwahusu wao wakimaliza muda wao wanalipwa chao hawasubili mpaka miaka 55 kwanini sisi ndiyo watupitishie sheria kandamizi kwanini?
 
Back
Top Bottom