Chama kipya kuzoa wabunge Chadema, NCCR-Mageuzi

Chama kipya kuzoa wabunge Chadema, NCCR-Mageuzi

Hao wabunge kilichowavuna toka CHADEMA na NCCR na si CCM na CUF ni kwa namna gani eti kwa sababu nifamuvyo mimi uhai wa bunge hili ambamo ndani yake kuna hao wabunge ni hadi hapo mwezi septemba,2015 siku chache kabla ya uchaguzi?

Kwa mfumo wa sasa hakuna mbunge anayeweza kuchia ngazi aache mafao yake eti akaingie ktk chama kipya ambacho kumbe hata hakijasajiliwa,labda mwandishi kakosea anamaanisha ADC ambacho tayari kipo na bendera yake inaelekea kufafana kidogo na ya CHADEMA. Zitto Kabwe,Kafulila na Hamadi Rashidi wamegangamala hadi leo ili wasitemeshwe ubunge na vyama vyao!!

Huu naona ni uongo flani wenye malengo maalumu!!
 
Hakuna cha kuhangaika, ni strategies ndo inayotumika. Mkuu usisahau na madiwani wa kumwaga wa chadema watachukua fursa ya kujiunga na chama hicho. The Alliance

Watajiunga 2015 baada ya kuwa wametemwa kwenye vyama vyao vya sasa, lakini sahau Mbunge na diwani kuhama chama kabla ya 2015! Ni Mbunge gani anaweza kuchezea 160milions za kiinua mgongo chake eti anataka kuhamia chama kipya...forget it!
 
[h=2][/h]JUMAPILI, FEBRUARI 02, 2014 06:34 NA AGATHA CHARLES


BAADHI ya wabunge wa majimbo na wale wa viti maalumu kutoka vyama vya Chadema na NCCR-Mageuzi, wanatazamiwa kujiunga na chama kipya cha siasa kinachodaiwa kuundwa na wanachama waliomeguka kutoka vyama vya upinzani nchini, Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania).

Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa chama hicho kimejiandaa vya kutosha ili kuweza kuchukua wabunge hao pamoja na wale wa chama tawala, ili kujiimarisha katika harakati zake za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mpaka sasa kuna wabunge kadhaa kutoka Chadema na NCCR-Mageuzi ambao tayari wamethibitisha kujiunga na chama hicho.

“Nakwambia chama kimejipanga, kwani kitakuwa cha kipekee na hakijawahi kutokea nchini, kuanzia sera za chama, wanachama watakaojiunga, kwani mpaka sasa kuna watu wakubwa wanatazamiwa kujiunga nacho na kitafika 2015 kikiwa imara sana,” alisema mtoa habari huyo.

Taarifa za awali zilizolifikia MTANZANIA Jumapili, ziliwataja viongozi waliofukuzwa Chadema hivi karibuni ambao ni aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo pamoja na Samson Mwigamba, kujiunga na chama hicho, ingawa wenyewe hawakuwa tayari kukiri.

Mwingine ambaye gazeti hili lilidokezwa kuwa anapewa nafasi ya juu kuingia ndani ya chama hicho iwapo kitasimama vyema, ni Zitto Kabwe, ambaye kwa sasa ubunge wake unashikiliwa na Mahakama.

Chanzo cha gazeti hilo kilibainisha kuwa ACT-Tanzania, ambacho harakati zake zimekuwa za kimya kimya, kinatazamiwa kuzinduliwa mara kitakapokamilisha usajili wa kudumu, ambapo mpaka sasa kina wanachama Tanzania Bara na Zanzibar.

Gazeti hili limefanikiwa kuziona rangi za bendera ya chama hicho, ambazo ziko nne, ikitawaliwa na ile ya zambarau.

Alipotafutwa Mwigamba ili kupata ukweli kuhusu madai hayo, alisema kwa sasa hakuna chama ambacho viongozi wake wamemfuata ili ajiunge nacho, lakini kama chama hicho kitakuwa na sera anazozitaka, anaweza kujiunga nacho.

Alisema mpango alionao ni kuanzisha chama kipya ambacho kitaweza kuwa na sera za kujali Watanzania pamoja na kusimamia rasilimali za nchi.

“Kwa sasa nawasiliana na Kitila ili tushauriane, akikubaliana na mawazo yangu tutaanzisha chama kitakachoshiriki uchaguzi kuanzia wa Serikali za mitaa mwaka huu, iwapo hatutaangushwa na Ofisi ya Msajili na pia uchaguzi mkuu 2015 kwa kusimamisha wagombea mpaka ngazi ya urais,” alisema Mwigamba.

Alisema chama anachofikiri kuwa kinamfaa ni kile kitakachotetea wanyonge, fursa kwa watu katika rasilimali za nchi, huduma za jamii, kodi kulingana na pato la mtu pamoja na pensheni kwa wazee.

Dk. Kitila Mkumbo alipotafutwa juzi kwa njia ya simu, alisema bado anatafakari kwa kina kuanzisha chama ama kujiunga na chama chochote cha siasa kutokana na kuwa na majukumu ya kitaaluma zaidi.

“Nina kazi ya taaluma yangu, bado kwanza nafikiria, nikiona chama kinachonifaa nitajiunga nacho. Hivi sasa kuna ujio wa Katiba mpya, hivyo ngoja tusubiri, haina haraka,” alisema Dk. Mkumbo.

Gazeti hili liliwahi kuripoti kwa mara ya kwanza juu ya kuanzishwa kwa chama hicho kipya, kikiitwa African Alliance for Change and Transparence (AACT), lakini baadaye kilibadilishwa katika hatua za kukisajili na kuitwa ACT-Tanzania.


Ni Chadema pekee, ndiyo ilianzishwa na mwaka huohuo ikashinda uchaguzi mdogo kigoma mjini. Na ikakichukuq miongo miwili kufika hapo kilipofika

Kuanzisha chama kwa mihemko ya kutaka eti kikue haraka haraka na kiifunike Chadema, hizo ni akili za Popo,

Watasubiri sana Mazee, Chadema tunazidi kuimarika na zaidi Chadema kadi tunauza hatutoi bure
 
Vita yakombozi ningumu hizi niharakati zakutakatu nchi ijitawale wanzishe tu hata hiki chakwetu kilianzisha tofauti kidogo name ccm.ilizaliwa
 
mi nawashauri akina zzk wakaanzishe ufugaji wa kuku tu,maana haya wanayotaka kufanya yameshindwa kabla hayajafanyika. hivi hawajakaa na kujikumbusha yale ya ccj? viongozi fulani wa ccm walijiapiza kuhamia huko lkn mpaka leo wanakana hata kuwahi kukisikia ccj. Tunaisubiri hiyo ACT
 
Kwa waliokuwa wanamwamini ZZK nadhani sasa mmeshajua yeye ni nani, kama wanaunda chama au hawaundi hayo ni yao wala hayana msingi kwa taifa. Taifa la wajinga huongozwa na wajinga, ni vema kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii kuendleza maisha na si kuhangaika na hawa watu,
 
Kama ni kweli ccm itatawala milele tofauti kabisa na hivi tunavyofikiri,kuanzisha chama kipya ni kuipa ccm afya.CCM wanajitahidi sana kutugawa Watanzania kwa mbinu mbali mbali na hii ni mojawapo.
 
Kitila, you have put things in the manifesto which made me walk out of CCM (Kitila, umeweka mambo katika ilani ambayo yalinifanya mimi nitoke CCM). Nikamuulize yapi hayo mzee, akanieleza sera kama vile za elimu bure, serikali kusimamia kilimo, na akanionyesha sura kama mbili hivi katika ilani ambazo kwa maoni yake, na kweli ndivyo ilivyokuwa, zilikuwa haziendani na msimamo wa CHADEMA kiitikadi na kifalsafa. Nikacheka sana
 
Ni Chadema pekee, ndiyo ilianzishwa na mwaka huohuo ikashinda uchaguzi mdogo kigoma mjini. Na ikakichukuq miongo miwili kufika hapo kilipofika

Kuanzisha chama kwa mihemko ya kutaka eti kikue haraka haraka na kiifunike Chadema, hizo ni akili za Popo,

Watasubiri sana Mazee, Chadema tunazidi kuimarika na zaidi Chadema kadi tunauza hatutoi bure

Kitila, you have put things in the manifesto which made me walk out of CCM (Kitila, umeweka mambo katika ilani ambayo yalinifanya mimi nitoke CCM). Nikamuulize yapi hayo mzee, akanieleza sera kama vile za elimu bure, serikali kusimamia kilimo, na akanionyesha sura kama mbili hivi katika ilani ambazo kwa maoni yake, na kweli ndivyo ilivyokuwa, zilikuwa haziendani na msimamo wa CHADEMA kiitikadi na kifalsafa. Nikacheka sana
 
Kama Zitto yuko huko, sijui atatuthibitishiaje kuwa hicho chama siyo CCM C!!!??? Sijui ata-fight vipi na rafiki yake JK!!??
 
Back
Top Bottom