Chama kipya kuzoa wabunge Chadema, NCCR-Mageuzi

Chama kipya kuzoa wabunge Chadema, NCCR-Mageuzi

Maandalizi gani ya uchaguzi kama si mbinu ya kudhoofisha upinzanzani nchini? ccm at work.
 
Kikiongozwa na kitila nitamfwata kwani naeshimu mawazo yake na upeo wake jamaa ni balaaa nimecoka kuwa mfwasi wa cdm hakieleweki kwani sijasikia sera zake kwenye opretion opd sera niliosikia tu watauza ndege ya kikwete nikajiuliza ile ndege ni ya kikwete au ya watanzania slaa hana sera

Sidhani Chadema kama inao wafuasi kama wewe!
ImageUploadedByJamiiForums1391342461.796056.jpg
 
Zzk atajijambia had ----- lipasuke

vipande 30 vya pesa ndio vlivyomzika
 
eti hakuna chama kilichowahi kutokea kama hicho!shit!utahila mtupu!

kwa hiyo kinaanzishwa na wasaliti mbalimbali kutoka vyama mbalimbali siyo!upuuzi gani huu!.
 
Hakuna cha kuhangaika, ni strategies ndo inayotumika. Mkuu usisahau na madiwani wa kumwaga wa chadema watachukua fursa ya kujiunga na chama hicho. The Alliance

labda Msando!!!! sioni mwingine mwenye akili fyatu anayeweza kujiunga na wasaliti au wahuni!!!
 
Tawi la ccm, be careful this is a straegy iliyoandaliwa miaka mingi tu iliyopita. Kuna agenda nyuma yake
 
Kama hukupumbazwa na ZZT basi unapumbazwa na Mbowe na Slaa! Bado wewe ni mtaji wa wanasiasa tu.

Haswaaa hao ndio wakombozi wangu nikiona mtu anataka kuwaletea za kuleta kam maccm yanavyofanya ndio unapoweza kuona nilivyo kuwa mbogo, Mh. Mbowe na Dr. Slaa ndio fahari yangu, je una lingine....
 
Wapiga kelele ni wengi watendaji ni wachache. Kuanzisha chama sio kazi ngumu ishu ni kisimamia na kuendesha. Sijaona uwezo wa Zitto katika utekelezaji wa agenda za muda mrefu. Kitila hayuko tayari kuacha ajira yake.
 
Walizoea kuhujumu na kusaliti mipango ya wenzao sasa wajiunge ili wasalitiane vizuri
 
Ingawa hii habari ni ya kutungwa na Mtanzania, ingekuwa kweli ingekuwa rahisi mtu kupata uenyekiti bila haja ya kuandaa mkakati wa ushindi au kuchafua wengine...

Namshauri ZZK awahi kujiunga akatimize ndoto ya kuwa mwenyekiti bila kuchafua watu...
 
Waje tu kimbunga cha chadema watakiona kitapitia mpaka magholofa pipozi?
 
Hii habari ni ya kweli kabisa,Chadema watamchukua Zitto na NCCR watamchukua Kafulila.
 
Litakuwa jambo jema kwa kuwa na chama kingine. Ndiyo kukua kwa demokrasia huko. Ninachoweza kusema huu ni muendelezo wa harakati ya wana-njama za kuivuruga chadema kwa maana ya kuwahusisha Zitto na kundi lake. kupitia chama hiki kipya watakitumia kama jukwaa la kuisema vibaya Chadema na si CCM kwenye sponsored platforms. Hawana mpango wa kushinda uraisi, but, kutawanya kura za Chadema ambazo zinatarajiwa kuwa nyingi uchaguzi ujao. Huu ni mkakati mkubwa, na kwamba kina Zito na wenzake hawana hasara kwa sababu, bill zao zitakuwa zimelipwa. Wanamageuzi msiwacheke na kuwashangaa hawa jamaa. Hii inaweza kuwa kweli. si mnakumbuka enzi za Mobutu na vyama vya upinzani!!!!!!!!. Kwa M4C, lichukulieni hili kwa makini na katika ziara zenu hivi sasa waambieni wanainchi kile wanachotaka kusikia kuhusu huu usaliti. God Bless the Movement.
 
Hata CCJ ilianza kwa mbwembwe kama hizi tatizo letu ni kusahau tu matukia yaliyopita. Leo hii kinajiita CCK, hata hawa nao wataenda na kufia mbele ya safari.

JUMAPILI, FEBRUARI 02, 2014 06:34 NA AGATHA CHARLES


BAADHI ya wabunge wa majimbo na wale wa viti maalumu kutoka vyama vya Chadema na NCCR-Mageuzi, wanatazamiwa kujiunga na chama kipya cha siasa kinachodaiwa kuundwa na wanachama waliomeguka kutoka vyama vya upinzani nchini, Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania).

Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa chama hicho kimejiandaa vya kutosha ili kuweza kuchukua wabunge hao pamoja na wale wa chama tawala, ili kujiimarisha katika harakati zake za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mpaka sasa kuna wabunge kadhaa kutoka Chadema na NCCR-Mageuzi ambao tayari wamethibitisha kujiunga na chama hicho.

“Nakwambia chama kimejipanga, kwani kitakuwa cha kipekee na hakijawahi kutokea nchini, kuanzia sera za chama, wanachama watakaojiunga, kwani mpaka sasa kuna watu wakubwa wanatazamiwa kujiunga nacho na kitafika 2015 kikiwa imara sana,” alisema mtoa habari huyo.

Taarifa za awali zilizolifikia MTANZANIA Jumapili, ziliwataja viongozi waliofukuzwa Chadema hivi karibuni ambao ni aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo pamoja na Samson Mwigamba, kujiunga na chama hicho, ingawa wenyewe hawakuwa tayari kukiri.

Mwingine ambaye gazeti hili lilidokezwa kuwa anapewa nafasi ya juu kuingia ndani ya chama hicho iwapo kitasimama vyema, ni Zitto Kabwe, ambaye kwa sasa ubunge wake unashikiliwa na Mahakama.

Chanzo cha gazeti hilo kilibainisha kuwa ACT-Tanzania, ambacho harakati zake zimekuwa za kimya kimya, kinatazamiwa kuzinduliwa mara kitakapokamilisha usajili wa kudumu, ambapo mpaka sasa kina wanachama Tanzania Bara na Zanzibar.

Gazeti hili limefanikiwa kuziona rangi za bendera ya chama hicho, ambazo ziko nne, ikitawaliwa na ile ya zambarau.

Alipotafutwa Mwigamba ili kupata ukweli kuhusu madai hayo, alisema kwa sasa hakuna chama ambacho viongozi wake wamemfuata ili ajiunge nacho, lakini kama chama hicho kitakuwa na sera anazozitaka, anaweza kujiunga nacho.

Alisema mpango alionao ni kuanzisha chama kipya ambacho kitaweza kuwa na sera za kujali Watanzania pamoja na kusimamia rasilimali za nchi.

“Kwa sasa nawasiliana na Kitila ili tushauriane, akikubaliana na mawazo yangu tutaanzisha chama kitakachoshiriki uchaguzi kuanzia wa Serikali za mitaa mwaka huu, iwapo hatutaangushwa na Ofisi ya Msajili na pia uchaguzi mkuu 2015 kwa kusimamisha wagombea mpaka ngazi ya urais,” alisema Mwigamba.

Alisema chama anachofikiri kuwa kinamfaa ni kile kitakachotetea wanyonge, fursa kwa watu katika rasilimali za nchi, huduma za jamii, kodi kulingana na pato la mtu pamoja na pensheni kwa wazee.

Dk. Kitila Mkumbo alipotafutwa juzi kwa njia ya simu, alisema bado anatafakari kwa kina kuanzisha chama ama kujiunga na chama chochote cha siasa kutokana na kuwa na majukumu ya kitaaluma zaidi.

“Nina kazi ya taaluma yangu, bado kwanza nafikiria, nikiona chama kinachonifaa nitajiunga nacho. Hivi sasa kuna ujio wa Katiba mpya, hivyo ngoja tusubiri, haina haraka,” alisema Dk. Mkumbo.

Gazeti hili liliwahi kuripoti kwa mara ya kwanza juu ya kuanzishwa kwa chama hicho kipya, kikiitwa African Alliance for Change and Transparence (AACT), lakini baadaye kilibadilishwa katika hatua za kukisajili na kuitwa ACT-Tanzania.

 
Back
Top Bottom