Chama kipya kuzoa wabunge Chadema, NCCR-Mageuzi

Chama kipya kuzoa wabunge Chadema, NCCR-Mageuzi

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=2][/h]JUMAPILI, FEBRUARI 02, 2014 06:34 NA AGATHA CHARLES


BAADHI ya wabunge wa majimbo na wale wa viti maalumu kutoka vyama vya Chadema na NCCR-Mageuzi, wanatazamiwa kujiunga na chama kipya cha siasa kinachodaiwa kuundwa na wanachama waliomeguka kutoka vyama vya upinzani nchini, Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania).

Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa chama hicho kimejiandaa vya kutosha ili kuweza kuchukua wabunge hao pamoja na wale wa chama tawala, ili kujiimarisha katika harakati zake za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mpaka sasa kuna wabunge kadhaa kutoka Chadema na NCCR-Mageuzi ambao tayari wamethibitisha kujiunga na chama hicho.

“Nakwambia chama kimejipanga, kwani kitakuwa cha kipekee na hakijawahi kutokea nchini, kuanzia sera za chama, wanachama watakaojiunga, kwani mpaka sasa kuna watu wakubwa wanatazamiwa kujiunga nacho na kitafika 2015 kikiwa imara sana,” alisema mtoa habari huyo.

Taarifa za awali zilizolifikia MTANZANIA Jumapili, ziliwataja viongozi waliofukuzwa Chadema hivi karibuni ambao ni aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo pamoja na Samson Mwigamba, kujiunga na chama hicho, ingawa wenyewe hawakuwa tayari kukiri.

Mwingine ambaye gazeti hili lilidokezwa kuwa anapewa nafasi ya juu kuingia ndani ya chama hicho iwapo kitasimama vyema, ni Zitto Kabwe, ambaye kwa sasa ubunge wake unashikiliwa na Mahakama.

Chanzo cha gazeti hilo kilibainisha kuwa ACT-Tanzania, ambacho harakati zake zimekuwa za kimya kimya, kinatazamiwa kuzinduliwa mara kitakapokamilisha usajili wa kudumu, ambapo mpaka sasa kina wanachama Tanzania Bara na Zanzibar.

Gazeti hili limefanikiwa kuziona rangi za bendera ya chama hicho, ambazo ziko nne, ikitawaliwa na ile ya zambarau.

Alipotafutwa Mwigamba ili kupata ukweli kuhusu madai hayo, alisema kwa sasa hakuna chama ambacho viongozi wake wamemfuata ili ajiunge nacho, lakini kama chama hicho kitakuwa na sera anazozitaka, anaweza kujiunga nacho.

Alisema mpango alionao ni kuanzisha chama kipya ambacho kitaweza kuwa na sera za kujali Watanzania pamoja na kusimamia rasilimali za nchi.

“Kwa sasa nawasiliana na Kitila ili tushauriane, akikubaliana na mawazo yangu tutaanzisha chama kitakachoshiriki uchaguzi kuanzia wa Serikali za mitaa mwaka huu, iwapo hatutaangushwa na Ofisi ya Msajili na pia uchaguzi mkuu 2015 kwa kusimamisha wagombea mpaka ngazi ya urais,” alisema Mwigamba.

Alisema chama anachofikiri kuwa kinamfaa ni kile kitakachotetea wanyonge, fursa kwa watu katika rasilimali za nchi, huduma za jamii, kodi kulingana na pato la mtu pamoja na pensheni kwa wazee.

Dk. Kitila Mkumbo alipotafutwa juzi kwa njia ya simu, alisema bado anatafakari kwa kina kuanzisha chama ama kujiunga na chama chochote cha siasa kutokana na kuwa na majukumu ya kitaaluma zaidi.

“Nina kazi ya taaluma yangu, bado kwanza nafikiria, nikiona chama kinachonifaa nitajiunga nacho. Hivi sasa kuna ujio wa Katiba mpya, hivyo ngoja tusubiri, haina haraka,” alisema Dk. Mkumbo.

Gazeti hili liliwahi kuripoti kwa mara ya kwanza juu ya kuanzishwa kwa chama hicho kipya, kikiitwa African Alliance for Change and Transparence (AACT), lakini baadaye kilibadilishwa katika hatua za kukisajili na kuitwa ACT-Tanzania.

 

Mbona hii Habari inazizitizia Wabunge watakaotoka CHADEMA na NCCR pekee?? kwanini hawatoki CCM au CUF... ???

Au ni ZITTO METHODOLOGY kueleza kuwa atahamia hicho chama na kuna NCCR watamfuata??

Mmm Sijui kama Tanganyika ni kama KENYA... Tunachagua Jina mtu na familia yake na sio Party PLATFORM -- Hapo then kwanini tunalalama kuhusu ARDHI; MAFISADI; UNGA ??
 
Huyo zzk atahangaika sana ila watu kama mimi hawezi kunipumbaza hata kidogo
 
Ngoya tusubiri maana hakuna mbunge hata 1 anaweza kuacha kiinua mgongo yaye yamkute kama yaliyomkuta mpenda zoe na CCJ tusubiri tuone
 
CCJ ilikuwa na mbinu hizi hizi ikawa hata kabla .........
 

Mbona hii Habari inazizitizia Wabunge watakaotoka CHADEMA na NCCR pekee?? kwanini hawatoki CCM au CUF... ???

Au ni ZITTO METHODOLOGY kueleza kuwa atahamia hicho chama na kuna NCCR watamfuata??

Mmm Sijui kama Tanganyika ni kama KENYA... Tunachagua Jina mtu na familia yake na sio Party PLATFORM -- Hapo then kwanini tunalalama kuhusu ARDHI; MAFISADI; UNGA ??
Nina hakika hakuna chama kitakachoanzishwa sasa kikapata umaarufu, Yawezekana hata wasipate Mbunge hata mmoja.
 
Ina maana mpaka sasa hivi hawajahamia hicho chama chao kipya??
Nawashauri wawahi mapema kabla chama hakijachacha
 
Ingawa hii habari ni ya kutungwa na Mtanzania, ingekuwa kweli ingekuwa rahisi mtu kupata uenyekiti bila haja ya kuandaa mkakati wa ushindi au kuchafua wengine...
 
Hiko chama lengo lake ni kuua upinzani tanzabia
 
Teh teh, yangu masikio, kuanzisha chama ni rahis, kazi kukieneza kwa wananchi, wapi Dp, Tlp, Sau, PPT-MAENDELEO, jahazi asilia?
 
Ningekuwa msajili singetoa kibali wakaashe mavyama yaliyolala
 
Hakuna cha kuhangaika, ni strategies ndo inayotumika. Mkuu usisahau na madiwani wa kumwaga wa chadema watachukua fursa ya kujiunga na chama hicho. The Alliance
 
Wivu huo, kwa mujibu wa katiba lazima kipite, alafu ndo chadema margaya to sasa-lla
 
Si Bora APPT Maendeleo inawafuasi kuliko hicho chama, watanzania siyo wajinga tena hawana muda wa kupoteza na vyama vinavyoanzishwa na CCM.
 
Lazima kipite kwa mujibu wa katika,kwa kuwa wewe unatawaliwa na emotions ndo maana sio msajali wa vyama. Any way kitapita mda si mrefu kisha wale Jamaa wa chadema ambao ni pro Zitto kabwe will join him, kisha chadema ni margayato saa-llaa
 
Kikiongozwa na kitila nitamfwata kwani naeshimu mawazo yake na upeo wake jamaa ni balaaa nimecoka kuwa mfwasi wa cdm hakieleweki kwani sijasikia sera zake kwenye opretion opd sera niliosikia tu watauza ndege ya kikwete nikajiuliza ile ndege ni ya kikwete au ya watanzania slaa hana sera
 
kila unapokaribia uchaguzi ccm inaanzisha tawi lake kwa mgongo wa chama cha upinzani,obviously wakina zitto ndipo wanapoelekea huko.
 
Back
Top Bottom