Chama Kipya cha Siasa chasajiliwa, CM-TANZANIA!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
VYAMA vya Siasa nchini vimeaswa kuepukana na migogoro na kutumia vikao vyao katika kuendeleza shughuli zao za kisiasa.
Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis Mutungi wakati akikabidhi Cheti cha Usajili wa muda kwa Chama kipya cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA).

Aidha, Jaji Mutungi amevitaka Vyama vya siasa nchini kufanya siasa na sio uanaharakati kwaki kwa kufanya hivyo malengo yao yatatimia na kuifanya Tanzania kuwa na amani.
‘’Msipende kukimbilia kwenye vyombo vya habari mnapokuwa na migogoro bali malizeni tofauti zenu ndani ya vikao vyenu kulingana na Katiba ya Vyama vyenu’’, alisema Jaji Mutungi.

Aliongeza kuwa, Tanzania inapaswa kuwa na vyama vya siasa vinavyojitambua na vinavyojua wajibu wao katika kuleta maendeleo ya Taifa kwani siasa sio chuki wala uasama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA) Bwana Laban Nkembo amesema kuwa, chama hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuiweka Tanzania kimaadili na uwajibikaji kwa kuwa kinabeba mambo makubwa mawili yakiwemo Amani na Upendo.

Ameongeza kuwa, chama chao sio cha Upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani hivyo, kinaahidi kushirikiana na Chama Tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na chama hicho.
‘’Chama chetu sio cha upinzani, tunataka nchi nyingine duniani ziwe zinakuja kujifunza Tanzania kuhusu amani na maendeleo tulionayo’’, alisema Nkembo.

Aidha, amebainisha kuwa, chama chao cha CM-TANZANIA kitatoa ajira za kudumu kwa Wanachama wake na hata kwa wale wasiokuwa wanachama ambapo kimeshaandaa Idara ya usimamizi mzuri wa huduma kwa jamii kama vile Wazee, Wajane, Walemavu pamoja na Yatima.
CM-TANZANIA ni Chama cha 23 kupokea usajili baada ya Vyama vingine vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu.
 
Hivi vyama mbona vimekuwa vingi sana na havioneshi tija yoyote?
 
"...Chama siyo cha Upinzani, kinaheshimu chama kilichopo madarkani". Ndiyo nini sasa?

Huyu Nkembo asije kuwa ni jamaa fulani alisomaga DUCE akiwa kama mwehu mwehu hivi japo wenye kupata access na classified za nchi walikuwa wakimuhusisha na jamaa wa KIJITONYAMA
 
hii ndio Tanzania, kila kukicha chama kipya cha siasa, swali la kujiuliza je, tulivyokuwa navyo vinauthubutu.?
 
"...Chama siyo cha Upinzani, kinaheshimu chama kilichopo madarkani". Ndiyo nini sasa?

Huyu Nkembo asije kuwa ni jamaa fulani alisomaga DUCE akiwa kama mwehu mwehu hivi japo wenye kupata access na classified za nchi walikuwa wakimuhusisha na jamaa wa KIJITONYAMA

wababaishaji ktk maisha huwa wa kwanza kufanikiwa. wanabahati za ajabu. hivyo usishangae classmate wako kesho kuwa mwajiri wako. nenda kadake ajira maana hicho siyo chama, ni NGO ya kusaidia makundi maalumu
 
Pia na Gazeti jipya limeanzishwa na toleo la kwanza limetoka leo linaitwa Tanzania mpya.
------------------------------------
CM-TAnzania siyo.....wangefupisha hivi.... CCMU yaani Chama cha Maadili na Uwajibikaji...! Wangepata promo ya bure kupitia ccm.
 
"...Chama siyo cha Upinzani, kinaheshimu chama kilichopo madarkani". Ndiyo nini sasa?

Huyu Nkembo asije kuwa ni jamaa fulani alisomaga DUCE akiwa kama mwehu mwehu hivi japo wenye kupata access na classified za nchi walikuwa wakimuhusisha na jamaa wa KIJITONYAMA
Hakika.He's!
 
Inchi hii ni ya vyama vingi na ipo kikatiba..tena kwa taarifa yako mimi ni mwanachama..
Mwanachama wa hicho chama kipya? Najua katiba inasema hivyo, namaanisha sioni kipya chochote kitakacholetwa na chama hicho zaidi kitakuwa tu kama hivi vilivyopo
 
Ameongeza kuwa, chama chao sio cha Upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani hivyo, kinaahidi kushirikiana na Chama Tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na chama hicho.
‘’Chama chetu sio cha upinzani, tunataka nchi nyingine duniani ziwe zinakuja kujifunza Tanzania kuhusu amani na maendeleo tulionayo’’, alisema Nkembo.
Ametumia muda mwingi kusajili chama. Angeweza kusajili kama NGO au kufanya jumuiya ya chama
 
Pia na Gazeti jipya limeanzishwa na toleo la kwanza limetoka leo linaitwa Tanzania mpya.
------------------------------------
CM-TAnzania siyo.....wangefupisha hivi.... CCMU yaani Chama cha Maadili na Uwajibikaji...! Wangepata promo ya bure kupitia ccm.

Yasemekana andiko lao la kuomba usajili liliandika ccm-u msajili akawabania. Wangebamba kinoma.
 
hiyo ya kuenzi mazuri ya chama tawala inatakiwa kutolewa ufafanuzi zaidi. mbali na hapo hicho ni chama cha magumashi
 
‘’Chama chetu sio cha
upinzani, tunataka nchi
nyingine duniani ziwe
zinakuja kujifunza
Tanzania kuhusu amani na
maendeleo tulionayo’’,
alisema Nkembo.

???????!!!!!!!???????????????????
 
Back
Top Bottom