CHAMA KIPI CHAWEZA KUJIVUNiA NINI NA KWA MAFANIKIO YAPI?

MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
0
Mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania ulianza mwaka 1992 baada wanaharakati wakisaidiawa na Nyerere kuilazimisha CCM kukubali mfumo huo ingawa CCM ilikuwa imeshinda kwa asilimia 85 -15 ya kura za maoni. Tangu kuanza kwa mfumo huo, mabadiliko mengi ya ki utawala ktk nchi hii yamekuwa yakitokea hasa kwa kusukumwa na vyama kutekelezwa kwa sera zao na chama tawala na mengine kwa sababu za kawaida.


Naomba tujadili chama kipi kimefanya nini cha kukumbukwa na kijivunie kwa lipi. Mimi nitaanza kwa kutaja matukio machache ili wengine mchangie na mwishoni ntajumuisha tuone chama kinachostahili kupata heshima iliyotukuka hapa Tanzania.
 1. CCM ndicho chama kilichoshinda shinda ktk chaguzi zote 1995,2000,2005 na 2010 hivyo kudhihirisha kuwa kinakubalika zaidi.
 2. CCM ndicho chama pekee ambacho kimekuwa kikishindanisha wagombea wake wakati wakupata mgombea urais kupitia chama chao.
 3. CCM ndicho chama kimekuwa kikitumia fedha nyingi kwenye Kampeni zake.
 4. CUF ndicho chama kilichosumbua sana Chama tawala katika medani za kimataifa baada ya kukataa kuitambua serikali ya mapinduzi na kususia baraza la wawakilishi mpaka Jumuiya za Kimataifa kuibana serikali ya Muungano na kuinyima misaada SMZ
 5. CUF ndicho chama ambacho kiliibana serikali sawasawa mpaka maeneo waliko na wafuasi yasitawalike.
 6. CUF ndicho chama ambacho kimelazimisha hoja zake zikakubaliwa, kutekelezwa na kuingizwa kwenye Katiba ya zanzibar.
 7. CUF ndicho chama Kilicho anzisha vuguvugu lililo pelekea kwa mara ya kwanza Tanzania ikazalisha wakimbizi.
 8. CHADEMA ndicho Chama pekee cha Upinzani ambacho Mwasisi wa Taifa hili Mwl. Nyerere alikisifia kuwa ni Chama Mbadala na kwamba kina sera nzuri.
 9. CHADEMA ndicho chama ambacho sera yake ya kuigeuza Dodoma kuwa Mji wa Elimu badala ya kuufanya Mji Mkuu, inatekelezwa ingawa kwa shingo upande na chama kinachotawala.
 10. CHADEMA ndicho chama cha upinzani pekee ambacho kimewahi kushinda viti vya ubunge vingi na katika mikoa tofauti tofauti hata kuonekana kukubalika nchi nzima.
 11. CHADEMA ndicho chama cha kwanza kufanya kampeni kwa kutumia Helkopta.
 12. CHADEMA ndicho chama cha upinzani pekee kilicho na waasisi ambao si viongozi wake tena lakini bado wanaheshimiwa.
 13. NCCR Mageuzi ni chama cha upinzani ambacho Muasisi wa taifa Mwl. Nyerere aliwahi kukipigia kampeni kwenye uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Mwibara.
 14. NCCR Mageuzi ni chama kiliwahi kuvuma sana baada ya kumpata kada maarufu kutoka chama tawala.
 15. NCCR Mageuzi ni chama kiliwahi kumvisha uenyekiti wa papo kwa papo Mwanachama aliyejiunga nacho bila taratibu za kichama.
 16. NCCR Mageuzi ni chama kilichotokana na wanaharakati waliosukuma hadi kuleta mfumo wa vyama vingi.
 17. DP ni chama ambacho kimesimamia sera ya kurudisha Tanganyika bila kuchoka wala kubembeleza.
 18. UDP ni chama ambacho kinaonekana kama cha mtu binafsi, familia au wilaya moja.
 19. UDP ni chama kinaonekana kuwa kidogo lakina hakijawahi kukosa mbunge kwenye Bunge la JMT tangu mfumo wa vyama vingi.
 20. ENDELEZA..........
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom