Chama gani kilifanikisha mitandao kufikia hatua hii na urahisi wa mawasiliano

Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,660
3,233
JF,

Tumekuwa tunadanganywa na wagombea wetu hasa Lowassa na Sumaye eti kwa zaidi ya miaka 50 CCM haijafanya kitu. Tumekuwa na maswali meeengi ya kujiuliza.

1). Hivi hata upanuaji wa matumizi ya mitandao kama hivi tunavyowasiliana si ni kazi ya CCM. Mbona hatuwapongezi?

2). Hivi Lowasa na Sumaye si nao walikuwa mawaziri wakuu kwa jumla ya miaka 13. Ina maana na wao hawakufanya chochote? Ilikuwa total workdone zero?

Na wanaendelea kula kodi za wananchi bila aibu mpaka sasa!

Ni lazima tutafakari sana nchi yetu hii.
 
Mchango wa ccm kwenye mawasiliano ni ttcl (ambayo almost ni mfu tayari). ..
 
Babeli, umesema tutafakari lakini sidhani kama umetafakari nini maana ya neno upinzani!

Ukitafakari kwa makini utaona kwamba ni lugha ya kisiasa tu kwa wanasiasa ili kuonesha upinzani. Labda wasiitwe wapinzani la sivyo hawatakuwa na la kupinga
 
Huyu naye mawasiliano na Serikali wapi na wapi CCM imekufa na TTCL sababu ya ufisadi mmeua TTCL ili mlete kampuni binafsi kazi yenu ni kutunga sheria za kudumaza vyombo vya habari.
 
Haujui kwamba ndio nchi ambayo inatoza kodi kubwa kwenye mawasiliano hadi unalazmishwa ujiunge na kifurushi ili waweze kutumia hela yako vizuri.
 
Haujui kwamba ndio nchi ambayo inatoza kodi kubwa kwenye mawasiliano hadi unalazmishwa ujiunge na kifurushi ili waweze kutumia hela yako vizuri.

Acha uongo wewe usishabikie usiloelewa , tembea uthibitishe usemayo . unaonekana haujawahi kusafiri kwenda nchi yoyote pole sana
 
Back
Top Bottom