Chama cha wananchi (CUF) Kuzungumza na wana habari kesho

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
KESHO JUMATATU Tarehe 26/2/2018 saa 5 kamili asubuhi katika Ofisi ya Wabunge wa CUF, Magomeni –Dar es Salaam. Mwenyekiti wa KAMATI YA UONGOZI TAIFA MHE. JULIUS MTATIRO atafanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya Kitaifa kuhusu Hali ya kisiasa na Demokrasia nchini, uchumi, usalama na jamii kwa ujumla.

Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii [Social Media Networks] mnakaribishwa kuhudhuria kwa wakati na pia mtapata fursa ya kuuliza na au kupata ufafanuzi wa masuala Mbalimbali yanayohusu mashauri yanayoendelea Mahakamani, Mwelekeo wa Chama cha CUF na Taifa kwa ujumla na kwa kadri mtakavyo hitaji juu ya ufafanuzi wa masuala hayo. Aidha, kwa vyombo vitakavyohitaji mahojiano maalumu [Exclusive Interview] vinakaribishwa na kutujulisha mapema kwa uratibu.

CUF NI TAASISI IMARA YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa leo Tarehe 25/2/2018 na;

ANDERSON NDAMBO
AFISA HABARI CUF-TAIFA

Mawasiliano; +255 (0) 677332808, 078234841 Email:andambo@yahoo.com

Mkurugenzi Salim Bimani- 0655314112, 0777414112

Naibu Mkurugenzi Mbarala Mahargande- 0715062577, 0767062577
 
Msije mkaletewa Polisi na kuambiwa hicho kikao chenu si halali na mnaleta uchochezi.......

Kwa kuwa hii hali tuliyofikia ni mbaya mno ya Bwana Mkubwa kutaka watu wamsifie tu bila kumkosoa hata kidogo!

Yeye anajiaminisha kuwa ni mkamilifu wa 100% sawasawa na Mungu!
 
Msije mkaletewa Polisi na kuambiwa hicho kikao chenu si halali na mnaleta uchochezi..

!
Mtatiro hatambuliwi na msajili wa vyama vya siasa hivyo hana nguvu kisheria kuitisha kikao chochote hata press conference wakipigwa virungu wasipige yowe kuwa wanaonewa. Mwenyekiti CUF Taifa ni Lipumba hicho cheo anachojinadi nacho Mtatiro hakipo kwenye katiba ya CUF
 
Wd

Wewe ni nani huko cuf?
 
kwa mara ya kwanza nchi inakua attention kutoka uchaguzi mmoja hadi mwingine kwa kipindi cha miaka mitano......wananchi hawasahau kama walipiga kura .....
 
wengine wanajutia kura zao...wengine hawatam tena kupiga kura....wengine wahajielewi....
 
Mtatiro hatambuliwi na msajili wa vyama vya siasa hivyo hana nguvu kisheria kuitisha kikao chochote hata press conference wakipigwa virungu wasipige yowe kuwa wanaonewa. Mwenyekiti CUF Taifa ni Lipumba hicho cheo anachojinadi nacho Mtatiro hakipo kwenye katiba ya CUF
Ila Musiba anatapuliwa na Mtungi kwamba ndio intelligence wa Lumumba ndio maana kila mara anakurupuka na kuita waandishi?
 
Mtatiro hatambuliwi na msajili wa vyama vya siasa hivyo hana nguvu kisheria kuitisha kikao chochote hata press conference wakipigwa virungu wasipige yowe kuwa wanaonewa. Mwenyekiti CUF Taifa ni Lipumba hicho cheo anachojinadi nacho Mtatiro hakipo kwenye katiba ya CUF
Kamuulize Lipumba, kama Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na Ikulu, ameisha pata ruzuku kiasi cha shilingi ngapi kwenye hawamu hii ya 5?
 
Ni matumaini yetu makubwa tu kwamba hiyo Press yao ya Kesho haitoonyesha udhaifu mkubwa kama ambao tumeuona leo katika Press ya Cyprian Musiba.
 
Mtatiro hatambuliwi na msajili wa vyama vya siasa hivyo hana nguvu kisheria kuitisha kikao chochote hata press conference wakipigwa virungu wasipige yowe kuwa wanaonewa. Mwenyekiti CUF Taifa ni Lipumba hicho cheo anachojinadi nacho Mtatiro hakipo kwenye katiba ya CUF
Wewe mkata mauno wa lumumba Tangu lini umekuwa msemaji wa cuf? Tangu uje mjini kwa mbio za mwenge unajitia kiburi sana,,, wasalimie wenzako UWT
 
Back
Top Bottom