Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT): Hatutaichagua CCM

Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT): Hatutaichagua CCM

Awsom

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
1,085
Reaction score
307
Habarini wadau,

Tokea Alhamisi asubuhi mpaka jana jioni kulikuwa na meeting katika ofisi mpya ya CWT iliyojengwa kwa mfuko wa waalimu kuanzia june 2013, Kwakweli ingawa halikuwa katika agenda,ila Ghafla waalimu kwa pamoja walilizungumzia na walikubaliana kutomchagua Mgombea yeyote wa CCM.

Asilimia 80% ya waalimu walisema kuwa CCM imekuwa ikiwadanganya waalimu kama watoto wadogo,yaani wakitoa ahadi ambazo hawazitekelezi kwa miaka yote.

Aliyekuwa katibu wa CWT Mkoa naye alisema tatizo la kutopandishiwa mishahara au kupandishiwa kwa asilimia ndogo sana,Waalimu kutopandishwa madaraja na Malimbikizo ya mshahara ndilo limewafanya waalimu wasiwe na imani na serikali ya CCM tena.

Naye Mwalimu mkuu kwa muda wa miaka 15 kazini alisema kuwa: Hatuwezi kuwapigia kura viongozi wa serikali wanaotudharau na kudharau fani yetu ya ualimu,aliendelea kusema kuwa Waalimu wa taifa hili wamekuwa wakipuuzwa na hata kutukanwa tofauti na wafanyakazi wa taasisi zingine,na wamekuwa wakionekana bora tu wakati kipindi cha kampeni na sensa ya watu na makazi.

Mwishoni kwa kumalizia,Katibu wa CWT kwa waalimu wa shule za msingi yeye alisema tu wanachotaka ni Mabadiliko,ije serikali nyingine labda itawajali waalimu kwa kazi zao ngumu na zisizo na overtime wala marupurupu.
 
Walimu hawawezi kumtosa mwalimu mwenzao JPM
 
Hao CWT nao wezii tu kama CCM, wanataka kujikosha hizi dakika za mwisho na kutafuta kick.....

Kwanza watwambie michango inamnufaishaje mwanachama...Nimeshuhudia MTU anastaafu halafu mwakilishi wa Chama la wezi Tanzania (CWT) ametoa elfu 50....I was like..seriously!!!! huyu mama ameanza kuchangia huko toka yupo kigoli, Leo hii anastaafu hata meno hana mnampa elfu 50 huku nyinyi mnajenga majengo marefu tusojua yanamnufaisha nani?

Tena wanyamaze kabisaa, wawakome walimu....Mara mia CCM kuliko hao Majambazi....Nina hasira.
 
Kwani umelazimishwa kubaki cwt si uachane nayo mkuu mbona wapo wengi sio wanachama
 
Walimu safari hii msikubali kabisa.... Jakaya alienda kuaga wasanii na kuwapa posho then nyie mnaachwa kama waji.nga tu
 
Tumewazowea!! Kila ikikaribia uchaguzi mnakuja na mikwara mbuzi
 
Kada ya UALIMU Tz, ni kada ambayo ni rahisi sana kudanganywa na watawala. Haya maumivu yao yamekuwepo tangu zamani sana bila kupata utatuzi..... Kesho kutwa tu wataitwa na tume ya Uchaguzi na wakipewa posho ya siku moja au mbili kwa semina wanasahau kila kitu. Siwatukani waalimu ila huu ni ukweli, nimezaliwa na waalimu, nimelelewa na waalimu lakini ukweli lazima usemwe!!!!
 
CWT nyie wahuni tu? mnatukata pexa nying 2kistafu mnatupa blanket ujinga huu? bora CCM kuliko chama hichi bora mkae kmya
 
CCM hawafai...

1: Wamedangaya wafanyakazi wote, hasa WAALIMU...MADAKTARI hadi kuwang'oa meno

2: Imewapiga wana habari hadi kuwaua wengine, eg Mwangosi

3: Imewapiga Mama zetu, mama ntilie, boda boda, na machinga kama mbwa vile...

4: CCM wanatumia polisi kupiga watu mabomu, sbb tu hawaipendi CCM...

5: CCM imeua uchumi wetu, imemaliza TEMBO, imeharibu maisha yetu, UMEME umekuwa ghali sbb ni IPTL...ikazaa na ESCROW na capacity charges tshs 6,000 kila mwezi kwa kila mtumia umeme, huu ni wiziiiiiiiii...

6: ELIMU, MAJI, MADAWA ni za kubahatisha... hakunaa sehemu nyingi...wameua Elimu, Elimu imekuwa ANASA... maskini hawana lao

7: CCM wametufanya wajinga, kwani MTAJI mkubwa wa CCM ni UJINGA...!!
 
Hivi walimu shemeji yenu anawaachaje? Hajaitisha hata sherehe ya kuwaaga? Ama kweli nyie hamna umhimu wwt kwa serikali ya CCM...wenye umhimu ni wasanii wa bongo fleva!???
 
Pamoja na hilo.....
Nyie walimu mngekataa kwanza kutumika na NEC kwenye harakati uchaguzi... Make kule mnakuwa kama rubber stamp ya ushindi haramu wa CCM...
 
Hata Hivi Watanzania Tunawashangaa Mmechelewa Kushtuka Na Nyinyi Ndio Mliolifikisha Hapa Taifa Letu Na Kama Nilaana Bas Iwe Juu Yenu, Kwasababu Uwizi Wa Kura Wote Nyinyi Mnahusika Kwasababu Asilimia 80 Ya Mawakala Wa Selikali Mnatumika Walim Kwahiyo Kila Uhuni Unaotumika Nyinyi Mnahusika Pengine Hata Hicho Kilio Chenu Kutokusikilizwa Ni Pigo Kutoka Kwa Mwenyezi Mungu
 
Hao CWT nao wezii tu kama CCM, wanataka kujikosha hizi dakika za mwisho na kutafuta kick.....

Kwanza watwambie michango inamnufaishaje mwanachama...Nimeshuhudia MTU anastaafu halafu mwakilishi wa Chama la wezi Tanzania (CWT) ametoa elfu 50....I was like..seriously!!!! huyu mama ameanza kuchangia huko toka yupo kigoli, Leo hii anastaafu hata meno hana mnampa elfu 50 huku nyinyi mnajenga majengo marefu tusojua yanamnufaisha nani?

Tena wanyamaze kabisaa, wawakome walimu....Mara mia CCM kuliko hao Majambazi....Nina hasira.

Si ndio maana umeanzishiwa bank yako dada? Au hujui benki ya waalimu itakunufaisha? Kwanza umeshanunua hisa yako? itafikia mahali chama kitajiweza hata serikali hawatawasumbua tena.
 
CWT acheni siasa walimu tupo weng rukwa huku tutamuunga magufuli tatzo viongoz wa juu CWT ni tatzo na wananunuliwa xana
 
Huwezi kutofautisha CCM na CWT maana wote hao ni wezi. CWT hawana hoja kuelekea uchaguzi mkuu. Waendelee tu kukusanya michango ya wanachama wao na kujineemesha wao binafsi.
 
Back
Top Bottom