Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 464
- 687
Katika utamaduni wa siasa ya vyama vingi, kawaida ni kuwa na chama tawala na vyama vya upinzani. Katika hali isiyoyakawaida, hapa Tanzania, chama kikuu cha upinzani ndio kimepata wapinzani.
Ni rasmi sasa CHADEMA inapingwa na wana CHADEMA wa kundi la G55, Chama Cha Mapinduzi, vyama vya upinzani, Msajili wa vyama vya siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasiojulikana na wanaojulika. Kwa kifupi CHADEMA ndicho chama kinachopingwa zaidi Tanzania.
Jambo hili sio tu kwamba sio la kawaida katika utamaduni wa siasa ya vyama vingi, lakini pia linatafakarisha sana. Nini msukumo wa muungano huu wa makundi yote niliyoyataja dhidi ya CHADEMA? Chama ambacho hakina dola wala hakijaridhia kanuni za uchaguzi 2025 ili kishiriki uchaguzi?
Kwa wafuatiliaji wa mwenendo wa matukio ya kisiasa hapa nchini; kutoa matamshi yenye mwelekeo wa kuegemea CHADEMA na sera zake, ni independent risk factor ya kupigwa, kukamatwa, kutekwa au kupotea kama tulivyoshauriwa na Mh. Spika kukuita hivyo. In fact kama hujawahi kusimamiwa nyuma na polisi wakiwa na bunduki na mabomu ya machozi, njia rahisi ya kupata uzoefu huo ni kuhudhuria mikutano ya CHADEMA.
Kwayeyote aliyefuatilia mahojiano ya Kigaila na Odemba pamoja na press conference ya Mrema na Wenzake atakubaliana na mm kuwa, G55 wana nongwa na uongozi mpya wa CHADEMA kuliko walivyowahi kuwa na nongwa na CCM. Sijaingia kwenye moyo wa Kigaila, ila kwa maneno aliyoyasema mwenyewe alipohojiwa na Odemba, hana tatizo kabisa na kesi ya uhaini ya Lisu, ila alikuwa na tatizo na kesi ya ugaidi ya Mbowe. Chuki ya kiwango hiki inaacha walakini mkubwa.
Mm siamini kama CHADEMA imekuwa tishio kiasi hiki. CCM haihitaji rafu hata moja kushinda uchaguzi. Kwa CCM kuendelea kuhangaika na CHADEMA sio tu kunayapa madai ya CHADEMA uhalali ambao hauna msingi wowote bali pia kunawapa nafasi CHADEMA kutafuta public sympathy kitaifa na kimataifa. Lingelikuwa ndani ya uwezo wangu, ningesawazisha uwanja, uwe sawa kwa wote, nione huo ushindi wa CHADEMA unatokea wapi?
Tusisahau, vyama vingi lilikuwa ni Azimio la halmashauri kuu ya CCM, na kwakweli CCM kama chama tawala ndio mnufaika mkubwa wa upinzani imara. Gharama pekee ya kufaidi faida za upinzani ni kuwavumilia wapinzani, na hata wanapovuka mipaka ya kisheria nguvu inayotumika kuwakabili isivuke mipaka ya kisheria ili kuweka tofauti ya chama cha ukombozi na chama upinzani.
Nchi hii ni yetu sote, na sote tunawajibu sawa katika kutoa mchango wetu kuijenga. Ni wajibu wa upinzani kutoa constructive criticism, siyo matusi na uchochezi. Kadhalika ni wajibu wa CCM, kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na sheria za nchi bila upendeleo.