Hivi karibuni chama cha soka Tanzania kiliufunga uwanja wa Jamhuri wa Morogoro kuwa haufai kuchezewa mechi za ligi kuu Tanzania bara.Mashariti waliopewa ni kuufanyia marekebisho ili uwe katika kiwango cha ubora unaotakiwa.Lakini katika hali ya kushangaza uwanja huo umefunguliwa ukiwa katika hali ile ile ya ubovu.Mkoa mzima ulishindwa kabisa kununua mabati yasiopungua kumi ili wajengee au wafunike sehemu wanapokaa makocha na benchi la ufundi.Mabanda hayo hadi sasa hayana mabati juu na hivyo kama kuna mvua au jua kali basi wanaokaa pale cha moto watakiona.Hata uwanja wenyewe ndani bado wa ovyo kabisa haufai kuchezewa ligi kuu.Hivi ni kweli kabisa mkoa mzima hauna uwezo wa kununua mabati kumi ya kufunikia mabanda hayo?Hii ni aibu ya kufungulia mwaka 2o17 kwa wana Morogoro wote.Na je chama cha soka Tanzania kilikula MLUNGULA kiasi gani hadi kuruhusu tena uwanja huo uanze kutumika ukiwa bado mbaya kiasi hicho.Hii ni aibu kubwa wa chama cha soka Tanzania na chama cha soka Morogoro kushindwa kurekebisha uwanja huo.