Chama cha Mapinduzi kishtakiwe rasmi UN

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,944
3,820
Ni wakati muafaka Vyama vyenye ushawishi mkubwa kwa wananchi wajiwezeshe na kujipanga ili kuishataki CCM katika Umoja wa Mataifa.

Tunajua ipo kesi au madai ya WaZanzibari kudai nchi yao ambayo yamefikia mahala pazuri,ila hilo halitoshi kuona haki za binadamu zinakiukwa na wananchi wengi wamekuwa wakiuliwa na kufungwa na kutekwa. Vithibitisho vipo vingi tu na wengine hadi leo wapo makolokoloni na wengine ndio hao kina Mbowe.

Chaguzi za Tanzania zimekuwa zinapoteza wananchi kila zinapofanywa na wahusika wakuu ni CCM na inaonekana hakuna linalofanywa labda hii njia ya Mheshimiwa Tajiri wa madini alipowaondolea uvivu inaosemekana wamemdhulumu.

Ni bora wananchi wasifikishwe huko kwenye kuondoleana uvivu maana hili la Hamza linaitwa Act Alone (AA),hii ni stage mbaya sana maana ni zaidi ya kujitoa muhanga.

Sasa sasa ni shauri bora kufungua hati ya Mashtaka huko UN japo hakuna litakalo kuwa lakini iwepo tu kama ya WaZanzibari. Ili kuepepukana na AA.
 
AA inaweza kupoteza hata wasio na hatia maana wale waliohamziwa sijui kama ndio wahusika wa dhulma zinazosemekana alitendewa Hamza.
 
Back
Top Bottom