Chama cha Mapinduzi kimeamua kuanzisha Bank

Chama cha Mapinduzi kimeamua kuanzisha Bank

Pwito

Senior Member
Joined
Mar 28, 2012
Posts
180
Reaction score
40
Wadau hii imekaaje, maana namsikia mwakilishi kutoka CCM Vijana akilizungumzia hapa star TV
 
Nilipata kufanya kazi bank, na wakati wa induction wakufunzi walisema kwa kurudiarudia sana kuwa "A bank is an institution built on TRUST".

Kwa kuzingatia hilo nachelea kuwatahadharisha ccm juu ya uamuzi wao huo, maana wanaweza wakaja kulia kilio cha mbwa.
 
Nauliza tu jamani je, hizi ni mojawapo ya kazi za chama cha siasa? Au ni onlyn in Tanzania.
 
Sasa ajira tutapata au????????
 
Wajifunze kwenye saccos kwanza na vicoba wakiweza ndio wafikirie bank!maana mikopo yoote watapeana wao kwa wao wengine kanyaboya tu
 
Naona ccm badala ya siasa kupita pembeni wanaanza kuingia kwenye ufisadi kwa staili nyingine ya mgongo wa bank fanyeni siasa ccm bank kaz kubwa, hapa tu hamna bank mnatukana, je mkiwa na bank c mta ua!!!!!!!!!!!!!
 
....labda ndio wanajiandaa kuondoka madarakani!Vitega uchumi muhimu na ni muhimu zaidi kuviweka kabla ya kustaafishwa.
 
Let us wait and see, huenda ikawa siasa za njozi. Maana mara nyingi matamshi ya viongozi wetu hawa badala ya kupeleka maamuzi ya chama mtu anapopata nafasi ya kuongea anasema kile anachofikiria bila hata kuangalia mapokeo yake kwa wananchi yatakuwaje.

We are now used to such statements. Kauli hizi katika hali ya kawaida bado zinamitazamo ya kijima-jima vile, bado wanaozitoa wanadhani wananchi bado wapo katika enzi hizo.
 
Itakuwa kama sukita. Haijawahi kuwa na mradi wowote endelevu zaidi ya mradi wa ufisadi, rushwa na wizr wa kura.
 
Itafilisika baada ya muda mfupi kama walivyoifilisi SUKITA.
 
Watu walioshindwa kusimamia mradi wa mabasi ya shule uliokuwa na dala dala zisizozidi 20 ndio leo wataweza kuendesha bank?

Na waanzishe tu mimi nitakuwa wa kwanza kuchukua mkopo maana najua hiyo bank itakufa kabla sijaanza kulipamkopo!
 
amesema itawakopesha vijana wote bila ubaguzi wa vyama. Je anajua kuwa kuna benk zina miaka mingi lkn zimeshindw kukopesha kila mhitaji. Ccmvijana mnazo ngapi?
 
Labda kama wanaongeza tawi lingine , mbona wanayo bank kubwa sana inaitwa BOT ! Mmesahau mambo ya EPA ?
 
Back
Top Bottom