Chama cha makahaba chasajiliwa rasmi

Chama cha makahaba chasajiliwa rasmi

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,113
Reaction score
34,953
rais_banda.jpg
Rais wa Malawi,Joyce Banda
“Muda wa kujadili kwa pamoja matatizo yanayowakabili ndio huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama vinavyowabana na kwamba mnahitaji kupata huduma nzuri za kulinda afya zenu na afya ya uzazi bila kipingamizi,” alisema mwanasheria wa haki za binadamu, Chrispin Sibande alipokuwa akizungumza na kundi la wateja wake wapatao 50 ambao ni makahaba.

Malawi
ZAIDI ya makahaba 2000 nchini Malawi wameungana kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayoyapata na kuboresha mazingira ya afya, baada ya kuzindua rasmi chama cha kuwatetea juzi.

Kundi hilo linaundwa na vyama visivyo vya kiserikali vya ndani na nje ya nchi hiyo, ikiwa ni la kwanza kutambuliwa rasmi na kupewa usajili katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambapo biashara ya ukahaba inaharamishwa.

“Muda wa kujadili kwa pamoja matatizo yanayowakabili ndio huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama vinavyowabana na kwamba mnahitaji kupata huduma nzuri za kulinda afya zenu na afya ya uzazi bila kipingamizi,” alisema mwanasheria wa haki za binadamu, Chrispin Sibande alipokuwa akizungumza na kundi la wateja wake wapatao 50 ambao ni makahaba.
Makahaba nchini humo mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na Polisi hata kwa makosa madogo ikiwemo kukutwa wakiwa wamekaa bila kazi, ambayo pia huambatana na kutozwa faini.

Miaka mitatu iliyopita, makahaba 14 walikamatwa na Polisi na kulazimishw akupimwa Virusi vua Ukimwi (VVU) na wote kukutwa wakiwa wameathirika, ambapo walishtakiwa mahakamani kwa kufanya biashara ya ngono huku wakijua kuwa wana maradhi hayo ya kuambikiza, ambapo walichajiwa Dola7 kila mmoja na kuachiwa huru.
Baadaye waliishtaki Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia mambo yao binafsi katika kesi ambayo hadi sasa bado inasubiri kusikilizwa katika mahakama kuu.

Wataalamu wa afya nchini humo wanasema maambukizi ya Ukimwi miongoni mwa makahaba hao yanafikia asilimia 70. Mawakili wao wanasema kuw awanatumiani umoja wao utawasaidia pia katika kuwaelimisha kuepuka maambukizi hayo.
Chama cha makahaba chasajiliwa rasmi - Habari - mwananchi.co.tz






 
Hii dunia inapolekea si pema hata kidogo mambo mengine yanasimanzisha roho
 
Hii dunia inapolekea si pema hata kidogo mambo mengine yanasimanzisha roho
bibieqSwts dunia yetu inaongozwa na mashetani wakubwa wawili Mmarekani na muingereza wao ndio

wanatupangia sisi wakisema tuhahalalishe Ushoga itabidi tukubali tukikataa na Misaada ya Pesa tunanyimwa wakisema tuhalalishe

mambo ya kusagana itabidi tukubali tukikataa wanatunyima misaada yao ya Pesa uchwara hii ndio dunia yetu chafu. Watu

wamemsahau Mungu Muumbaji wamekumbatia mungu Pesa na Uongozi ndio hao miungu 2 wanayoiongoza hii dunia

yetu, ukiwa na pesa basi hata kuuwa mtu unaweza ukiwa masikini tabu tupu utakachoambiwa wewe itabidi ufuate tu

ukitaka usitake. Itafika wakati na sisi Wa-Tanzania tutaruhusu sheria ya hiyo Ukahaba tukitaka tusitake.
 
Huyu mama is desperate kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ujao kwani kumbukeni kwamba ingawa katiba ya nchi yao inasema Vice President automatically anachukua kiti rais akifariki, bado yeye alipata wakati mgumu kuchukau nafasi hiyo, hasa kwa siasa kwamba ni mwanamke; Ndio maana sasa anajaribu kila njia ili awe favourite ya wananchi, including uchokozi wa mpaka na Tanzania;
 
good move. tatizo sisi waafrika hatujaamka usingizini. tunapenda sana kuweka utashi wetu kwa watu wengine. mungu alimuumba binadamu na kumpa uhuru wa hufanya lolote apendalo.
 
Back
Top Bottom