Chama cha kutetea wanaume chaanzishwa.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha kutetea wanaume chaanzishwa..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sosoliso, Jun 19, 2012.

 1. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Chama cha kutetea haki za wanaume Tanzania (TAMERA), kimeanzishwa ili kuweka usawa ikiwamo kuondoa dhana potofu inayoendelea kupandikizwa kwenye jamii na mitandao mbalimbali kuwa, mwanaume ni bingwa wa kuendesha mfumo dume na unyanyasaji dhidi ya wanawake.

  Katibu mkuu wa TAMERA Anthony Sollo, alisema wanaume wameamua kuanzisha chama hicho kutokana na kuchoshwa na tuhuma mbalimbali dhidi yao, ikiwamo kutupiwa virago kwenye majumba yao, kunyimwa unyumba na kukatwa mishahara baada ya kushtakiwa kwa waajiri wao.

  Sollo alisema pia hatua ya kuanzishwa kwa chama hicho ni kutocikilizwa malalamiko ya pande zote, ili kujua kama sababu hizo zina ukweli au la lakini zinaporipotiwa huanza kuchukuliwa hatua mara moja. "taarifa ambazo hutolewa na wanawake huwa hazina mtu wa kujibu kwa vile wanaume hawakuwa na chombo cha kutetea haki zao," alisema Sollo na kuongeza kuwa, makao makuu ya TAMERA yatakuwa Mwanza.

  Alisema wamejipanga vizuri kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanaume nchini na kwamba kuna mawakili mahiri watakaokuwa wanafuatilia matatizo mbalimbali.

  Katika tukio jingine, mlezi wa chama hicho Khamis Mgeja ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation, alitoa Sh5 milioni kuunga mkono harakati hizo ili chama kiweze kuenea haraka.

  Chama hicho kinaongozwa na Juma Kombo (meneja miradi), Khatibu Mgeja (katibu uhamasishaji) na Irine Msangi (mjumbe wa Mkutano Mkuu)..

  Source: Mwananchi
   
Loading...