Waswahili wanasema kwamba uwema wa mtu unanzia nyumbani kwake, halafu unasambaa nje ya nyumba yake, ofisi za chama cha cuf makao makuu zipo Buguruni karibu kabisa na shule ya msingi Buguruni, ukienda katika shule ya msingi Buguruni A utakuta kuna darasa ambalo lilijengwa kwa msaada wa wamarekani ili watoto wa shule ya msingi buguruni waweze kusoma computer, hao wamerekani walitoa hicho chumba pamoja na computer zake, cha ajabu mlm mkuu wa shule hiyo ameamua kuwanyima haki hiyo watoto kwa tamaa zake za pesa na kumkodisha mtu binafsi ambaye anafundisha computer course kwa watu wazima. Kwa taarifa zilizopo viongozi wa cuf ktk eneo hilo wanazo taarifa za suala hilo ila wameamua kufumbia macho sijui kwa maslahi ya nani. Wanajanvi wenzangu kweli kuna chama hapo? Usiniulize nimepata wapi hizo taarifa nenda kashuhudie mwenyewe. NAWASILISHA.