Chama cha CHAUMMA chaendelea kujikusanyia wanachama wengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha CHAUMMA chaendelea kujikusanyia wanachama wengi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHAUMMA, Aug 2, 2012.

 1. C

  CHAUMMA Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WANAJF,

  Chama Kipya chenye usajili wa Muda CHAUMMA kimeendelea kujikusania wafuasi na wanachama wengi Dar Es Salaam na mikoani. Kwa Dar Es Salaam pekee wiki ya kwanza wanachama zaidi ya 45,000 walichukua kadi.Tunaamini zoezi litakamilika mapema kwani ni wanachama 2000 tu wanaohitajika na msajili wa vyama vya siasa kwa mikoa 10 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kupata usajili wa kudumu

  Maandalizi kabambe yanapamba moto. Tovuti ya chama iko mbioni na maandalizi yote ya usajili kwa njia ya electronic kwa walioko nje ya nchi yanaendelea

  Karibu CHAUMMA!
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Eti mkuu ni kweli hiki chama ni cha Kafulila?
   
 3. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mtahangaika sana lakini mwisho wa siku Tanzania inahitaji vyama viwili tu.

  TUMBIRI (Tunduru, Ruvuma - Tanzania),
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 4. C

  CHAUMMA Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo ni porojo za mitaani tu.Kafulila anakaribishwa na hata wewe unakaribishwa CHAUMMA

  Tumbiri,

  Usiwasemee watanzania.Uliwakusanya wapi watanzania ndio wakakueleza hayo? Naomba uendelee kufanya utafiti.Watanzania wanatafuta chama chenye dira sahihi na sera za kuwaletea ukombozi wa kweli.CHAUMMA tunaamini Watanzania ndiyo msingi wa mamlaka yote na kama chama cha siasa usipopata sapoti ya watanzania basi utapotea kama vilivyopotea vyama vingine au kujisalimisha chama tawala kama vilivyofanya baadhi ya vyama vya upinzani

  Hata uingereza na Marekani hakuna vyama viwili tu kama watu wengi wanavyofikiria.Chukulia mfano wa Uingereza,watu wengi hawakujua kwamba Uingereza kuna vyama zaidi ya Labour na Conservative hadi uchaguzi wao wa juzi walipoona chama cha Liberal democrats kilichoongozwa na Nick Clegg ambao walifikia hatua ya kuunda serikali ya pamoja na David cameron kutoka Conservative.Kiongozi wa upinzani Ed Milband anaendelea kufanya kazi ya kujenga nguvu ya pamoja na vyama vidogo ili apate platform nzuri ya kukiongoza chama chake uchaguzi ujao


  Tuwape watanzania haki na fursa ya kidemokrasia ya kuamua ni chama gani kisimame kuwapeleka katika ukombozi wa kweli

  Nitarudi baadae kidogo.Karibuni sana
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Rubbish
   
 6. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHAUMMA v/s ADC nyie wote wachumia tumbo ya vibaraka wa magamba.
   
 7. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unanikataza nisiwasemee Watanzania, mbona na wewe unawasemea? Na wewe uliwakusanya wapi watanzania wakakueleza hayo?

  TUMBIRI (Tunduru, Ruvuma - Tanzania),
  tumbiri@jamiiforums.com

   
 8. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Watazunguka sana cuf b hao
   
 9. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Lakini hatuna uhakika bado kama Chadema kita sustain kama chama kikuu cha upinzani au CCM kitaendelea kuishi katika zama mpya za ushindani. Mfano mzuri ni kwamba upepo wa sasa kisiasa ni uwajibikaji, na usimamizi wa rasilimali za taifa. Chadema wamefanikiwa sana kulipigia hili suala kelele hivyo kupanda chati katika medani za kisiasa, lakini cha ajabu ni kwamba, baada ya CCM kuanza kutekeleza yale ya chadema in the context of kuanza kuwa serikali inayowajibika, inayokemea ufisadi, CCM nayo inapanda chati. Now what does this tell you?

  Binafsi nadhani given the fact kwamba vyama vyote vya siasa (including CCM) havijitofautishi kiitikadi na badala yake based on personalities zilizopo kwenye chama huku kila chama kiki exploit upepo wa siasa wa wakati huo, bado kuna uwezekano mkubwa wa vyama vipya kuweza kufanikiwa, hasa kama vitasimamia itikadi inayouzika kwa wananchi in the sense kwamba kweli utekelezaji wake ni practical na can bring a social, political and economic change to the people; Karibuni sana CHAUMMA. Ni dhahiri mmeona ideological vacuum nayozungumzia vinginevyo msingepoteza muda wenu bure.
   
 10. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  huyu jamaaa mwenyekiti wa chaumma anaitwa athanas methusela ni mhitimu wa chuo cha usimamizi wa fedha,alishawai kugombea ubunge kibondo kupitia nccr mageuzi,ila kwa jinsi anvyoonekana hana ujanja wa kuanzisha chama, kunauwezekano mkubwa anatumiwa na rafiki yake wa karibu david kafulila(mb)asiye na chama
   
 11. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna sehemu nimesema kwamba tunahitaji vyama viwili tu ambavyo ni CCM na CHADEMA? Ninachopinga ni huu mtindo wa watu kukimbilia kuanzisha vyama vipya wakati tayari tuna vyama zaidi ya 20 vimesajiliwa. Hivi unataka kuniambia katika hivi vyote 20 hakuna chenye dira na sera za kuwakomboa watanzania na kuwapa ukombozi wa kweli?

  Tumepigania kuindoa CCM tangu 1992, miaka 20 sasa. Leo watu wanakuja na chama wakishindwa hata kuonyesha utofauti wa Chama chao na hivi vilivyopo zaidi tu kuropoka wao ndiyo wakombozi wa kweli. Kwamba wao hawana ukabila, ukanda wala ubabe. Hivi kuna chama cha upinzani kilichowai sema chenyewe siyo mkombozi wa kweli? Na kwamba ni cha ukabila, ukanda na cha wababe? Tuwaamini tu kwa maneno yao matupu? Hawa ndio wanarudisha harakati zetu nyuma.

  Nawashauri watafute vyama vilivyopo hivi sasa wanachokiamini wakiimarishe watuletee huo ukombozi. Kwanza kuanzisha chama kipya kwa sasa ni gharama sana, isitoshe uhai wa Chama cha Siasa ni zaidi ya kuwa na usajili. Kuna safari ndefu na ngumu hadi chama cha siasa kiaminiwe na wananchi. Kuna vyama vimesajiliwa tangu 1992 hadi leo havijawi pata hata mjumbe wa serikali ya mtaa, Kijiji na kitongoji iweje hivyo vinavyoanzishwa sasa?

  Tuwapinge wanaonzisha vyama vya siasa kwa sasa. Tuwaambie wachague kimoja vilivyopo wakiimarishe! Tukiwaona wana nia ya dhati tutawaunga mkono.

  TUMBIRI (Tunduru, Ruvuma - Tanzania)
  ,
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,833
  Trophy Points: 280
  Chauma ni chama kinacho hitaji ruzuku kwa nguvu. Kuna jipya gani mnalotaka ambalo halija semwa na vyama vingine?
   
 13. r

  rwazi JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunawatakia safari njema
   
 14. r

  rwazi JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mkuu ni chaumma kweli au chakijiko kwaajiri ya kuchotea ruzuku.

  Unadhani kuanzisha chama ni mchezo,lazima makamasi yatawatoka
   
 15. sikafunje.N

  sikafunje.N Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongereni... kaza buti
   
 16. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Waanzilishi wa mfumo huu wa demokrasia ( ulaya na Amerika) karibu wote wana vyama kati ya 2 hadi 3. Sisi tuna zaidi 20 for what? Nadhani tuviboreshe vyama visivyozidi 3 tu basi. Maoni yangu tu.
   
 17. a

  andrews JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​wazunguke koote chadema ndio mwiba wa ccm
   
 18. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hizi pumba pelekeni kwa mume wenu magamba!!!!hakuna chauma wala cha kijiko hapa....
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  mimi na chadema, chadema na mimi
   
Loading...