Chama cha BDP kimeshinda uchaguzi Botswana

Chama cha BDP kimeshinda uchaguzi Botswana

Kingdom Finder

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
1,118
Reaction score
1,397
Kwa wale mnaofuatilia uchaguzi katika nchi ya Botswana chama tawala kimeshinda na Dr Masisi ametangzwa kuwa ni Raisi chini ya BDP. Nipo hapa Botswana nikifuatilia uchaguzi huu na yafuatayo nimeyaona.

1. Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki kulinganisha na nchi nyingi za Africa. Kwa SADC imeonyesha mfano na ingekuwa vizuri hizi nchi wakajifunza kwa nchi ya Botswana.
2. Chama tawala kikifanya vizuri kinapata ridhaa kwa wananchi wake na hakuhitajiki nguvu nyingi kukirudisha madarakani. Upinzani ulikuwa mkubwa sana lakini hatukuona mahali chama tawala kilitumia nguvu au wizi wa kura.
3. Hakuna mtu aliyepigwa wala kupoteza maisha.
4. Hakuna askari aliyesaidia chama chochote kushinda.
5. Uchaguzi umefanyika kwa uwazi. Meaning Everything was transparent.

Wakati wa uchaguzi kulikuwa na amani sana. Vyama vyote vimepewa level ground ya kushindana bila kuoneana.

Demokracy ikifuatwa vizuri ina raha yake na unaifurahia. Hakuna chama kilichogawa chakula wala nguvu. Hatukisikia mahali watu wamehongwa. Huwezi kuamini kwamba sijaona hata askari anayetembea na silaha barabarani au magari ya washawasha kuwa stand-by. Amani imetawala wakati wote wa election.

Chaguzi nyingi zinatia aibu kwa kweli katika nchi zetu za Afrika ukilinganisha na huu wa Botswana. Mungu ibariki Botswana iendelee kufanya vizuri kwenye chaguzi zijazo labda nchi zetu za Afrika zitajifunza ili wawe na chaguzi huru na za haki kama huu.

Kulikuwa na Observers wa SADC na nchi nyingine ambao watatoa official report. Wale wa SADC amabao wametoka kwenye nchi zinazogandamiza demokrasia wamesema wanaona aibu kwa yanayofanyika katika baadhi ya nchi zao kulinganisha na waliyoyaona hapa Botswana.

Haya ndiyo niliyoyaona. Baadaye mtafute official reports kutoka kwa international observers. Watakuwa wameandika vizuri.

Ahsanteni.
 
Safi sana wale wagombea Mabeberu wameangukia pua

Imebaki Tanzania tutawanyoonsha kwenye sanduku wanaotumiwa na mabeberu
 
Mkuu nimefuatilia post zako kuhusu Botswana , inaelekea unampenda sana Rais wa sasa na chama tawala , na kama si hvyo basi Botswana inaongozwa na Yesu/Mtume M(S.A.W)...
 
Safi sana wale wagombea Mabeberu wameangukia pua

Imebaki Tanzania tutawanyoonsha kwenye sanduku wanaotumiwa na mabeberu
Hata usomi na kuelewa au labda mnasoma mkiwa under influence ya viroba.
Huoni kuwa akina Tanzania ndio walengwa wa kuvuguga uchaguzi wanaozungumziwa hapo. Please come to your senses.
 
Back
Top Bottom