Kaptula la Marx
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 981
- 449
Hali ya kifedha ya Chama cha ACT-Wazalendo ni taabani, Kaptula La Marx anaweza kuthibitisha. Kwa mjibu wa taarifa kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya ACT-Wazalendo akaunti za chama hicho kichanga zina salio la fedha kiasi cha shilingi millioni kumi zikiwa ni ada ya viti maalum pamoja na fedha zilizoingizwa kimakosa katika akaunti hiyo ya kampeni kutokana na ada ya madiwani. Habari zaidi kutoka ndani ya ACT-Wazalendo zinasema kuwa mgombea urais kupitia chama hicho, Mama Anna Elisha Mgh'wira anatarajia kuendelea na ziara yake katika mikoa ya kusini ambako viongozi wa hiyo mikoa wameandika barua kudai hizo pesa ili waendelee na maandilizi. Nakala ya barua hizo mwandishi anazo lakini hataziweka hapa kwa sasa kwa sababu sio vizuri kumaliza risasi zote kwenye bunduki kwa wakati mmoja. Mwandishi ataendelea kumwaga risasi moja baada ya nyingine, na hatua kwa hatua ili kuumbua vikundi vya kitapeli na kilaghai kama hiki cha ACT-WAZALENDO na mawakala wao.
Kutokana na ukata huo wa fedha, timu ya mikakati ya kampeni ndani ya ACT-WAZALENDO imeshauri ziara za mgombea Urais kupitia ACT-WAZALENDO mama Anna Elisha Mgh'wira ziendelee ili kiasi cha fedha kinachofikia milioni 7 kitolewe katika fedha hiyo ya milioni kumi iliyoko kwenye akaunti maalum kwa ajili ya kampeni. Kwa mjibu wa mnyetishaji wangu kutoka jikoni ndani ya ACT-WAZALENDO, kiasi cha milioni 3 kilichosalia kimetolewa kwa ajili ya services ya magari ya kampeni ili kesho mgombea wa Urais na timu yake waondoke kwenda kuendelea na kampeni huko mikoani. Kaptula La Marx hajaweza kuthibitisha kama kiasi cha milioni 7 kinatosha kuandaa mikutano mingapi yenye hadhi inayotakiwa na ikiwa hiyo fedha itatumika kwa siku ngapi. Inahitajika bana matumizi kali kweli kweli. Mgombea wa Urais kupitia chama hicho cha ACT-WAZALENDO anatarajia kuendelea na ziara yake mikoa ya kusini, hususani Lindi, Mtwara na Ruvuma; na akimaliza huko ataelekea Zanzibar. Chanzo changu kilithibitisha
Kuvuja kwa taarifa hizi za ACT-WAZALENDO kuwa taabani kifedha kunakuja ikiwa ni baada ya mazungumzo yao na chama dada cha CCM kutozaa mafanikio. Mnyetishaji wangu kutoka jikoni ndani ya CCM na Ikulu amenithibitishia kuwa "Makubaliano yetu na Kuongozi Mkuu wa ACT-WAZALENDO, Mh.Zitto Kabwe a.k.a Supreme Leader au Ayatollaaah, yalikuwa kwamba CCM itaisaidia ACT-WAZALENDO gharama za kampeni kama watasimamisha mgombea wa Urais ili kupunguza makali ya nguvu kubwa za mgombea wa CHADEMA, anayewakilisha pia UKAWA ndugu Edward Lowassa". Hata hivyo, mnyetishaji wangu huyo amesema CCM wamegundua kuwa uwepo wa mgombea wa Urais kupitia ACT-WAZALENDO hakujaleta athari zozote kwa UKAWA kama CCM walivyotarajia. Kutokana na hali hiyo, CCM wameendelea kusita katika kutoa fedha hizo ambapo makubaliano ya awali ilikuwa watoe kiasi cha milioni 800 katika awamu ya kwanza ya kampeni; na kiasi cha milioni 800 kilichobaki kitolewe katika awamu ya pili ya kampeni.
Hata hivyo, mpaka wakati wa kuandika andiko hili, mwandishi hakuweza kuthibitisha ni asilimia ngapi ya kiasi hicho cha fedha imetolewa katika awamu ya kwanza ya kampeni mpaka sasa. Mawasiliano kwa ajili ya kupata kiasi kamili kilichotolewa mpaka sasa yanaendelea ndani ya CCM na ACT-WAZALENDO. Kutokana na mkwamo huo, mnyetishaji wangu ndani ya ACT-WAZALENDO amenithibitishia kuwa viongozi wakuu wa wa chama hicho wameamua kuandaa fundraising dinner itakayofanyika tarehe 2th Oktoba, 2015 ili kuokoa jahazi. Mpaka sasa maandalizi ya fundraising au harambee hiyo yanaendelea na yako katika hatua nzuri. Mmoja wa vigogo ndani ya ACT-WAZALENDO, amenithibitishia kuwa kama hali itaendelea kuwa ni ya ukata kama ilivyo sasa, itaathiri kwa kiasi kikubwa kampeni za chama hicho katika ngazi zote za urais, ubunge na udiwani.
Kigogo huyo amewalaumu pia viongozi wenzake kwa kitendo chao cha kukaidi ushauri wa kitaalamu uliowataka wasisimamishe mgombea wa Urais, na badala yake wajikite kwenye majimbo na udiwani. Aidha, ushauri huo wa kitaalamu uliotolewa na watalaamu wao uliwataka ACT-WAZALENDO wasimamishe wagombea wachache wa ubunge na udiwani hususani katika maeneo ambayo chama chao kina nguvu kubwa kama Kigoma na baadhi ya maeneo katika mikoa ya Katavi, Tabora na Kagera. Lakini kiongozi mkuu wa chama hicho, alikataa katakata kwa madai kuwa tayari alikuwa ameshaongea na viongozi wakuu wa CCM waliokuwa wamemhakikishia kumpa fedha za kampeni. Pamoja na viongozi wakuu wa chama hicho kujitapa kuwa ndicho chama cha pili kuwa na wagombea wa Ubunge wengi baada ya CCM, lakini kutokuwa na rasilimali za kutosha ili kugharamia kampeni hizo kutakifanya chama hiki kipoteze hata vile viti ambavyo kingeweza kuvipata kama kingekuwa na wagombea wachache.
Kaptula La Marx (Jikoni muda huu)