Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
CHAMA CHA AAFP WILAYA YA ARUMERU KINATANGAZA KUJITOA KATIKA MCHAKATO WA UCHANGUZI WA UBUNGE NA MADIWANI KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI ΚΑΤΙΚΑ MAJIMBO YA ARUMERU MASHARIKI NA ARUMERU MAGHARIBI
Chama cha AAFP wilaya Arumeru, Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kujitoa katika mchakato wa uchaguzi wa wabunge, na madiwani kwa majimbo ya Arumeru mashariki na Arumeru Magharibi kwasababu zifuatazo.
1. Wasimamizi wa uchaguzi kushindwa kutupatia orodha ya vituo vya kupigia kura katika majimbo ya Arumeru mashariki na Arumeru Mgharibi. Kinyume na kitabu cha maelekezo kwa vyama vya siasa na wagombea, Uchanguzi wa Raisi, wabunge na madiwani ya mwaka 2025. Sura ya saba kifungu No 7.1.1 jambo ambalo halikufanyika katka majimbo ya Arumeru mashariki na Arumeru magharibi
2. Kutunyima haki ya kua na mawakala kwenye vituo vya kupigia kura siku ya kupiga kura kwa kutokutoa taaarifa yoyote ya uapishwaji wa mawakala siku saba kabla ya tarehe ya uchaguzi, Kinyume na sheria ya uchanguzi ya 2024 kifungu 77 {1} na {2}.
Pamoja na kwamba tuliwasilisha malalamiko yetu tangu tar. 24/10/2025 lakini bado wasimamizi wa uchanguzi katika majimbo haya wamekaa kimya bila majibu.
Kwa sababu hizo wagombea wetu wameamua kujitoa kwasababu wanaamini hakuna haki itakayotendeka katika uchuguzi huu. Badala yake chama kitapiga kwa nguvu zote na kutafuta haki mahakamani kama hatuta sikilizwa.
Katibu AAFP Arumeru
Katibu wa AAFP Mgina Ibrahim Mob no. 0789166567.
Katibu wa AAFP Mgina Ibrahim Mob no. 0789166567.
==============================
UPDATES: AAFP YATOA UFAFANUZI WA TAARIFA HIYO...
Akifafanua kuhusu taarifa inayoonesha AAFP imejitoa katika Uchaguzi Mkuu 2025 ngazi ya Ubunge na Udiwani Jimbo la Arumeru Mashariki na Magharibi, Katibu wa AAFP, Mgina Ibrahim anasema:
Ni kweli tuna dhamira hiyo ya kujitoa kwenye Uchaguzi ngazi ya Ubunge na Udiwani kutokana na kutotendewa haki.
Tumewasilisha malalamiko yetu kwa INEC na hawajatujibu mpaka sasa, hivyo dhamira yetu ipo palepale.
Suala la kujitoa lina taratibu zake ikiwemo kwenda Mahakamani na kuwasilisha nyaraka rasmi za kufanya hivyo, sisi bado hatujafanya huo mchakato.
Suala kama tutafanikiwa au la ndani ya muda huu uliosalia kabla ya Uchaguzi Mkuu hatujajua, lakini hata kama itatokea hatujafanikiwa tutaenda Mahakamani baada ya Uchaguzi Mkuu, hatuwezi kukubali kutotendewa haki.