comrade_kipepe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2019
- 6,446
- 11,504
"Nabii" ni neno la Kiswahili lenye maana ya mjumbe au msemaji kwa niaba ya Mungu
Chalamila anamuweka samia kundi moja na watu kama Yohana Mbatizaji na wakina Musa.
Hapa ndio wanaosema hakuna Mungu wanapokua na point, Kama kweli Mungu yupo, kwa damu aliomwaga anaruhusu vipi hizi dharau ziendelee?!
Ngoja tuone.
======
Ametoa kauli hiyo leo, Machi 3, 2026, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa matanki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
Soma Rais Samia: Wizara ya Nishati iimarishe akiba ya kimkakati ya mafuta ili kujilinda dhidi ya misukosuko ya siasa za kidunia
Chalamila amesema kuwa miradi mikubwa kama hii mara nyingi wananchi wa kawaida hudhani haiwahusu, lakini kwa muktadha wa matukio ya dunia, umuhimu wake ni mkubwa kuliko inavyodhaniwa.
“Mheshimiwa Rais unapotekeleza miradi kama hii ni rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuhisi kwamba mradi huu sio wa watu. Mtu wa kawaida akiangalia anaweza kudhani haumhusu yeye, lakini Mheshimiwa Rais wewe umekuwa kama nabii. Kwa yale yanayoendelea duniani leo, unaweza kuona hatari ya taifa kukosa maghala yanayomilikiwa na Serikali.” amesema