Chakula cha mama lishe(Mama ntilie)

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,051
12,950
Kiukweli nina miaka mingi sana sijawahi kula kwa mama lishe.
Kiuna sababu nyingi zinasababisha sili kwa mama lishe ikiwemo usafi na ubora wa chakula na mazingira ambayo hawa mama zetu wajasiriamali wanaandalia chakula.

Lakini kwa bahati nzuri au mbaya leo niko mahali sasa tumeenda kula na jamaa yangu mgahawani bahati mbaya tukakosa chakula tulichokitaka, hatua chache toka mgahawani hapo kuna vibanda vya mama lishe kibao, jamaa yangu akanishauri kwa nini tusile kwa mama lishe nikamkatalia kwa grounds nilizozisema hapo juu na ukizingatia kipindi hiki cha mvua unaeeza kupata kipindupindu bure, ila badae nikaamua kwenda kula kwa mama lishe.

Kilichonishangaza ni kwamba nikichokua nawaza kwa miaka mingi sicho nilichokikuta, mama kapika chakula kizuri sana, aina nyingi za mboga,nyama,dagaa,mlenda,mchicha,maharage,kachumbari.kisamvu.
Kilichonishangaza zaidi ni bei ya chakula chake, chakula kizuri na chenye ubora akadai kila mtu elfu 2 chakula ambacho ukienda migahawa ya kawaida si chini ya elfu 4.

Nimegundua kua kumbe watu wanokula kwa mama oishe wanafaidi sana, chakula poa bei poa.

Serikali iangalie jinsi ya kuwawezesha hawa kina mama, wanafanya biashara katika mazingira magumu,watengewe maeneo mazuri ya biashara zao na wasisumbuliwe na mamlaka za miji. Binafsi nimeufurahia sana msosi wa mama lishe, siku moja moja ntakua nakula.
 
Huwa wanapika chakula kizuri Sana, ila mazingira wanayofanyia shuguri zao ndizo zinazowarudiisha nyuma. Wanatakiwa pia kuacha kutumia vyombo plastick mfano: Sahani, bakuli Na vikombe vya chai, waache pia kutumia vijiko vya hadhi ya chini vile vyepesi. Wawe na maji ya kutosha kuoshea vyombo, alau wakirekibisha hayo itakua inafaa Kula kwao.
 
Back
Top Bottom