Chai ya kijani ndio ile ya mchaichai au?

zamuhalelu

Senior Member
Oct 5, 2017
140
131
Habari wana jf naomba kujuzwa

jee hivi chai ya kijani(green tea) ndiyo ule mchai chai unaopatikana sehemu nyingi ambao ukiuchemshia na maji chai inabadilika rangi au chai ya kijani ni ipi. ??
 
Kuna majani yanaitwa green tea
Kiongozi nilikuwa napiga sana mchai chai nikijua ndo hyo daaaah mwisho mkojo nao unasadifu rangi ya mchai chai kumbe sioo kiongozi doooh...

Hii grean tea naipata maduka gani?
 
Green tea hutengenezwa kutokana na mti wa kawaida unaotumiwa kutengeneza majani kama yale tunayotumia kila siku. Tofauti yake na majani ya kawaida ya chai ipo katika utayarishaji au utengenezaji wenyewe kiwandani. Zipo aina nyingi za chai mfano ni hii green tea, black tea(ambazo ni zile za kawaida kama chai bora, greenlable, tausi nk hapa kwetu), pia kuna white tea, yellow tea nk. Hivyo kimsingi chai hizo zote hutokana na mti mmoja tu uitwao kwa jina la kisayansi Camellia sinensis. Tofauti huja wakati wa uchakataji ambapo kila aina ya chai ina viwango tofauti vya uchakataji.

Hatua ya uchakataji iitwayo Oxidation ambapo chai hupashwa joto kali ndiyo huifanya chai kuwa na rangi aidha kijani(green), yellow au white. Na kwa green tea, yenyewe mchakato huu hufanywa kidogo sana na ndiyo sababu utakuta chai hii haipotezi ile rangi yake ya asili yaani kijani, wakati chai ya kawaida(black tea) yenyewe hupashwa joto kali(higher oxidation) mpaka kubadilika rangi yake ya asili na kuwa black(nyeusi).

Inasemekana chai ya kijani ina faida nyingi kiafya, na hutumiwa sana na Wachina, Wajapani na watu wengi kutoka bara la Asia. Green tea kwa hapa Tanzania inapatikana maduka mengi na super markets ila watu wengi hawajui, hudhani green tea ni kitu tofauti sana na majani yale ya kawaida. Paketi zake zimeandikwa Green Tea na karibu kampuni zote zinazotengeneza majani ya chai zina brandi zao za green tea. Unapotia green tea kwenye maji ya moto hutoa rangi ya kijani kama mchaichai lakini yenyewe siyo mchaichai bali ni majani ya chai hayahaya ya kawaida yanayolimwa Milimani Mufindi na Njombe.
 
Mmmhu
 
Habari wana jf naomba kujuzwa

jee hivi chai ya kijani(green tea) ndiyo ule mchai chai unaopatikana sehemu nyingi ambao ukiuchemshia na maji chai inabadilika rangi au chai ya kijani ni ipi. ??

Hapana hiyo ni green tea inakuwa ni majani hayafanyiwa process yaani yanachumwa yanakaushwa yakiwa hivyohivyo ya kijani
 
Kiongozi nilikuwa napiga sana mchai chai nikijua ndo hyo daaaah mwisho mkojo nao unasadifu rangi ya mchai chai kumbe sioo kiongozi doooh...

Hii grean tea naipata maduka gani?
Green tea ni chai ya kijani kimsingi hata mchaichai ukiwa wakijani ukachemsha kama chai na ukatoa kijani ni chai ya kijani au "GREEN TEA" ORODHA YA MAJANI AMBAYO HUWEZA KUTUMIKA KAMA GREEN TEA -:
NANAA
MCHAICHAI
MAJANI YA MCHAI AMBAYO YAMEKAUSHWA KIVULINI
MAJANI YA MLONGE
MAJANI YA ROSEMERY
MAJANI YA.LAMAO,MCHUNGWA
MAJANI YA MDALASINI
 
ORODHA YA MAJANI AMBAYO HUWEZA KUTUMIKA KAMA GREEN TEA -:

Huweza kutumika kama Green Tea, lakini siyo green tea.
Mkuu peter Agostino yupo sahihi.
Hizo ulizozitaja zinatumika kama chai kwa majina yake ,mfano mint tea ni chai ya mnanaa kama sikosei.
 
Back
Top Bottom