Chaguzi ndogo 16/6 na 14/7 majumuisho na tathmini

Inatia shaka na kinyaa kama ni asilimia tatu (3%) ya waliojiandikisha ndio walipiga kura ndio ushindi hu ni ubakaji wa demokrasia, halafu tunashangilia. Kweli ndiyo simple majority hii?
 
Yafuatayo ni matokeo ya kata zote 26 katika chaguzi zilizofanyika 16/06/2013 na 14/07/2013
WILAYA
KATA
CCM
CHDM
CUF
NCCR
DP
APPT
ADC
NRA
TOTAL
WINNER
former
Loser
Nachingwea
Stesheni
806
327
480
-----1613
CCM
CCM
Sengerema
Nyampulukano
1073
1476
38
45
----2632
CHDM
CCM
CCM lost
Sengerema
Lugata
2214
1044
------3258
CCM
CCM
Muheza
Genge
347
326
6
-----679
CCM
CCM
Muheza
Tingeni
362
244
4
-----610
CCM
CCM
Bahi
Ibungule
863
248
---9
--1120
CCM
CCM
Chemba
Dalai
1361
1027
377
----2765
CCM
CCM
Mbinga
Langiro
-
-NO
-
-C
-O
-N
-T
-E
-STCCM
CCM
Serengeti
Manchilla
676
625
16
-----1317
CCM
CCM
Mbeya
Iyela
1163
1918
-12
20
---3113
CHDM
CCM
CCM lost
Mufindi
Mbalamaziwa
1420
184
------1604
CCM
CCM
Kilolo
Ng'ang'awe
686
217
------903
CCM
CCM
Bukombe
Runzewe west
612
529
----153
1294
CCM
CCM
Temeke
Mianzini
1283
315
494
---25
9
2126
CCM
CCM
Ulanga
Minepa
1196
1029
------2225
CCM
TLP
TLP lost
Kilombero
Ifakara
3746
4106
------7852
CHDM
CCM
CCM lost
Kilosa
Masanze
948
638
------1586
CCM
CCM
Monduli
Makuyuni
1547
360
------1907
CCM
CCM
Arusha
Themi
326
678
313
-----1317
CHDM
CHDM
Arusha
Kimandolu
1169
2665
------3834
CHDM
CHDM
Arusha
Kaloleni
389
1019
169
-----1577
CHDM
CHDM
Arusha
Elerai
1239
1715
213
-----3167
CHDM
CHDM
Babati
Bashnet
1130
2008
------3138
CHDM
CCM
CCM lost
Mbulu
Dangobesh
968
1558
5
-----2531
CHDM
CCM
CCM lost
Singida
Iseke
791
831
96
-----1718
CHDM
CHDM

Mtwara
Mnima
918
206
626
414
----2164
CCM
CUF
CUF Lost
Kura kata zote27233
25293
2837
471
20
9
178
9
56050
Asilimia49%
45%
5%
1%
0%
0%
0%
0%
100%

Positions of the Parties before and After.
CCMCHADEMACUFTLPTOTAL
Wards Before1951126
Wards After16100026

Gainers and Losers
Losers (Former Seats lost)
Gainers (New seats gained)
Net Final position
TLP – Lost 1 to CCM
CHADEMA – Gained 5 from CCM
CHADEMA GAINED 5
CUF – Lost 1 to CCM
CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)
CCM LOST 3
CCM – Lost 5 to CHADEMA

TLP – LOST 1
CHADEMA - none

CUF – LOST 1

Ni matumaini yangu kuwa namba zinajieleza vizuri.

1. Asilimia ya Kura:
CCM wamepata 49%, Chadema 45%, CUF 5% vyama vingine 1%

2. Ushindi wa Jumla wa Kata:
CCM wameshinda kata 16 (moja wameshinda bila kupiga kura kwa kuwa hakukuwa na wagombea wa upinzani) na Chadema wameshinda kata 10.

3. MLINGANISHO NA HALI ILIVYOKUWA BAADA YA UCHAGUZI 2010
  • Chadema wameongeza viti 5
  • CCM wamepoteza viti 3
  • TLP na CUF wamepoteza kiti kimoja kimoja.
4. MAMBO YA KIMKAKATI YA KUZINGATIA KWA VYAMA HUSIKA.
a. Vyama vya Upinzani.
Ukiangalia majimbo ya Stesheni (Nachingwea) na Mnima (Mtwara) wapanzani wakijumlisha kura zao walipata kura nyingi zaidi kuliko CCM, lakini CCM ameibuka mshindi. Hali hii ilikuwepo Kenye pia katika chaguzi mbili za kwanza za vyama vingi ambapo KANU ilikuwa inashinda, lakini kura za upinzani ni nyingi. Hapa ndipo inabidi kufikiria mkakati wa ushindi.

Niwakumbushe tu, wakati wa vita ya pili ya dunia Uingereza iliunda ushirika na Urusi, kwa kuwa waliona nguvu za Ujerumani wasingeziweza wakiwa wametengana. Japo kwa kweli hakukuwa na urafiki mwingine wowote wa dhati kati ya nchi hizi, lengo la ushindi kwa wote liliwaunganisha. Maadui huungana na kuwa rafiki wanapokuwa na tishio la pamoja. Vyama vya upinzani visipoona hivyo, CCM itaendelea kudumu miaka mingi sana ijayo, japo kwa kura kidogo zaidi na zaidi.

Wapinzani Tanzania kama wanahitaji ushindi, wanahitaji kufikiria hili. Ukiangalia jumla ya kura zilizopigwa, CCM wana 49% lakini wana viti vingi zaidi ya 50% vilivyogombaniwa. Hakika CUF ingeungwa mkono na CHADEMA NA NCCR Mageuzi Mtwara na Nachingwea CCM wangepoteza. Kadhalika CUF ingeunga mkono Chadema Kata ya Dalai Dodoma wangewashinda.

Hata hivyo kila chama kinapaswa binafsi kuendelea na kampeni za kujijenga kule ambako bado hawafahamiki, huku wakijitahidi kuhudumia vema wale waliowapa uwakilishi.

b. Chama cha Mapinduzi.
Kwa kweli chama chetu kikongwe Tanzania kinahitaji kujitafiti. Uchaguzi mdogo wa madiwani wa Oktoba 2012, CCM ilipoteza viti kadhaa. Kwa haraka haraka nakumbuka walipoteza Kata 4 zikiwemo ya Daraja Mbili Arusha, Kata ya Ipole wilayani Sikonge - Tabora, na kata ya Lengali wilayani Ludewa. Katika uchaguzi huu CCM wamepoteza kata 5 zilizokuwa mikononi mwao, na kupata mpya mbili zilizokuwa TLP na CUF.

Kipropaganda ni rahisi kuhesabu viti kuwa kati ya kata 26 mmeshinda kata 16. Kimoyomoyo mnajua kuwa mnawakilisha kata chache zaidi sasa kuliko awali. Ni vizuri kujiuliza kama chama iwapo mambo yako sawa ndani ya Chama. Je ni sera? Je ni watendaji? Je ni kubweteka? Je ni mbinu ambazo badala ya kujenga mvuto kwa watu zinazidi kuwafanya watu wakichoke na kukichukia chama hiki tawala? Je ni timu ya kampeni?

Kwa vyovyote vile ni lazima mfanye tafakari. Mfahamu pia kuwa mbinu za kutisha watu kwa vyombo vya dola na kufungua kesi za kubambikiziana, na kujaribu ku criminalize the opposition zinafanya wananchi wawachukie zaidi kuliko kuwapenda.

Hiyo ni tathmini yangu. Nakaribisha mjadala.
Excellent analysis: Wale FISI bado kidogo tuyazamishe baharini!! yanatapatapa hadi yafe menyewe!! CCM ni FISI lazima yauawe!!!!!!!!!!!!!!
 
Mtu wa shamba,

Hongera sana. This is good analysis. Kuungana kwa vyama ili kuindoa ccm madarakani ni vigumu sana. Hii inatokana na rule and divide strategy ya ccm. Inafahamika wazi kuwa vyama vingi vya upinzani ni vibaraka wa ccm, hat hivyo imewashangaza sana ccm kuona chama kimojawapo kama cdm wanakuwa vigahiri na kinyume cha mategemeo yao.

Kwa miaka mingi ccm imejiaminisha kuwa chama tawala milele ndo maana wanashangaa, na hawaamini kama madaraka yao yatapokonywa 2015. Mbinu zao zote hakuna inayofanikiwa zikiwemo hizo za mauaji, vitisho na kuwanyima maendeleo majimbo pinzani.

Kibaya zaidi ni ulevi wa madaraka, kiburi na uongo wa wazi wazi wa watawala wao. Kwa ujumla mimi binafsi nashangaa nikiona bado kuna hata kijana mmoja anaisupport ccm. Wanayoyafanya sasa ni zaidi ya ubaya wa kibinadamu uliopitiliza. Ukiona watu walionakashifa ndio wanajipitisha kutafuta urais....; ukiona mwendelzo wa rushwa....ukiona hoja za wabunge wa chama chao.....; ukiona majigambo ya maendeleo ya waliyafanya 50 yrs kwa kulinganisha na hali halisi ya resources zetu na nchi nyingine.....inatia kinyaaa

Hata hivyo ccm wanweza kuendelea kuwepo kwa sababu kuu mbili 1) ujinga na elimu ndongo ya wapiga kura 2) umaskini (kwa kupewa chakula, khanga....wakati wa kura); 3) Vitisho na maandalizi yao ya kufanya mapinduizi (rejea nchi siwezi kuwapa wapinzani...ili limeishatokea Zanzibar na watataka kulifanya Bara), wapige tu, wapige tu, tumeishawachoka.....

CDM itaweza kuingia madarakani 2015 hata bila support ya kura za 'wapinzani wengine' kama 1) wakiendeleza m4c vijijijini 2) kusimamia uboreshaji wa kitabu cha wapiga kura 3) tume ya uchaguzi kuwa huru (zaidi kwa amani ya tzn), kuhimiza watu kupiga kura kama silaha ya ukombozi wao 5) KULINDA KURA ZAO, KUHIMALISHA red brigade...
 
Mkuu Mtu wa Shamba,
Kwanza asante sana kwa tathmini iliyokwenda shule.

Tathmini yako inaonyesha wazi CCM is loosing big time na Chadema id gaining big gain!.

Kwa upande wangu, kushinda au kushindwa ni matokeo, nataka nijikite zaidi katika the reasons behind that loss or gain kwa vyama viwili tuu, CCM na Chadema tuu!.
Nikianza na CCM.
CCM imepoteza ama kutokana na kuchokwa, kukosa mvuto, au kuadhibiwa kwa kupigiwa kura za chuki kufuatia kampeni chafu, siasa za majo taka, na baadhi ya mbinu chafu inazotumia kisiasa, kubakia watu kesi, matumizi mabaya ya vyombo vya dola, mauaji, etc, kwa kifupi CCM imeangushwa kwa chuki, hasira na kuchokwa na sio kwa sababu haijafanya kitu!.
Nikija kwa Chadema
Chadema kimeendelea kupata ushindi mnono kutokana na kupendwa!. Nakijiuliza Chadema kimefanya nini kustahili kupendwa huku, sioni kitu!. Chadema kinaendelea kushinda kwa sababu CCM imechokwa, na inachukiwa, hivyo kuna maeneo hata Chadema wangesimamisha jiwe, jiwe lingeshinda!. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa baadhi ya ushindi wa Chadema kwenye uchaguzi wa 2010, kuna wabunge na madiwani wa Chadema wameshinda, ukiangalia any substance ya ushindi wao, huioni, ila wameshinda simply kwa sababu CCM imechokwa!.

Kuelekea Uchaguzi wa 2015.
Kwa Upande wa CCM
Kufuatia CCM kuchokwa baadhi ya maeneo, CCM itaendelea kushindwa hata itafanya nini!. Mfano jimbo la Ubungo, by 2015, serikali ya CCM itakuwa imeishakamilisha kujenga barabara za juu kwa juu (fly over) pale makutano ya Ubungo, na mabasi ya mwendo kasi yakiranda kwenye njia zake jijini Dar es salaam, hivyo itajiamini sasa itapendwa wanananchi watakuwa wameshuhudia maendeleo kwa macho yao wenyewe, hivyo sasa wataichagua tena CCM!, no way!. Salama ya CCM kwa 2015 ni kukubali kubadilika na kujiandaa kwa co-existance na wapinzania kuwakubali kuwa hawa sio maadui bali ni washirika wenza katika utawala wa taifa hili, wawapende, wawakubali, na wajiandae kushirikiana nao vinginevyo ....
Kwa Upande wa Chadema.
Wasiendelee kuvimba kichwa kwa kupendwa na kubetweka kwa ushindi uliopatikana kwa muchukiwa kwa CCM!, ili Chadema kiweze kwenda Ikulu, it has to give out reasons za kuichagua besides ushindi wa kura za walioichoka CCM!. Jee Chadema ikishinda, inataraji kufanya nini Ikulu tofauti na CCM?!. Hicho Chadema inachotaraji kufanya, ndicho kiwe sababu ya kuiingiza Ikulu, na sio huu ushindi wa ubwete kinaupata kwa sasa kwa sababu tuu CCM imechokwa!.

My Take.
Naendelea kuipongeza Chadema kwa kukubalika, bali bado naendelea kulitoa angalizo lile lile kuwa kwa uongozi wa nchi kuelekea 2015, Chadema bado haijajipanga!, rejea hapa.

Ila pia Mkuu Mtu wa Shamba, nimeipenda sana hii statement yako
"Maadui huungana na kuwa rafiki wanapokuwa na tishio la pamoja. Vyama vya upinzani visipoona hivyo, CCM itaendelea kudumu miaka mingi sana ijayo, japo kwa kura kidogo zaidi na zaidi".
Naemdelea kuwasisitiza Chadema, peke yenu hamuwezi!. Japo rasimu ya katiba mpya inapendekeza serikali tatu, Watanzania wanaweza kuamua wanataka serikali mbili, hivyo ili chama kishinde, ni lazima kipate angalau theluth moja ya kura kutoka kila upande!, siioni theluth yoyote ya kura za Chadema kutoka visiwani. Japo CUF ni chama adai kwa Chadema kutoka na usharika wake na CCM, Chadema has to find a common denominator ya kushirikiana na adui for fighting a common enemy!, vinginevyo 2015 wapinzani watagawana kura na kujikuta CCM ikiendelea kuongoza kwa simple majority, wakati kama wange join forces, wanaweza kabisa kuiweka kando CCM!.
All the best.
Pasco.
Sikatai kila mtu anamapungufu yake kama ilivyo kwa ccm hivyo na cdm yaweza kuwa nayo na kwakweli napenda kuona wapenda mabadiliko kuichallange cdm ili izidi kujiimarisha zaidi ni vizuri kwa hilo ulilolisema na sina ugomvi nalo. kwa hayo machache nililosema nitarejea kauli yako kuwa cdm haijanya chochote sehemu ilikopita mi nadhani ili kuijenga cdm ungeainisha kabisa ni wapi huko ili tuelewe kuwa umeweka data zenye uhakika zitakazosaidia kujisahihisha kinyume na hapo zitakuwa ni propaganda za kuwaaminisha watu kuwa cdm haijafanya chochote ilhali watu tukiziona tofauiti kubwa ktkhalmashauli zile zinazoongozwa ccm na zile za cdm. Je usafi wa mji wa moshi vip ? mpango wa kusomesha baadhi ya watoto bure sec Arusha na Moshi huoni? ufisadi unaoibuliwa kwenye Halmashauli vp mpaka kazi ya Utto imeanza kuonekana kwani siku zote utto alikuwa wapi. vp hoja ya mnyika bungeni kuhusu maji? vp hoja ya zitto kuhusu mapesa ya uswiss na kumng'oa waziri mkuu pale asipowajbika. vp hoja ya kamanda kipenzi cha vijana ambaye hata mimi nampenda sana lema kuhusu waziri mkuu pale anapolidanganya taifa nayo sio kitu? vp uhodari wa kamanda mrembo sana aliyeandika historia ktk taifa hili kuongoza jimbo muhimu tz, Mdee, vp hoja zake juu ya migogoro ya Ardhi? Ni yeye aliyefanya nikajua kuwa ardhi ya wazee wangu imeuzwa kwa mwekezaji wakati mi niko shule......na mifano mingine mingi.
Sasa ninaloweza kusema ni kwamba hoja za wapinzani ni kuwapa presha hawa watawala kutekeleza miradi ya maendeleo maana mafungu wanayo wao, CDM sio mpaka ikununulie shati au kofia na kiremba kama ccm ndio uje wamefanya kitu. Nadhan nimeeleweka kama wewe nilivyokuelewa yote ni ktk kujenga...ila mimi si kwamba naichukia tu ccm bali hata walichokifanya sikioni. Kwanini? kwa sababu miaka zaidi ya 50 sio kutuhesabia hapa na pale tumefanya, tulipaswa tuone wenyewe sio kusontewa kwa vidole kwani sisi mataahira. Kwenye sheria kunausemi wa kilatini usemao "Les ipsa loquitur" wenye maana mambo au jambo linajieleza lenyewe-ikiwa na maana kwamba miaka 50 ya uhuru na maendeleo vinatakiwa kwenda sanjari tena kwa nchi za wenye mawazo inatakiwa maendeleo yavuke lengo maana rasilimali kibao.
 
Asante sana mkuu kwa analysis yako nzuri, nimeipenda sana hii, but nataka kuongezea kidoogo kuhusu kuchukiwa kwa CCM, CCM inachukiwa kutokana na mambo mabaya iliyofanya na inayoendelea kuyafanya kwa watu wake, na haya yote hapo awali yalikuwa hayaonekani, lakini CHADEMA wakaibuka na kutueleza kinachoendelea, wakatueleza jinsi serikali inavyoendesha mambo, wakatueleza juu ya watu wa CCM wanavyotuibia mali zetu, wakatueleza vitu vingi ambavyo hapo awali vilikuwa kama kificho. Hivyo tunaweza kusema kuwa CHADEAMA ndio wametusababishia tuichukie CCM kwa kiasi flani pamoja na mambo mengine, tuwapongeze kwa hilo huku tukiwapa angalizo kwamba kwa matokeo hayo japo ni mazuri kazi ndio kwaanza imeanza wakaze buti na sisi wapenda mabadiliko tuwe pamoja nao kwenye harakati zao kwa hali na mali.
 
kula kudos mkuu analysis hii inaweza kupingwa na mwehu tu maana namba zinazungumza zenyewe wala hukuhitaji kuongeza hata neno baada ya majedwali yako. kazi nzuri na tunashukuru kwa hilo
 
Chadema fanyeni kila linalowezekana muje tena mtwara mutoe dozi hawa maccm tumechoshwa nayo na lema asikose kuja.
 
Hizi ndo analysis za ma great thinker, thanx mkuu umelitendea haki jukwaa letu..kazi kwao viongozi wa vyama vya siasa kuitumia analysis kujiweka vizuri
 
Mkuu, watakuwa wamekusikia
Mtu wa shamba,

Hongera sana. This is good analysis. Kuungana kwa vyama ili kuindoa ccm madarakani ni vigumu sana. Hii inatokana na rule and divide strategy ya ccm. Inafahamika wazi kuwa vyama vingi vya upinzani ni vibaraka wa ccm, hat hivyo imewashangaza sana ccm kuona chama kimojawapo kama cdm wanakuwa vigahiri na kinyume cha mategemeo yao.

Kwa miaka mingi ccm imejiaminisha kuwa chama tawala milele ndo maana wanashangaa, na hawaamini kama madaraka yao yatapokonywa 2015. Mbinu zao zote hakuna inayofanikiwa zikiwemo hizo za mauaji, vitisho na kuwanyima maendeleo majimbo pinzani.

Kibaya zaidi ni ulevi wa madaraka, kiburi na uongo wa wazi wazi wa watawala wao. Kwa ujumla mimi binafsi nashangaa nikiona bado kuna hata kijana mmoja anaisupport ccm. Wanayoyafanya sasa ni zaidi ya ubaya wa kibinadamu uliopitiliza. Ukiona watu walionakashifa ndio wanajipitisha kutafuta urais....; ukiona mwendelzo wa rushwa....ukiona hoja za wabunge wa chama chao.....; ukiona majigambo ya maendeleo ya waliyafanya 50 yrs kwa kulinganisha na hali halisi ya resources zetu na nchi nyingine.....inatia kinyaaa

Hata hivyo ccm wanweza kuendelea kuwepo kwa sababu kuu mbili 1) ujinga na elimu ndongo ya wapiga kura 2) umaskini (kwa kupewa chakula, khanga....wakati wa kura); 3) Vitisho na maandalizi yao ya kufanya mapinduizi (rejea nchi siwezi kuwapa wapinzani...ili limeishatokea Zanzibar na watataka kulifanya Bara), wapige tu, wapige tu, tumeishawachoka.....

CDM itaweza kuingia madarakani 2015 hata bila support ya kura za 'wapinzani wengine' kama 1) wakiendeleza m4c vijijijini 2) kusimamia uboreshaji wa kitabu cha wapiga kura 3) tume ya uchaguzi kuwa huru (zaidi kwa amani ya tzn), kuhimiza watu kupiga kura kama silaha ya ukombozi wao 5) KULINDA KURA ZAO, KUHIMALISHA red brigade...
 
Pamoja na analysis nzuri ya Mtu wa Shamba, nina swali la kizushi.

Hivi huu mkakati unaoonekana kwenye picha hii, ulisaidia kiasi gani kuongeza kura za CCM au kupunguza kura za CDM?

attachment.php
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mtu wa Shamba,
Kwanza asante sana kwa tathmini iliyokwenda shule.

Tathmini yako inaonyesha wazi CCM is loosing big time na Chadema id gaining big gain!.

Kwa upande wangu, kushinda au kushindwa ni matokeo, nataka nijikite zaidi katika the reasons behind that loss or gain kwa vyama viwili tuu, CCM na Chadema tuu!.
Nikianza na CCM.
CCM imepoteza ama kutokana na kuchokwa, kukosa mvuto, au kuadhibiwa kwa kupigiwa kura za chuki kufuatia kampeni chafu, siasa za majo taka, na baadhi ya mbinu chafu inazotumia kisiasa, kubakia watu kesi, matumizi mabaya ya vyombo vya dola, mauaji, etc, kwa kifupi CCM imeangushwa kwa chuki, hasira na kuchokwa na sio kwa sababu haijafanya kitu!.
Nikija kwa Chadema
Chadema kimeendelea kupata ushindi mnono kutokana na kupendwa!. Nakijiuliza Chadema kimefanya nini kustahili kupendwa huku, sioni kitu!. Chadema kinaendelea kushinda kwa sababu CCM imechokwa, na inachukiwa, hivyo kuna maeneo hata Chadema wangesimamisha jiwe, jiwe lingeshinda!. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa baadhi ya ushindi wa Chadema kwenye uchaguzi wa 2010, kuna wabunge na madiwani wa Chadema wameshinda, ukiangalia any substance ya ushindi wao, huioni, ila wameshinda simply kwa sababu CCM imechokwa!.

Kuelekea Uchaguzi wa 2015.
Kwa Upande wa CCM
Kufuatia CCM kuchokwa baadhi ya maeneo, CCM itaendelea kushindwa hata itafanya nini!. Mfano jimbo la Ubungo, by 2015, serikali ya CCM itakuwa imeishakamilisha kujenga barabara za juu kwa juu (fly over) pale makutano ya Ubungo, na mabasi ya mwendo kasi yakiranda kwenye njia zake jijini Dar es salaam, hivyo itajiamini sasa itapendwa wanananchi watakuwa wameshuhudia maendeleo kwa macho yao wenyewe, hivyo sasa wataichagua tena CCM!, no way!. Salama ya CCM kwa 2015 ni kukubali kubadilika na kujiandaa kwa co-existance na wapinzania kuwakubali kuwa hawa sio maadui bali ni washirika wenza katika utawala wa taifa hili, wawapende, wawakubali, na wajiandae kushirikiana nao vinginevyo ....
Kwa Upande wa Chadema.
Wasiendelee kuvimba kichwa kwa kupendwa na kubetweka kwa ushindi uliopatikana kwa muchukiwa kwa CCM!, ili Chadema kiweze kwenda Ikulu, it has to give out reasons za kuichagua besides ushindi wa kura za walioichoka CCM!. Jee Chadema ikishinda, inataraji kufanya nini Ikulu tofauti na CCM?!. Hicho Chadema inachotaraji kufanya, ndicho kiwe sababu ya kuiingiza Ikulu, na sio huu ushindi wa ubwete kinaupata kwa sasa kwa sababu tuu CCM imechokwa!.

My Take.
Naendelea kuipongeza Chadema kwa kukubalika, bali bado naendelea kulitoa angalizo lile lile kuwa kwa uongozi wa nchi kuelekea 2015, Chadema bado haijajipanga!, rejea hapa.

Ila pia Mkuu Mtu wa Shamba, nimeipenda sana hii statement yako
"Maadui huungana na kuwa rafiki wanapokuwa na tishio la pamoja. Vyama vya upinzani visipoona hivyo, CCM itaendelea kudumu miaka mingi sana ijayo, japo kwa kura kidogo zaidi na zaidi".
Naemdelea kuwasisitiza Chadema, peke yenu hamuwezi!. Japo rasimu ya katiba mpya inapendekeza serikali tatu, Watanzania wanaweza kuamua wanataka serikali mbili, hivyo ili chama kishinde, ni lazima kipate angalau theluth moja ya kura kutoka kila upande!, siioni theluth yoyote ya kura za Chadema kutoka visiwani. Japo CUF ni chama adai kwa Chadema kutoka na usharika wake na CCM, Chadema has to find a common denominator ya kushirikiana na adui for fighting a common enemy!, vinginevyo 2015 wapinzani watagawana kura na kujikuta CCM ikiendelea kuongoza kwa simple majority, wakati kama wange join forces, wanaweza kabisa kuiweka kando CCM!.
All the best.
Pasco.
hizo bold red za kutafakali san kwa CDM. kubaki madalakn ni jambo dogo sana kwa viongozi, jarb hata kufanikisha 10% ya ahdi zako hakika utarudi uongozin Lov CDM.
 
notradamme Mkuu umejitahidi sana kupotosha baadhi ya mambo mengi katika uchambuzi wako.Kwanza ni makosa sana kuihusisha Chadema na vurugu.Ingekuwa vizuri ukatambua kwanza nini maana ya vurugu na chanzo chake ni kipi.(VURUGU-kuvunja/kuharibu utaratibu flani/kufanya mambo kinyume).

Kwa tafsiri hiyo ndogo nnaomba tujiulize kati ya CHADEMA/police na Serikali kuu ni nani anafanya vurugu.Kwa mujibu wa katiba yetu inaturuhusu kukusanyika/kujadiliana na inatutaka tu kutoa TAARIFA kwa jeshi la police ili watupatie wananchi haki yetu ya kulindwa.Chadema wanatoa matangazo kwa raia kuhusu mkutano na wananchi wanaitikia mwito,tatizo linakuja kwa police na Serikali.Police wanatoa katazo la kutokufanya mkusanyiko wowote(kumbuka police hawana mamlaka ya kuzuia mkusanyiko wao hupewa TAARIFA tu).Wanapokuja na kulipua mabomu ya machozi na risasi za moto kisa kutawanya mkutano halali(kwa mujibu wa katiba yetu)ni nani kati ya hawa(police/Chadema/Serikali)wanafanya fujo-kuvuruga utaratibu?

Mlipuko wa bomu Arusha uliosababisha maisha ya watu kupotea tuliona fujo za police/ccm/Seikali.Lukuvi aliamka Bungeni na kuudanganya uma,Nape nae aliibuka mbele ya waandishi wa habari na kudanganya uma na alifika mbali zaidi kwa kuitaja Chadema ndio wahusika wakuu.Police kupitia kwa Chagonja aliibuka na vitisho vya hali ya juu kwa viongozi wa Chadema kwa kuwataka wajisalimishe kwake utafikiri Mbowe na Lema ndio watuhumiwa wakuu.Police/Serikali/CCM ndio vyanzo vikuu vya vurugu nchini.

Tukio la Mwangosi police walimuua live bila chenga mwandishi wa habari Daudi Mwangosi mbele ya RPC Kamhanda na bila ya woga wakaja na sinenma yao kuwa waliomwua Mwangosi ni wafuasi wa CHADEMA na alikufa kutokana na kitu kizito kilichorushwa na hao wafuasi,TUNASHUKURU MUNGU PICHA ZILIWAUMBUA WAKIMUUA MWANGOSI picha likageuka na kumfungulia masitaka askari alieua na kichekesho zaidi wakampandisha cheo Kamhanda(kwa kusimamia mauaji).

Katika matukio yoote mabaya yanayofanywa juu ya Chadema ili mkiangamize hamtaweza asilani abadani,angaliana uchambue mambo kiuhalisia na sio kihisia zaidi.Kama chama cha CHADEMA ni hatari kwa nini msajili wa vyama vya siasa hajakifuta?Tuna matatizo mengi sana ya kujadili katika nchi hii tajiri inayonyonywa na Watawala(Mafisadi)wachache,Ushauri wa bure CCM pambaneni na matatizo yanayoikabili nchi hii acheni kupambana na chama cha CHADEMA.
ciril ndugu yangu, huwezi kutoa andishi bila kujali hisia. ila hisia haziruhusiwi kufifisha ukweli na uhalisia wa chochote kinachojadiliwa.
labda nianze kwa kulitetea jeshi la polisi na jinsi ambavyo chadema wanalionea na kulidhalilisha wakati jeshi hilo linafanya kazi kwa mujibu wa sheria. ni mzandiki tuu atakayekataa kuwa jeshi la pilisi tulilonalo sasa ni bora kiutendaji kuliko kipindi chochote tangu uhuru, na ndio jeshi la polisi pekee miongoni mwa nchi za SADC na EAC. polisi ya tz chini ya said mwema imejipenyeza mpaka miongoni mwa raia kupitia polisi jamii na ulinzi shirikishi kiasi ambacho askari polisi wa tz sio kiumbe cha kuogopwa zaidi ya kuonekana rafiki wa watu. nenda katika nchi zinazotuzunguka au hata SOUTH AFRICA kisha uje ulinganishe na TZ.
tatizo la CHADEMA ni PROVOCATION! mnawa-provoc polisi kwa makusudi ili watimize wajibu wao ili mpate platform ya kulalamika. tunajua kabisa kuwa MAANDAMANO, MIKUTANO na uhuru wa kutoa maoni ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania...
ni kwa nini sasa inalazimika polisi kupewa taarifa?? ni kwa sababu mikutano na maandamano yatahitaji ulinzi toka jeshi la polisi.sasa polisi wakiwa hawana askari wa kutosha kutoa ulinzi katika mkutano/maandamano husika ni wajibu wao kupiga marufuku. tatizo lenu kubwa mnafanya siasa huku mkidhani ninyi ni weledi wa kila kitu(hili ni tatizo la wanasiasa wooote wa africa), mnajiona kuwa ni wataalamu wa SHERIA,UCHUMI,USALAMA,VITA,HABARI,ELIMU,UVUVI,HIFADHI,UHANDISI na kila kitu kiasi cha kuingilia hata mamlaka za kiutawala. hebu jiulize kwa kutenda haki kabisa,, hivi ni chama gani kinachoongoza kwa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ndani ya miaka mitatu iliyopita??? hivi kweli kama serikali na jeshi la polisi wangekuwa wana dhamira mbaya ya kukandamiza democrasia kama mnavyotaka tuamini, hayo yote yangewezekana??????? jibu utakuwa nalo moyoni hata kama humu utajibu tofauti na moyo wako...
kuhusu mauaji ya MWANGOSI, nadhani lile llikuwa ni kosa la kimedani na kwa kutambua hilo, serikali ilichukua hatua kwa mujibu wa sheria na yule askari nadhani sisi wote ni mashahidi kuwa yuko mahakamani, tatizo ni kwamba hata katika matukio ya kijeshi mnataka maamuzi yatolewe kisiasa kwa matakwa yenu ili mwisho wa siku mje humu na kujitapa kwamba serikali inaendeshwa kwa amri za chadema.
kuhusu bomu la arusha>>>>> mtanisamehe saaana kama mtapenda lakini kwa mtu yeyote mwenye akili isiyoendeshwa na ushabiki hawezi kuihusisha serikali wala CCM katika mlipuko ule. na kuna kila sababu ya kuihusisha CHADEMA na tukio lile na hata matukio baada ya mlipuko ule yanathibitisha dhana hiyo. hivi labda nikuulize, ni kwa maslahi gani CCM/SERIKALI itaayapata kwa kulipua bomu kwenye mkutano wa chadema!!!?????? ni mwendawazimu tu ambae ataacha kuihusisha serikali/ccm kama mlipuko ukitokea kwenye mkutano wa chadema(kama mnavyoihusisha sasa).Na hivyo basi ili kuichafua serikali/ccm NI LAZIMA WALE WENYE MALENGO HAYO(CHADEMA) wafanye tukio kama lile ili mwisho wa siku lawama zielekezwe kwa serikali/ccm kama jinsi mnavyojitahidi kutuaminisha.
lakini vilevile ukiangalia na kutafakari kauli za viongozi wa chadema baada ya mlipuko wa pale soweto, kuna kitu kinajionyesha. kwa nini mkutano ule waliandaa vifaa maalum(bullshit) vya kurikodi matukio??? kwa nini walengwa wa lile bomu hawakuwa na dhamira ya kuwalenga viongozi?? kwa nini camera iliyochukua tukio haikushituliwa na mlipuko wa bomu lile??? kwa nini yalikuwa yamelengwa maeneo maalum kwa mpiga picha kuchukua matukio???na LA MSINGI KABISA, KWA NINI USHAHIDI WA MLIPUKO ULE MPAKA SASA UNAJULIKANA NA WATU WATATU TUU NDANI YA CHADEMA???? KWA NINI HATA VIKAO VYA JUU VYA CHAMA VIMESHINDWA KUDAI NA KUPEWA (japo kwa kuonyeshwa tuu) USHAHIDI HUU???? KWA NINI HATA WANASHERIA WA CHAMA (ambao ndio haswaa waliostahili kukaa na ushahidi huo kwa ajili ya taratibu za kisheria) MAPAKA LEO HII HAWAJUI HUO USHAHIDI UNAOONGELEWA NI UPI????
jiulize kwa nini wale watu makini kabisa ndani ya chama chenu kama akina ZZK,KITILA MKUMBO,TUNDU LISSU, PRO SAFARI NA PROF BAREGU wamejitenga kabisa na upuuzi wa bomu la pale soweto???? amini nakwambia, something is cooking and when the right time comes, mtalalamika kuwa mnahujumiwa... ona yanayotokea kwa KILEO kule igunga, imechukua miaka mingapi kwa ukweli kuja kujulikana???? ni muda tu kaka na mlipuko wa arusha utapata mwenyewe.
kwangu mimi naona ni upuuzi kwa mzalendo yeyote wanchi hii atakaposimama na kusema"""eti tuzingatie na kutatua kero za wananchi na sio kujaribu kuiangamiza chadema'''' mimi naamini kabisa kuwa SIASA ZA CHADEMA ZA HIVI SASA NI TATIZO KUBWA KATIKA NCHI YETU KULIKO MATATIZO YOOOTE YANALOLIKABILI TAIFA hata kama chadema yenyewe sio tatizo.
ni halmashauri ngapi mnazoziongoza ambazo manawakataza wananchi kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo???
ni kwa kiasi gani mnawashawishi na kuwa-organise wamachinga wafanye biashara maeneo mabayo ni kinyume cha sheria?
ni kwa kiwango gani mnajaribu kuzipaka matope juhudi za serikali (hata kama hazitoshi) katika kutimiza ahadi na malengo yake????
ni kwa kiwango gani mnajaribu kuuteketeza na kuuangamiza uzalendo tokamioyoni mwa watanzania na kuwashawishi kuichukia nchi yao tz na kuipenda chadema kama vile chadema/ccm zinaweza kuwepo bila tanzania???????
'' DEMOCRACY IS NOT ALL ABOUT ELECTIONS, IT'S ABOUT NATIONAL STABILITY AND PATRIOTISM''
kumbuka HAMMAS, MUSLIM BROTHERHOOD, MDC na CUF..hivi vyama vilishinda uchaguzi lakini havikupewa nchi.unajua ni kwa nini???? havikuwa vinawakilisha matakwa na hatma ya mataifa husika
 
Huu mchanganuo umekaa kichadema zaidi, sidhani kama mnajua kuwa Wananchi wamechoka na fujo,dalili za vita, na maandamano.
Kama kweli kuna wachanganuaji wa maana hapa hebu mtuwekee "response" ya Wananchi baada ya uchaguzi huu.
 
Nakushukuru sana kwa uchambuzi makini unaonyesha uhalisia wa siasa za hapa Tanzania na jinsi demokrasia inavyokua kwav kasi. mabadiliko yanayotokea ni ishari nzuri kwa vyama vya siasa. wajitahidi kujipanga vizuri kwani fikra za wanananchi zinabadilika.
 
Mkuu Awo, cheo cha U-DC ni cheo kikubwa sana kwangu, na mshahara wake na marupurupu yake manene sana, wengi wanautamani, ila amini usiamini, kuna wengine wetu tumezoea shida kiasi kwamba hatuzitamani kabisa hizo posti za kupewa!. Mimi tangu 2002 I'm on my own, more than 10 years now!, situmwi, natuma!, although I don't make much, kuniambia nasotea tena kuja kutumwa kwa take home ya DC, ni kunishusha sana!. Kwa vile CCM ndio mpango mzima wa dili zote za kukomba fungu, nikikwama kabisa, nitakata kadi ya CCM na kupiga hodi Ikulu kuomba kazi ya U DC na kwa CV yangu na uzoefu, nitapata ili nianze tena kutumwa na kuyaka asubuhi kuwahi kazini. Tena nitashauri nipangiwe kuwa DC wa Hai au Karatu, ili niwashughulikie ipasavyo jamaa zangu wawili hawa kabla ya 2015 ibakie hadithi tuu!.

Hivi unajua kuna watu fulani fulani wanatafutwa na maisha mazuri, wao hawapendi kisa wamezoea shida?!, hata raha zikiwaita wanazigomea wao wanatafuta tuu shida?!. Kwa mfano namuonea raha sana mwalimu wangu mmoja wa pale UD alikuwa ni mkuu wa idara na level ya kukaribia kabisa kuwa Prof, ati na yeye sasa ni DC!. Just imagine Pasco wa PPR, anaeroll almost that much wakati wa Saba Saba pekee, leo anakuwa DC kusubiria ...mwisho wa mwezi!.
Please gi'me a break!.

Pasco.

Duuu, aisee!
 
Back
Top Bottom