Chaguzi ndogo 16/6 na 14/7 majumuisho na tathmini

Mkuu Pelekete, huwezi amini, kuna type fulani ya watu wachache wa aina yangu ambao kwetu ukuu wa wilaya sio deal kabisa!. Kwa ukaribu nilionao na hozo top corridors, ingekuwa U DC kwangu ni deal, ningeshakuwa siku nyingi!, ningeanzia tuu na kukata kadi ya CCM, mengine yote yangefuatia!, maskini Pasco mimi, hata kadi ya CCM sina, leo ukuu wa wilaya upi ninaupumulia?!.

Nimeipenda hii ya kwenye bold, kumbe unatambua kuna kukabidhiwa nchi!, wakati wewe ukiconcentrate kusubiria kukabidhiwa, mimi ninamuimagine huyo mkabidhi, atamkabidhi nani?. Kabla mkabidhi hajakabidhi, kwanza anamtathmini mkabidhiwa, ataweza kuubeba huo mzigo anaotaka kukabidhiwa?!. Ili mkabidhiwa aweze kukabidhiwa, lazima aonyesha utayari wa kuubeba huo mzigo!, tena utayari ni kitu mimoja na uwezo wa kubeba ni kitu kingine!. Kwanza aonyeshe utayari tuu, akabidhiwe ndipo aonyeshw uwezo!, hayo yote kwa Chadema wewe umeyaona?!.
Pasco.

Pasco,nafikiri umepotoka kidogo.Mkabidhi nchi ni mwananchi, na ameishaanza kuonyesha kuikabidhi CDM,ukitaka kuniambia CCM ndio mkabidhi nchi na atakabidhi atakaporidhika yeye nafikiri unapotoka.Daima anayetawala huwa hayuko radhi kukabidhi, mpaka mazingira yamlazimishe.Hii itatokea kwetu soon.
 
Yafuatayo ni matokeo ya kata zote 26 katika chaguzi zilizofanyika 16/06/2013 na 14/07/2013
WILAYA
KATA
CCM
CHDM
CUF
NCCR
DP
APPT
ADC
NRA
TOTAL
WINNER
former
Loser
Nachingwea
Stesheni
806
327
480
-----1613
CCM
CCM
Sengerema
Nyampulukano
1073
1476
38
45
----2632
CHDM
CCM
CCM lost
Sengerema
Lugata
2214
1044
------3258
CCM
CCM
Muheza
Genge
347
326
6
-----679
CCM
CCM
Muheza
Tingeni
362
244
4
-----610
CCM
CCM
Bahi
Ibungule
863
248
---9
--1120
CCM
CCM
Chemba
Dalai
1361
1027
377
----2765
CCM
CCM
Mbinga
Langiro
-
-NO
-
-C
-O
-N
-T
-E
-STCCM
CCM
Serengeti
Manchilla
676
625
16
-----1317
CCM
CCM
Mbeya
Iyela
1163
1918
-12
20
---3113
CHDM
CCM
CCM lost
Mufindi
Mbalamaziwa
1420
184
------1604
CCM
CCM
Kilolo
Ng'ang'awe
686
217
------903
CCM
CCM
Bukombe
Runzewe west
612
529
----153
1294
CCM
CCM
Temeke
Mianzini
1283
315
494
---25
9
2126
CCM
CCM
Ulanga
Minepa
1196
1029
------2225
CCM
TLP
TLP lost
Kilombero
Ifakara
3746
4106
------7852
CHDM
CCM
CCM lost
Kilosa
Masanze
948
638
------1586
CCM
CCM
Monduli
Makuyuni
1547
360
------1907
CCM
CCM
Arusha
Themi
326
678
313
-----1317
CHDM
CHDM
Arusha
Kimandolu
1169
2665
------3834
CHDM
CHDM
Arusha
Kaloleni
389
1019
169
-----1577
CHDM
CHDM
Arusha
Elerai
1239
1715
213
-----3167
CHDM
CHDM
Babati
Bashnet
1130
2008
------3138
CHDM
CCM
CCM lost
Mbulu
Dangobesh
968
1558
5
-----2531
CHDM
CCM
CCM lost
Singida
Iseke
791
831
96
-----1718
CHDM
CHDM

Mtwara
Mnima
918
206
626
414
----2164
CCM
CUF
CUF Lost
Kura kata zote27233
25293
2837
471
20
9
178
9
56050
Asilimia49%
45%
5%
1%
0%
0%
0%
0%
100%

Positions of the Parties before and After.
CCMCHADEMACUFTLPTOTAL
Wards Before1951126
Wards After16100026

Gainers and Losers
Losers (Former Seats lost)
Gainers (New seats gained)
Net Final position
TLP – Lost 1 to CCM
CHADEMA – Gained 5 from CCM
CHADEMA GAINED 5
CUF – Lost 1 to CCM
CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)
CCM LOST 3
CCM – Lost 5 to CHADEMA

TLP – LOST 1
CHADEMA - none

CUF – LOST 1

Ni matumaini yangu kuwa namba zinajieleza vizuri.

1. Asilimia ya Kura:
CCM wamepata 49%, Chadema 45%, CUF 5% vyama vingine 1%

2. Ushindi wa Jumla wa Kata:
CCM wameshinda kata 16 (moja wameshinda bila kupiga kura kwa kuwa hakukuwa na wagombea wa upinzani) na Chadema wameshinda kata 10.

3. MLINGANISHO NA HALI ILIVYOKUWA BAADA YA UCHAGUZI 2010
  • Chadema wameongeza viti 5
  • CCM wamepoteza viti 3
  • TLP na CUF wamepoteza kiti kimoja kimoja.
4. MAMBO YA KIMKAKATI YA KUZINGATIA KWA VYAMA HUSIKA.
a. Vyama vya Upinzani.
Ukiangalia majimbo ya Stesheni (Nachingwea) na Mnima (Mtwara) wapanzani wakijumlisha kura zao walipata kura nyingi zaidi kuliko CCM, lakini CCM ameibuka mshindi. Hali hii ilikuwepo Kenye pia katika chaguzi mbili za kwanza za vyama vingi ambapo KANU ilikuwa inashinda, lakini kura za upinzani ni nyingi. Hapa ndipo inabidi kufikiria mkakati wa ushindi.

Niwakumbushe tu, wakati wa vita ya pili ya dunia Uingereza iliunda ushirika na Urusi, kwa kuwa waliona nguvu za Ujerumani wasingeziweza wakiwa wametengana. Japo kwa kweli hakukuwa na urafiki mwingine wowote wa dhati kati ya nchi hizi, lengo la ushindi kwa wote liliwaunganisha. Maadui huungana na kuwa rafiki wanapokuwa na tishio la pamoja. Vyama vya upinzani visipoona hivyo, CCM itaendelea kudumu miaka mingi sana ijayo, japo kwa kura kidogo zaidi na zaidi.

Wapinzani Tanzania kama wanahitaji ushindi, wanahitaji kufikiria hili. Ukiangalia jumla ya kura zilizopigwa, CCM wana 49% lakini wana viti vingi zaidi ya 50% vilivyogombaniwa. Hakika CUF ingeungwa mkono na CHADEMA NA NCCR Mageuzi Mtwara na Nachingwea CCM wangepoteza. Kadhalika CUF ingeunga mkono Chadema Kata ya Dalai Dodoma wangewashinda.

Hata hivyo kila chama kinapaswa binafsi kuendelea na kampeni za kujijenga kule ambako bado hawafahamiki, huku wakijitahidi kuhudumia vema wale waliowapa uwakilishi.

b. Chama cha Mapinduzi.
Kwa kweli chama chetu kikongwe Tanzania kinahitaji kujitafiti. Uchaguzi mdogo wa madiwani wa Oktoba 2012, CCM ilipoteza viti kadhaa. Kwa haraka haraka nakumbuka walipoteza Kata 4 zikiwemo ya Daraja Mbili Arusha, Kata ya Ipole wilayani Sikonge - Tabora, na kata ya Lengali wilayani Ludewa. Katika uchaguzi huu CCM wamepoteza kata 5 zilizokuwa mikononi mwao, na kupata mpya mbili zilizokuwa TLP na CUF.

Kipropaganda ni rahisi kuhesabu viti kuwa kati ya kata 26 mmeshinda kata 16. Kimoyomoyo mnajua kuwa mnawakilisha kata chache zaidi sasa kuliko awali. Ni vizuri kujiuliza kama chama iwapo mambo yako sawa ndani ya Chama. Je ni sera? Je ni watendaji? Je ni kubweteka? Je ni mbinu ambazo badala ya kujenga mvuto kwa watu zinazidi kuwafanya watu wakichoke na kukichukia chama hiki tawala? Je ni timu ya kampeni?

Kwa vyovyote vile ni lazima mfanye tafakari. Mfahamu pia kuwa mbinu za kutisha watu kwa vyombo vya dola na kufungua kesi za kubambikiziana, na kujaribu ku criminalize the opposition zinafanya wananchi wawachukie zaidi kuliko kuwapenda.

Hiyo ni tathmini yangu. Nakaribisha mjadala.

Mkuu hii analysis imetulia sana na kwangu mimi mengi yaliyo changiwa na wana jf nayakubali sana tu. Suala la muungano wa uingereza na urusi ni touch base kwa vyama vyetu vya upinzani. Sina uhakika sheria inasemaje kwa sas lakini katiba mpya kama haitabakwa na magamba huk mbele kutakuwa na uwezekano wa kuunda coharitions hasa kukiisha kuwa na mgombea binafsi and thats a killing kick kwa ccm. Nina wasa wasi sana na wapinzani wa wapinzani means -ve na -ve means +ve. Mbatia anako ipeleka nccr ni shida, mwelekeo wa cuf baada ya kupewa share zanzibar na mrema baada ya kulipwa jk mafao yake ya muda mrefu. Cdm waangalie muungano wowote kwa makini but thee bottom line thats a great idea. Once again Ahsante mkuu kwa input yako yenye mashiko sana tu.
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa.

Lakini kuna namna nyingi za kuungana. Mfano CUF wanaweza kukubaliana KUIUNGA MKONO CHADEMA ARUSHA, na CHADEMA IIUNGE MKONO CUF LINDI NA MTWARA; na wakaishia hapo. Huo ni mfano tu, lakini mfano huu ungewezesha CUF kupata viti vya Mtwara na Nachingwea kwenye uchaguzi huu. WIN-WIN Alliance.

Cha muhimu vyama viweze kupanga mikakati ya ushindi.
 
Ila pia Mkuu Mtu wa Shamba, nimeipenda sana hii statement yako
"Maadui huungana na kuwa rafiki wanapokuwa na tishio la pamoja. Vyama vya upinzani visipoona hivyo, CCM itaendelea kudumu miaka mingi sana ijayo, japo kwa kura kidogo zaidi na zaidi".
Naemdelea kuwasisitiza Chadema, peke yenu hamuwezi!. Japo rasimu ya katiba mpya inapendekeza serikali tatu, Watanzania wanaweza kuamua wanataka serikali mbili, hivyo ili chama kishinde, ni lazima kipate angalau theluth moja ya kura kutoka kila upande!, siioni theluth yoyote ya kura za Chadema kutoka visiwani. Japo CUF ni chama adai kwa Chadema kutoka na usharika wake na CCM, Chadema has to find a common denominator ya kushirikiana na adui for fighting a common enemy!, vinginevyo 2015 wapinzani watagawana kura na kujikuta CCM ikiendelea kuongoza kwa simple majority, wakati kama wange join forces, wanaweza kabisa kuiweka kando CCM!.
All the best.
Pasco.

Pasco, Mtu wa Shamba

Ahsanteni kwa uchambuzi.

Natofautiana nanyi kwa kitu kimoja cha msingi, nacho "wapinzani" kuungana.

Definition yangu ya upinzani inatokana na dhana ya kupinga; kwangu mimi na hapa Tanzania haipo. Labda kwa mamluki wa kisiasa wasiojua wajibu wao wa kisiasa kwa sera wanazowashawishi wapiga kura.

Kuna historia nyuma ya haya yote.

Kuna vyama vimeanzishwa kukidhi matakwa ya upinzani kwa maana ya umamluki; dalili zao za nje ni kutumika kuharibu agenda za kisiasa kwa kupinga kwa sababu za kipumbavu. Kuna vyama vimeanzishwa kwa dhamira ya kuendesha siasa ya mtazamo mbadala nadhani havizidi viwili sana sana vitatu. Kuna chama dola ambacho hakina hata usajili.

Kwa misingi hii mtazamo wangu ni kuwa kwa miaka ishirini (20) kila chama kilikuwa na dondoo na mkakati. Dola dhaifu imekidhoofisha chama dola au kinyume chake. Vyama makini vilijikita kuwaelimisha kisiasa wapiga kura. Kwa ujumla uelewa wa watu baada ya miaka 20 uko tofauti sana.

Upigaji kura; kuna neno mmelitumia CCM kuchwokwa ndiyo turufu ya upinzani, basi kama ndiyo hivyo ina maana turufu hiyo ndiyo inaviangamiza vyama mamluki. Lakini tuingie kwenye saikolojia ya kupiga kura. Kupiga kura ni hiari ya mtu kuchagua. Anachagua kwa malengo ya ulinganisho wa kinachotokea (uzoefu), kinachoelezwa(mantiki ya hoja) na kinachotarajiwa (jumla ya uzoefu na hoja). Hayo yote yana msingi wa uelewa sitaki kuita elimu ambao vyama makini viljiwekea kama mkakati.

Uzoefu wa Arusha

Arusha ina historia ya kujituma kiuchumi, ilikuwa na uchumi wa kilimo, utalii na viwanda ambavyo vyote ni suala zima la ARDHI. Kilimo kimeshuka, utalii unaongezeka kwa kasi ndogo viwanda vimekufa wananchi wa Arusha wanajua sababu za yote haya. Mji unaendelezwa kwa Halmashauri ya kichina (feki) kwa maana maamuzi si ya madiwani bali ya watawala na si kwa maslahi ya utawala bali ya watu wenye nafasi kwenye utawala kwa manufaa yao. Wana sababu kuu mbili; kwanza wanajitahidi kuficha madhambi yao ya kiuchumi na kijamii. Pili "wanajaribu" kuendelea/za udhalimu wao kiuchumi na kijamii. Athari za uchumi ni watu kukosa kazi au kipato/ujira cha ajira, kijamii unazungumzia kupata na kumudu huduma za elimu afya, haki mbali mbali na zaidi kujipanga kwa maisha bora. Kwa maana hiyo chama makini kitaweka dondoo ya kiuchumi na kijamii inayomgusa mpiga kura.

Kinachotokea chama dola hakina agenda hizo ila kuwashinikisha watu kwa vitisho na kashfa za uongo. Ni kweli vyama makini vimerahisishiwa kuwaelimisha wananchi na kutoa hoja mbadala si suala la kuingia ikulu, ni suala la kugusa maisha ya kiuchumu na kijamii ya mtu binafsi. Ni suala la kupata mbadala wa kisera na kimkakati unaomgusa mtu binafsi.

Chadema kwa sisi watu wa Arusha kauli zao zinaendana na matendo yao. CCM inalazimisha kwa ukimbelembele wa watawala kama watu wanaotegemewa watoa sadaka na wababe pale mnapotofautiana kwa hoja.

Vyama vingine kwenye kapu la upinzani vinaponzwa na "upinzani" wao kwa agenda zinazowagusa wananchi (umamluki kwa chama dola)

Hitimisho

Ni upuuzi kufikiria kuungana na "wapinzani" (mamluki) ambao wanajulikana kwa kukosa agenda serious za ukombozi binafsi na wakitaifa. CHADEMA endeleeni na agenda yenu achaneni na wazo la kipuuzi la kuunganisha nguvu na mamluki. Mafanikio yenu haya ni ushahidi kuwa agenda yenu inatekeleza bila mamluki. Ondoeni dhana ya kupingana na CCM jikiteni kwenye ukombozi wa kifikra kwa wananchi wote ambao ndio chachu ya mafanikio ya kiuchumi kijamii. CCM imejichagulia kifo imeshaanza kufa na itakufa kwa wakati wake kama haijafa hadi sasa
 
Pasco,nafikiri umepotoka kidogo.Mkabidhi nchi ni mwananchi, na ameishaanza kuonyesha kuikabidhi CDM,ukitaka kuniambia CCM ndio mkabidhi nchi na atakabidhi atakaporidhika yeye nafikiri unapotoka.Daima anayetawala huwa hayuko radhi kukabidhi, mpaka mazingira yamlazimishe.Hii itatokea kwetu soon.
Nchi inakabidhiwa by vetting not by votting!.
Rais wa nchi ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama!. Hata ikitokea chama fulani kikamsimamisha a very popular linatic, akachaguliwa, jee atakabidhiwa?!. Utawala wa nchi una change hands kwa exchange of instrumetns of power ikiwemo kuapishwa na kukabidhiwa vyombo vya dola, wanaofanya hayo ni wale wapiga kura au nu yule mwenye navyo?!. JK ndie rais aliyeyepo, na whoever atakaye chaguliwa, JK ndiye mkabidhi!, jee atajikabidhia tuu kwa sababu wananchi wamesema au?!.

Kwa taarifa tuu matokeo halali ya uchaguzi, sio zile kura zilizopigwa bali ni zile zitakazo tangazwa!. Nasisitiza mshindi kupatikana by vetting, hata kama votting imesema ni fulani, vetting ndio itaamua atangazwe nani!. Waulizeni CUF wawaambie kilichikuwa kinatokea kwenye chaguzi zote Zanzibar na kilichukuwa kinatangazwa!.

Washaurini viongozi wa Chadema, waanze kuzungumza in good terms na Mwamunyange, Rashid Othman na Saidi mwema, ili pia wapite kwenye vetting!.. vinginevyo...!

kaka mimi naamini Vetting iliishafanyika siku nyingi tu, wewe subiri utaona.
 
Lowasa ana siasa kama za Mwingulu Nchemba. Hawa watu ni hatari sana. Lowasa fisadi , jizi nalo linataka kwunda ikulu.

Bora lijue Arusha hamna lake.
 
Nchi inakabidhiwa by vetting not by votting!.
Rais wa nchi ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama!. Hata ikitokea chama fulani kikamsimamisha a very popular linatic, akachaguliwa, jee atakabidhiwa?!. Utawala wa nchi una change hands kwa exchange of instrumetns of power ikiwemo kuapishwa na kukabidhiwa vyombo vya dola, wanaofanya hayo ni wale wapiga kura au nu yule mwenye navyo?!. JK ndie rais aliyeyepo, na whoever atakaye chaguliwa, JK ndiye mkabidhi!, jee atajikabidhia tuu kwa sababu wananchi wamesema au?!.

Kwa taarifa tuu matokeo halali ya uchaguzi, sio zile kura zilizopigwa bali ni zile zitakazo tangazwa!. Nasisitiza mshindi kupatikana by vetting, hata kama votting imesema ni fulani, vetting ndio itaamua atangazwe nani!. Waulizeni CUF wawaambie kilichikuwa kinatokea kwenye chaguzi zote Zanzibar na kilichukuwa kinatangazwa!.

Washaurini viongozi wa Chadema, waanze kuzungumza in good terms na Mwamunyange, Rashid Othman na Saidi mwema, ili pia wapite kwenye vetting!.. vinginevyo...!

Pasco.
Haya ni mawazo ya mtafuta Ukuu wa Wilaya! So low!
 
This is a good observation. Those concerned especially those from the opposition parties should take note of this observation. And we voters let also watch them with a macroscopic eyes so that come next election they should be ready to account for what they have done for us in the course of five years. Lets us now not allow money to be a stimulant to vote for a certain party. Let our education we got from schools and universities help us decide on the ballot box who our next leader would be. Thank you all for your consideration.
 
Kuna ukweli mmoja haujasemwa; Katika maeneo ambayo TLP, NCCR-Mageuzi au CUF walikuwa vyama vyenye nguvu, Wananchi wake wako tayari kurudia ccm na si kuchagua mpinzani mwingine. Tujiulize ni kwa nini? Hiki kiashiria ni muhimu sana kuking'amua tunapofanya tathmini kama kweli tuna dhamira ya kutumia takwimu hizi kama somo na nyenzo muhimu kupanga mikakati kwa ajiri ya 2015
TLP – Lost 1 to CCM
CHADEMA – Gained 5 from CCM
CHADEMA GAINED 5
CUF – Lost 1 to CCM
CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)
CCM LOST 3
CCM – Lost 5 to CHADEMA

TLP – LOST 1
CHADEMA - none

CUF – LOST 1
 
Haya ni mawazo ya mtafuta Ukuu wa Wilaya! So low!
Mkuu Awo, cheo cha U-DC ni cheo kikubwa sana kwangu, na mshahara wake na marupurupu yake manene sana, wengi wanautamani, ila amini usiamini, kuna wengine wetu tumezoea shida kiasi kwamba hatuzitamani kabisa hizo posti za kupewa!. Mimi tangu 2002 I'm on my own, more than 10 years now!, situmwi, natuma!, although I don't make much, kuniambia nasotea tena kuja kutumwa kwa take home ya DC, ni kunishusha sana!. Kwa vile CCM ndio mpango mzima wa dili zote za kukomba fungu, nikikwama kabisa, nitakata kadi ya CCM na kupiga hodi Ikulu kuomba kazi ya U DC na kwa CV yangu na uzoefu, nitapata ili nianze tena kutumwa na kuyaka asubuhi kuwahi kazini. Tena nitashauri nipangiwe kuwa DC wa Hai au Karatu, ili niwashughulikie ipasavyo jamaa zangu wawili hawa kabla ya 2015 ibakie hadithi tuu!.

Hivi unajua kuna watu fulani fulani wanatafutwa na maisha mazuri, wao hawapendi kisa wamezoea shida?!, hata raha zikiwaita wanazigomea wao wanatafuta tuu shida?!. Kwa mfano namuonea raha sana mwalimu wangu mmoja wa pale UD alikuwa ni mkuu wa idara na level ya kukaribia kabisa kuwa Prof, ati na yeye sasa ni DC!. Just imagine Pasco wa PPR, anaeroll almost that much wakati wa Saba Saba pekee, leo anakuwa DC kusubiria ...mwisho wa mwezi!.
Please gi'me a break!.

Pasco.
 
Kuna ukweli mmoja haujasemwa; Katika maeneo ambayo TLP, NCCR-Mageuzi au CUF walikuwa vyama vyenye nguvu, Wananchi wake wako tayari kurudia ccm na kuchagua mpinzani mwingine. Tujiulize ni kwa nini? Hiki kiashiria ni muhimu sana kuking'amua tunapofanya tathmini kama kweli tuna dhamira ya kutumia takwimu hizi kama somo na nyenzo muhimu kupanga mikakati kwa ajiri ya 2015
TLP – Lost 1 to CCM
CHADEMA – Gained 5 from CCM
CHADEMA GAINED 5
CUF – Lost 1 to CCM
CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)
CCM LOST 3
CCM – Lost 5 to CHADEMA

TLP – LOST 1
CHADEMA - none

CUF – LOST 1
Yes you are right. This message should go to Mbowe, Mbatia and Prof. Lipumba.
 
uchambuzi mzuri sana kaka,KIUKWELI LAZIMA VYAMA VYA SIASA VIUNGANE LAKINI KUNA VYAMA WAO NI WAFUASI WA CCM,LOOK LIKE TLP anajulikana mrema tu,UDP anajulika CHeyo tu,wengine wako wapi?katibu makamu wa mwenyekiti,katibu muenezi?angalia CUF wao pamoja na miaka yote kupata ruzuku zaidi ya millioni 200 awajengi chama bara,wao wamengangana na MTATIRO tu na majungu yao ya kuita waandishi wa habari,but COOLITION ni nzuri ila lazima chadema wajiulize hivi vyama vina nia ya kweli ya kuingoa CCM?MAANA KUNA VYAMA WAO HATA WAGOMBEA WA MADIWANI HAWANA ILA WAO WANA WAGOMBEA URAIS dovutwa UPDP peter kuga mziray APPT MAENDELEO MTIKILA DP?KWELI?CHADEMA WAKOMAE WENYEWE HUKU KITAA WANANCHI TUMESHA ANZA KUWAELEWA
 
Mkuu Awo, cheo cha U-DC ni cheo kikubwa sana kwangu, na mshahara wake na marupurupu yake manene sana, wengi wanautamani, ila amini usiamini, kuna wengine wetu tumezoea shida kiasi kwamba hatuzitamani kabisa hizo posti za kupewa!. Mimi tangu 2002 I'm on my own, more than 10 years now!, situmwi, natuma!, although I don't make much, kuniambia nasotea tena kuja kutumwa kwa take home ya DC, ni kunishusha sana!. Kwa vile CCM ndio mpango mzima wa dili zote za kukomba fungu, nikikwama kabisa, nitakata kadi ya CCM na kupiga hodi Ikulu kuomba kazi ya U DC na kwa CV yangu na uzoefu, nitapata ili nianze tena kutumwa na kuyaka asubuhi kuwahi kazini. Tena nitashauri nipangiwe kuwa DC wa Hai au Karatu, ili niwashughulikie ipasavyo jamaa zangu wawili hawa kabla ya 2015 ibakie hadithi tuu!.

Hivi unajua kuna watu fulani fulani wanatafutwa na maisha mazuri, wao hawapendi kisa wamezoea shida?!, hata raha zikiwaita wanazigomea wao wanatafuta tuu shida?!. Kwa mfano namuonea raha sana mwalimu wangu mmoja wa pale UD alikuwa ni mkuu wa idara na level ya kukaribia kabisa kuwa Prof, ati na yeye sasa ni DC!. Just imagine Pasco wa PPR, anaeroll almost that much wakati wa Saba Saba pekee, leo anakuwa DC kusubiria ...mwisho wa mwezi!.
Please gi'me a break!.

Pasco.
I rest my case.
 
Kwa tathimini nzuri na uchambuzi wa kina uliofanya ni kwamba CCM imeshindwa kabisa na upinzani CCm 49% na upinzani 51% hapo hata kwa kukokotoa upinzani 2015 unatoa raisi
 
Mkuu Mtu wa Shamba,
Kwanza asante sana kwa tathmini iliyokwenda shule.

Tathmini yako inaonyesha wazi CCM is loosing big time na Chadema id gaining big gain!.

Kwa upande wangu, kushinda au kushindwa ni matokeo, nataka nijikite zaidi katika the reasons behind that loss or gain kwa vyama viwili tuu, CCM na Chadema tuu!.
Nikianza na CCM.
CCM imepoteza ama kutokana na kuchokwa, kukosa mvuto, au kuadhibiwa kwa kupigiwa kura za chuki kufuatia kampeni chafu, siasa za majo taka, na baadhi ya mbinu chafu inazotumia kisiasa, kubakia watu kesi, matumizi mabaya ya vyombo vya dola, mauaji, etc, kwa kifupi CCM imeangushwa kwa chuki, hasira na kuchokwa na sio kwa sababu haijafanya kitu!.
Nikija kwa Chadema
Chadema kimeendelea kupata ushindi mnono kutokana na kupendwa!. Nakijiuliza Chadema kimefanya nini kustahili kupendwa huku, sioni kitu!. Chadema kinaendelea kushinda kwa sababu CCM imechokwa, na inachukiwa, hivyo kuna maeneo hata Chadema wangesimamisha jiwe, jiwe lingeshinda!. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa baadhi ya ushindi wa Chadema kwenye uchaguzi wa 2010, kuna wabunge na madiwani wa Chadema wameshinda, ukiangalia any substance ya ushindi wao, huioni, ila wameshinda simply kwa sababu CCM imechokwa!.

Kuelekea Uchaguzi wa 2015.
Kwa Upande wa CCM
Kufuatia CCM kuchokwa baadhi ya maeneo, CCM itaendelea kushindwa hata itafanya nini!. Mfano jimbo la Ubungo, by 2015, serikali ya CCM itakuwa imeishakamilisha kujenga barabara za juu kwa juu (fly over) pale makutano ya Ubungo, na mabasi ya mwendo kasi yakiranda kwenye njia zake jijini Dar es salaam, hivyo itajiamini sasa itapendwa wanananchi watakuwa wameshuhudia maendeleo kwa macho yao wenyewe, hivyo sasa wataichagua tena CCM!, no way!. Salama ya CCM kwa 2015 ni kukubali kubadilika na kujiandaa kwa co-existance na wapinzania kuwakubali kuwa hawa sio maadui bali ni washirika wenza katika utawala wa taifa hili, wawapende, wawakubali, na wajiandae kushirikiana nao vinginevyo ....
Kwa Upande wa Chadema.
Wasiendelee kuvimba kichwa kwa kupendwa na kubetweka kwa ushindi uliopatikana kwa muchukiwa kwa CCM!, ili Chadema kiweze kwenda Ikulu, it has to give out reasons za kuichagua besides ushindi wa kura za walioichoka CCM!. Jee Chadema ikishinda, inataraji kufanya nini Ikulu tofauti na CCM?!. Hicho Chadema inachotaraji kufanya, ndicho kiwe sababu ya kuiingiza Ikulu, na sio huu ushindi wa ubwete kinaupata kwa sasa kwa sababu tuu CCM imechokwa!.

My Take.
Naendelea kuipongeza Chadema kwa kukubalika, bali bado naendelea kulitoa angalizo lile lile kuwa kwa uongozi wa nchi kuelekea 2015, Chadema bado haijajipanga!, rejea hapa.

Ila pia Mkuu Mtu wa Shamba, nimeipenda sana hii statement yako
"Maadui huungana na kuwa rafiki wanapokuwa na tishio la pamoja. Vyama vya upinzani visipoona hivyo, CCM itaendelea kudumu miaka mingi sana ijayo, japo kwa kura kidogo zaidi na zaidi".
Naemdelea kuwasisitiza Chadema, peke yenu hamuwezi!. Japo rasimu ya katiba mpya inapendekeza serikali tatu, Watanzania wanaweza kuamua wanataka serikali mbili, hivyo ili chama kishinde, ni lazima kipate angalau theluth moja ya kura kutoka kila upande!, siioni theluth yoyote ya kura za Chadema kutoka visiwani. Japo CUF ni chama adai kwa Chadema kutoka na usharika wake na CCM, Chadema has to find a common denominator ya kushirikiana na adui for fighting a common enemy!, vinginevyo 2015 wapinzani watagawana kura na kujikuta CCM ikiendelea kuongoza kwa simple majority, wakati kama wange join forces, wanaweza kabisa kuiweka kando CCM!.
All the best.
Pasco.

Si sahihi kusema CHADEMA ina shinda kwasababu tu ccm imechokwa, CDM imejipambanua kwa wananchi kama chama chenye kuleta matumaini zaidi na ukombozi wa kweli ma tatizo sugu yanayowakabili watanzania toka Uhuru na mengine mengi ya hovyo yaliyoasisiwa na ccm kama Ufisadi, Chama kukosa viongozi wenye uwezo wa kuongoza na kazi za siasa kufanywa na polisi, chama kukabidhiwa genge la vijana wahuni wajifanyie wanachotaka na ccm kuwa kampuni badala ya chama cha umma.
 
1016236_674006945946158_966358015_n.jpg
 
Back
Top Bottom