for the first time in last 12 months tumepata mtu anayeweka analysis ambayo ni ya kisomi, yenye takwimu na isiyopendelea wala kushabikia upande wowote..THANKS MTU WA SHAMBA Kwa kutupa uwanja wa kujadili kwa kuzifikirisha bongo zetu na sasa ninadhani ni ruhsa kwa wale wanaofikiri ki-vyama kuikokotoa post kwa mitazamo ya mapenzi ya vyama vyao.
1.KWANZA NIANZE NA NAFASI YA CCM KATIKA SIASA ZA TANZANIA KATIKA MIAKA 5 ILIYOPITA.
ni mtu mjinga tu na asiyependa kukubali ukweli atakayekataa kuwa ndani ya miaka mitano iliyopita CCM imekutana na changamoto kubwa kiushindani kuliko kipindi chochote katika historia yake.
ni katika kipindi hiki ambako zile kashfa kubwa zilizofanyika katika utawala wa awamu ya tatu(under mkapa regime) zilihamia kwenye majukwaa ya siasa na muhanga mkubwa akawa ni CCM(na ilistahili) na katika kipindi hiki ndio chama cha CHADEMA kikawa na safu ya watu wenye uwezo wa kujenga hoja na kushawishi hadhira hata kama hoja waliokuwa wanaiongelea ni UZUSHI NA UONGO MTUPU.. kwa kubweteka na kudhani ukubwa na ukongwe wake ndio immunity!! CCM ikawa imapuuza na kuzibeza harakati za CDM bila kuona athari za waziwazi katika kupoteza uungwaji mkono miongoni mwa wananchi. mpaka walivyokuja kushituka CDM ikawa imekwisha pata nguvu katika maeneo mengi ya mijini hapa nchini na kujizolea wafuasi wengi.
kikubwa kinachoiweka CCM katika hadhi tofauti na vyama vingine na kukifanya kuwa chama tawala kwa miongo kadhaa ijayo ni UWEZO MKUBWA WA KUHIMILI MISUKOSUKO, KASHFA. MIFARAKANO BAINA YA VIONGOZI, DEMOKRASIA NDANI YA CHAMA NA KUPIMA UPEPO WA MATUKIO NA JINSI YA KU-DEAL NAYO.
hapa ndipo CCM inapopewa credity na mchambuzi yeyote wa kisiasa, imeweza kuhimili mashambulizi mfulizo tena ya kiwango cha kutisha toka CDM, imeweza kuhimili migongano na minyukano miongoni mwa viongozi wake waandamizi na imeweza kuhimili vuguvugu la mabadiliko linaloendelea kote duniani bila kutetereka.
kwa anayejua kuzifuatilia siasa za tz, hivi sasa ataona kuwa CCM hawajihami tena dhidi ya mashambulizi toka chadema bali wao nao wameshaanza kushambulia. athari za mashambulizi ya CCM kwa CHADEMA ziko wazi, ile taswira ya CHADEMA mbele ya jamii imeshaanza kuchafuka, kuna watu wengi tuu miongoni mwa watz ambao wanaiangalia CDM kwa jicho la MASHAKA na nina hakika hata ile EXPANSION YA chadema imeshadhibitiwa na kitakachofuata ni kuondolewa taratibu katika yale maeneo waliyoyateka( ntakuja na ushahidi kuhusu hili siku nyingine).
2. UZUSHI JUU YA CHADEMA KUENEA KUTOKA VIJIJINI KUELEKEA MIJINI
Nadhani tuwe wakweli kwa kulinganisha mambo kutokana na uhalisia wake,
leo hii, ARUSHA, MBEYA, MWANZA na DODOMA ni majiji kama lilivyo DAR ES SALAAM. kuita kuenea kwa CHADEMA toka maeneo hayo eti ni kupanuka toka vijijini na kuelekea mjini ni uongo wa wazi. labda tuipate upya tafsiri ya neno MJI na KIJIJI, Lakini kwa tafsiri tunayoijua kwa ujumla, huwezi ukasema MSIGWA,SUGU,G.LEMA,NDESAMBURO,WENJE na wengineo eti wanawakilisha watu wa vijijini pale bungeni.
ukweli ni kwamba,CHADEMA kama vilivyo vyama vyote vaya kisasa duniani, vinakubalika zaidi mijini na kama kupanuka vinapanuka toka mijini kuelekea vijijini na hata uchaguzi wa 2010 unadhihirisha na kuonyesha direction of expansion ya chama kama utaangalia kwa makini.
3. KINACHOIANGUSHA CHADEMA NA KUIPA NGUVU KUBWA CCM HUKO TUENDAKO
kama nilivyatangulia kusema hapo mwanzo, kwamba CCM wako in OFFENSIVE, ni wazi mashambulizi yao wanayaelekeza kwa CHADEMA. na chadema hawatakubali kamwe kukaa tu bila kujilinda na kujitetea kutokana na mashambulizi toka CCM, hivyo basi mkakati wao wa kushambulia utakuwa paralysed kwa sababu hawana ENOUGH ORGANISED TEAM TO DEFEND AND ATTACK AT THE SAME TIME(offence/diffence). na hilo limedhihirika jinsi ambavyo KUANZIA UONGOZI WA JUU KABISA WA CHADEMA hadi makada wa chini kabisa wanavyohangaishwa na mtu mmoja tu toaka CCM anayeitwa MWINGULU NCHEMBA. huu ni udhaifu mkubwa sana kitimu na kitaasisi. leo hii kama CCM itaanza mashambulizi toka kwa watu wengi tofauti wenye mtindo wa mwingulu nchemba, ni wazi kabisa CHADEMA kita-collapse ndani ya muda mfupi sana. kigezo cha pili ni jinsi ambavyo CHADEMA bado zinawekeza nguvu nyingi kupita kiasi katika maeneo ambayo walishayatangaza kuwa ni ngome zao( hii inaonyesha bado hawajajiamini katika ulinzi wa ngome zao na kwamba muda wowote ngome zinaweza kutekwa). rejea uchaguzi wa madiwani wa arusha ulioisha jana.hii inawapunguzia sana nguvu ya kujitanua na kutengeneza ngome mpya na hivyo kuendelea kuwa grounded on the same grounds and never expand.
4. KAULI ZA VIONGOZI NA WAFUASI WA CHADEMA NI KUROPOKA NA KUASHIRIA SHARI
Kuna dhana imejengeka miongoni mwa viongozi wa chadema na wafuasi wao kuwa eti'WATU WAMECHOKA'.
WAMESAHAU KUWA HAKUMA MWANADAMU ANAYECHOKA KUISHI.Wanapopata wafuasi katika mikutano yao ya hadhara wanajenga taswira kuwa wale ni mbuzi/farai/nguruwe wasio na akili ambao wakiambiwa chochote watakifuata. na kwa kujidanganya huko, wamejenga kiburi na majivuno juu ya dhana kwamba wao wako juu ya sheria, wanaweza kusema na kutenda lolote kwa sababu eti PEOPLE'S POWER iko nyuma yao.
wamefikia hatua ya kutunga uongo na kuuamini wenyewe, kufarakana kwa makusudi na vyombo vya ulinzi na usalama, kuchochea ghasia na maasi, kuchochea watu kutokufanya kazi wala kuchangia shuhuli za maendeleo na kufurahia pale serikali inaposhindwa kutumikia ipasavyo wananchi.
hawa viongozi na wafuasi wa chadema, wameshajitenga na taifa hili la tanzania na wako sambamba na maadui wa nchi yetu eti kwa sababu tu tanzania iko chini ya utawala wa CCM!!!! kamwe hawashangilii neema yoyote inayopatikana tanzania, hawaoni lolote jema chini ya anga la tanzania,wako tayari kujiunga na jeshi la (MSEVEN/KAGAME/BANDA/KENYATA) au yeyote atakayetaka kutushambulia kwa vile tu tuko chini ya utawala wa CCM. NA hili tunaliona humu J.F na tunawasikia hata mitaani jinsi ambavyo wanaropoka kauli ambazo zinakikosesha chadema sifa za kuwa mbadala wa CCM.
Nilipata kuwa katika miji mikubwa ya ZAMBIA wakati LEVY MWANAWASA akishinda uchaguzi katika awamu ya pili na jinsi PF(PATRIOTIC FRONT) KILIVYOKUWA kinazidi kujitanua kuelekea vijijini, nilishuhudia jinsi matokeo ya kushindwa kule yalivyowapa furaha na matumaini ya ushindi baada ya miaka mingine mitano, na katika bahati isiyo ya kawaida, nikawepo tena wakati MICHAEL CHILUFYA SATA na PF yake walivyoshinda ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa miaka 3 iliyopita.
dicpline katika utendaji na kutanguliza uzalendo ndio mambo ambayo waafrica wengi wanayataka.waafrica wengi wameshachoshwa na vita na mapigano ambayo yanawafaidisha wanasiasa.
kwa kiburi cha uongozi wa chadema pamoja na wafuasi wao,leo hii wameshakinasibisha chama chao na vurugu, ghasia na vita. na hawachukui hatua yoyote ya kuzuia hali hiyo zaidi ya kujenga mazingira ya kuthibitisha kuwa wao(chadema) wamejipanga kivita zaidi kuliko kujipanga kisiasa. hali hii inawatia doa na kuondoa umaarufu wao katika hadhi ya chadema.
mmetegewa mtego nanyi mmeingia kichwa kichwa na kitanzi kimekaa tayari shingoni.
noja niwafumbue macho kidogo......
watu wenye busara zao ndani ya taifa hili walishaiona dhamira chafu ya waasisi wa chadema tangu mwanzo. ila kwa sababu walitaka kuijua kwa ushahidi, wakaamua muendelee kufanya siasa zenu bila bughudha ili ile dhamira yenu ije kuonekana wazi.
mkafika mahali mkabweteka, mkajidanganya kuwa raisi J.K ni dhaifu na hivyo mkaamua kujiachia na kujisahau na mwisho mmeonyesha hata zile dhamira zilizojificha. mmejivua nguo mbele ya jamii ambayo ilishaanza kuwategemea, mmejiweka katika hali ngumu ya kuelekea anguko ambalo litaifanya CHADEMA IWE HISTORIA.
MMECHAGUA UPANDE WA MACHAFUKO NDANI YA NCHI AMBAYO HAKUNA MACHAFUKO NA WATU WAKE NI WAPENDA AMANI???
Hilo ni kosa amabalo mtakuja kulijutia milele.
Asante mkuu kwa mchango wako.
Naomba nikujibu kwenye namba 3 na 4.
Ni kweli CCM wanaishambulia Chadema. Lakini wanaishambuliaje? Nilivyoshuhudia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mashambulizi yameelekezwa
1.Kwenye kuwaaminisha wananchi kuwa Chadema ni Wahalifu. Hili linafanyika kwa kufungua kesi nyingi, ambazo kwa bahati mbaya nyingi zinaishia kufutwa kwa kukosa ushahidi, hatimaye madhara ya shambulio yanarudi kwa CCM wenyewe.
2. Kuhusisha Chadema na fujo na mauaji. Hili pia linaweza kuwa limeaminiwa na watu wa CCM na wengine ambao hawakujipa muda wa kutafakari vizuri. Kwanza Polisi haruhusiwi kutumia risasi za moto isipokuwa katika mazingira ambayo wanalazimika kujilinda maisha yao, au mhalifu hatari anapojaribu kutoroka na hapo wanapaswa kulenga miguuni. Polisi wanapoua katika mazingira kama aliyouawa Mwangosi, hilo ni doa kwa serikali na polisi wenyewe kwani askari 7 walio na silaha wamekamata mtu asiye na silaha, hakukuwa na hoja ya kujilinda. Hili nalo linaichafua serikali na chama cha mapinduzi.
Ndio maana Chadema waliomba uchunguzi ufanywe na Tume Huru ya Kimahakama kubainisha kama ni Chadema wanahusika na mauaji hayo au la? Kwa nini serikali haiundi tume hiyo?
3. Propaganda ya Udini na Ukabila: Hii pia imeigeuka CCM kwani watu wanaona watu kama akina Zito Kabwe, Prof. Safari, na vijana kama akina
mohamed Mtoi ni wanachama na wana nafasi yao kama wanachama, na hata uongozi.
4. Mashambulizi binafsi hasa kwa Dr. Slaa, Mbowe na Lema. Haya naomba wewe mwenyewe ufanye tathmini yako binafsi uone kama yameijenga CCM na kuidhoofisha Chadema.
5. Hicho unachoita dhamira chafu mimi sijakiona. Mimi nina watu wengi sana wasomi na waelewa wa mambo na wengine wamo serikalini na kwenye vyombo vya dola, lakini tunapoongea hakuna anayeisema hiyo dhamira chafu. Labda uwe wazi ni dhamira ipi chafu?
6. Mengi yanayopigiwa propaganda juu ya uhalifu wa Chadema, kama yangekuwa na ukweli yangepelekwa kwenye mkondo wa shéria na si kwenye majukwaa ya siasa. Kwenye mkondo wa sheria kwa sababu sheria ya vyama vya siasa inakataza kusajili chama cha UGAIDI, UKABILA, UDINI, FUJO. Jiulize kwa nini mambo ya kisheria yafanywe ya kisiasa kama si propaganda?
Naomba niseme kuwa iwapo wewe bado kwa dhati unaamini kuwa
Mwigulu Nchemba anajenga chama, na iwapo huu ndio msimamo wa wana CCM walio wengi, na kwamba mmeridhika kuwa ndio mkakati wa kuiua Chadema, nakwambia kuwa endeleeni kumtumia, na endeleeni kutumia mbinu hizo hizo. Lakini badala ya kuua Chadema mtaua CCM.
Chama cha siasa ni lazima kitengeneze mvuto kwa wananchi. Mkakati wenye mapato ya muda mrefu ni ule unaoshawishi watu wakipende chama kwa mazuri yake, na si kwa mabaya ya wapinzani wake. Chama cha siasa chenye malengo ya muda mrefu, ni lazima kiwe na ajenda za kujiuza chenyewe na mara moja moja kuonyesha udhaifu wa wapinzani wake. Alichofanya Mwigulu Arusha, kuonyesha kuwa Chadema ni wauaji, Chadema ni waongo, Chadema ni wafanya fujo, Chadema wanataka kula Halmashauri kilisikika kwa watu. Lakini Mwigulu alipoteza fursa ya kuelezea uzuri wa CCM na mipango ambayo CCM wanayo kwa wana Arusha.
CCM ikiona umuhimu wa kutathmini haya ni vema, la sivyo mtaendelea kushangaa kwenye masanduku ya kura, huku mkiendelea kulia na propaganda zilizokataliwa na watu.