Chaguo Sahihi?

Chaguo Sahihi?

Kwani ulimuoa ili kumfurahisha nani?na kama ulimpenda kwa ridhaa yako mwenyewe mbaka ukafikia hatua ya kumuoa, kwa nini sasa unamchukia?
 
Naombeni Msaada wenu wa mawazo tafadhali,Mimi ni Mkristo nina mke lakini nahisi nilifanya uchaguzi usio sahihi maana sina hisia nae kabisa japo tumezaa pamoja mtoto,najitahidi Kumpenda lakini wapi naombeni msaada wenu nifanyeje?je kumwacha ili nisiendelee kumuumiza inawezekana?kidini ikoje hiyo?
Hakuna kuacha....Jifunze kumpenda
 
hahahhahhahahhahahah have a coke tu bana!
au mtu aniambie maana ya uasherati!ila kama ni huu huu naoujua mie basi ndoa nyingi sana sio halali yailahi! kwa haya mambo nayoyaona mie mpka umri huu!lolz

ndo maana kuna kusameheana hii ni pale tu unaposhindwa kusamehe hata kanisa lintakua radhi ivunjwe hiyo ndoa
 
Hamna ndoa siku hizi.....!!!!

Ila mwanaume na mwanamke wanaoishi pamoja....
 
Naombeni Msaada wenu wa mawazo tafadhali,Mimi ni Mkristo nina mke lakini nahisi nilifanya uchaguzi usio sahihi maana sina hisia nae kabisa japo tumezaa pamoja mtoto,najitahidi Kumpenda lakini wapi naombeni msaada wenu nifanyeje?je kumwacha ili nisiendelee kumuumiza inawezekana?kidini ikoje hiyo?

hata sijui nisemeje ila ndoa za kikristu hapo ndo ntolee,,
 
Kwanza nikupe hongera kwa kukifikia kituo hiki cha 'loss of marital bliss' a.k.a 'feelings' ukiwapo ndoani bado...Labda nikuambie kwamba hata ukiwa peke yako, kuna mda maisha yanapoa sana kiasi cha kutokuwa na meaning kabisa!
Sasa ukifikia hapa haina maana kwamba ndio muda wa kujiua umefika. Ni juu yako kuurudisha.

i) Hakuna incompatibility tena once ndoa imefungwa. God can make the bond perfect, honestly kama kungekuwa na kitu kama 'incompatibility' kwenye ndoa then biblia ingesema. Unafikiri Mungu hajui hiyo hali ya ndoa yako? kwamba hajui wengi watafanya makosa katika uchaguzi?

ii) Labda nikuoneshe hiki. Love that results from friendship.Unakaa na mtu kwa mda mrefu then u wake up in the morning and you are in love with them. Ili hizo chemical zinazosababisha feelings zirun in your body then inabidi vitu vingi vifanyike. Kwanza anzisha tena casual relationship, ongea naye kama rafiki tu share matatizo yenu na mtafute solution pamoja. Jaribuni kufanya majukumu ya familia( KUPIKA, KUFUA, KUFANYA USAFI NJE NA NDANI) pamoja, nendeni kwenye vikao vya kijamii pamoja. Kisha tumieni muda wa ziada pamoja. Tena ikiwezekana muambiane tunafanya kazi kwa mutual agreement hakuna kulazimishana na kulaumiana ni mwiko.

iii) Through sharing your love will bloom again....na ni kitu kidogo tu kitaleta hizo feeling. You can love someone simply by their dedication in cleaning your place...Labda umeacha kuspend time nyumbani ukaona jinsi mkeo anavyojitolea kuhudumia familia ndio maana humuoni wa maana tena. Honestly if you take into account everything she does utaona tu strength zake.
Asante kwa ushauri nitajitahidi japo najifeel tofauti sana
 
Hiyo ni hali ya kawaida kwa sisi binadamu, haiwezekani kumpenda mkeo/mmeo kama ulivyokuwa ukimpenda mwanzo (miaka 10-15 iliyopita) hapo mnaishi kwa kuzoeana tu na si kwa hisia za kimapenzi, kwa kifupi mnakuwa na upendo wa nusu ndugu nusu wapenzi, hata mmoja akifa atakaebaki atajisikia uchungu wa kindugu au kimapenzi inategemea mlikuwa na muda gani katika ndoa.
 
ndo maana kuna kusameheana hii ni pale tu unaposhindwa kusamehe hata kanisa lintakua radhi ivunjwe hiyo ndoa

kuna kanisa linavunja ndoa kwa ajili ya kushindwa kusamehe? Suprise umeolewa?(nahisi we ni mdada samahani kama nimekosea)
una miaka mingapi kwenye ndoa yako?marafiki na ndugu na staff wwenzio wanaizungumziaje ndoa?
 
Last edited by a moderator:
kuna kanisa linavunja ndoa kwa ajili ya kushindwa kusamehe? Suprise umeolewa?(nahisi we ni mdada samahani kama nimekosea)
una miaka mingapi kwenye ndoa yako?marafiki na ndugu na staff wwenzio wanaizungumziaje ndoa?

hahaha kumbe me mdada eenh, snowhite mwaya hata mlango wa ndoa cujui mie
 
hahaha kumbe me mdada eenh, snowhite mwaya hata mlango wa ndoa cujui mie

kuna kanisa linavunja ndoa kwa ajili ya kushindwa kusamehe? Suprise umeolewa?

hakuna kanisa linalovunja ndoa kwa ajili ya kushindwa kusameheana bt kuhusu uasherati kama mmoja wenu kashindwa kusamehe hapo hata kanisa linaruhusu ivunjwe
 
Naombeni Msaada wenu wa mawazo tafadhali,Mimi ni Mkristo nina mke lakini nahisi nilifanya uchaguzi usio sahihi maana sina hisia nae kabisa japo tumezaa pamoja mtoto,najitahidi Kumpenda lakini wapi naombeni msaada wenu nifanyeje?je kumwacha ili nisiendelee kumuumiza inawezekana?kidini ikoje hiyo?
mi huwa napenda kutoa ushauri kwa kuuliza maswali kama hutajali!
-UNA MWANAMKE MWINGINE NJE YA NDOA YAKO?
-MARA YA MWISHO ULIMWANGALIA LINI MKEO KWA MAKINI?
-MKEO AMEBADILIKA UMBILE BAADA YA KUJIFUNGUA?
-UNAMHISI KITU CHOCHOTE KIBAYA WIFE?
-MARA YA MWISHO MMETOKA OUT NA MAMII NI LINI?
-ULISHAWAHI KUPIGA GAME OUT FIELD?
-MKEO ANAIHUDUMIA VIPI FAMILIA ?
-UNAAMINI UNAMRIDHISHA MKEO KIMAPENZI?
-UMEPATA TATIZO LOLOTE KIUCHUMI,KIHISIA,KIAFYA?
ni mengi lakini hebu yakusaidie katika kutafakari!
then tunaweza kuendelea!
-
-
 
hahaha kumbe me mdada eenh, snowhite mwaya hata mlango wa ndoa cujui mie

that explains a lot of things!
usijali mwaya ukifika utajionea!
nikwambie tu ndoa ni zaid ya hivi wengi tunavoistafsiri!
believe me!
 
sa ndo hutaki toa kitchen part before

wala usiwe na haraka mwali wangu!
we unialike tu wiki moja kabla ya harusi ntakuja na mke mwenzangu cacico pamoja kungwi mwenzangu gfsonwin hutojutia abadan!
bure sentano kipande hatutaki !twaja siye wenyewe!!na miguu yetu!
 
hahaha, noted, athante kwa promised huduma
 
Hizi kesi za ndoa, ni balaa!
Ndoa ya kikristo haivunjiki kwa mwenzi mmoja kukosa hisia kwa mwenzake labda kaw dhambi ya uasherati.
Muombe Mungu tu akusaidie manake duh!
Sasa na wewe ilikuwaje ukamuona mwanamke humpendi jamani tena ukaingia kichwa kichwa hadi mbele ya mchungaji, ona sasa. Ngaja FP, The Boss, Mzizi mkavu waje nadani wanaweza kukusaidia angalau kurudisharudisha hizo hisia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom