Chaguo la Mungu mwaka 2010 huyu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chaguo la Mungu mwaka 2010 huyu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Feb 24, 2010.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni wakati sahihi kwetu watanzania kujichagulia wenyewe chaguo la Mungu na si kuchaguliwa na wachache. Tumepata fundisho kuwa aliyedhaniwa kuwa chaguo la Mungu 2005 kumbe hakuwa. Si chaguo la Mungu kwa vile hasikii kilio cha watanzania walio wengi, haachani na mafisadi na haashi safari nyingi za nje kana kwamba maendeleo yetu yataletwa kwa safari zake. Rais wetu wa sasa afike mahali atambue kwamba nadharia ya maendeleo ya misaada imepitwa na wakati. Sayansi imekataa kuwa misaada kutoka nje inaleta maendeleo ya nchi.

  Hatukupata chaguo la Mungu mwaka 2005 kwa vile tuliangalia sura ya mtu, tulisikiliza maneno matupu ya mgombea, hatukutafuta historia ya Mgombea, tulidanganywa na watu wachache kuwa tuna chaguo la Mungu kumbe la. Sasa nani changu la Mungu mwaka huu 2010. Ni huyu hapa:

  1. Aliyethibitika wazi si kwa hisia kuwa amelinda maliasili ya nchi- Maliasili
  2. Aliyethibitika wazi si kwa hisia kuleta maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla wake
  si kuiba huku na kupeleke kwa wapiga kura-
  Maendeleo ya kweli
  3. Aliyethibitika kuwa hakuiba pesa za Watanzania ili kununua uongozi-
  Si mtoa
  rushwa wala hakutumia pesa za wizi
  4. Aliyethibitika wazi si kwa hisia kuwa ametetea katiba ya nchi yetu-
  Katiba
  5. Alitethibitika wazi kuwa anaipenda nchi yetu si kuleta wezi Tanzania kwa jina la
  wawekezaji-
  Mpenda nchi
  6. Aliyethibitika wazi kuwa ana dira sahihi ya elimu- si ubabaishaji wa maboma ya
  shule za kata-
  Elimu bora
  7. Aliyethibitika wazi kuwa anajali utu wa Watanzania si muigizaji huku anaenda
  safari akiacha watanzania wakilipukiwa na mabomu, wakifukiwa na milima,
  wakisombwa na mafuriko, wakifa njaa-
  Anayejali utu si msanii
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,074
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Na wale watanzania wasioamini Mungu, wao inakuwaje?

  Nimeipenda hii sentensi yako

  ''tulisikiliza maneno matupu ya mgombea, hatukutafuta historia ya Mgombea''

  aibu ya vizazi kwa CCM !
   
 3. Iramusm

  Iramusm JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 428
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Dk.Slaa anafaulu katika vigezo vyote saba ulivyoweka hapo juu..kwa mtazamo wangu.
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  nani, slaa, thubutu........................ ni JK kwa kwenda mbele................. rekodi yake ya utendaji inajieleza..................... napendekeza mgombea mwenza awe sophia simba ili amshauri kwa karib zaidi kuhusu uharaka wa kuchukua hatua inapolazimu kufanya maamuzi magumu................................
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana kabisa aliyesema kuwa Dr.Slaa anafaa kuwa rais wa Tanzania
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Mkuu sema chaguo letu! linakuwa la mungu pale tunapolichagua sisi
  kwa hiyo la akili kichwani ni SS??!! au
   
 7. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante
   
 8. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yote sawa
   
 9. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Onyesha hapa ni kwa namna gani huyo unayempigia upatu anakidhi kigezo kimoja baada ya kingine. Thibitisha kwa hakika bila kuleta hisia.
   
 10. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama wapo si wengi
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,867
  Likes Received: 2,620
  Trophy Points: 280
  Yes
   
 12. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 644
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Slaa si chaguo la mungu bali ana uelekeo mzuri wa kutufikisha tunapotaka. Naamini tukimpa tunaweza kumshuhudia Mkapa kizimbani. Atakayeweza kumfikisha Mkapa,Edrew Chenge, Edward Luasa, Kalamagi, Lostam, Edward Hosea ndilo litakuwa chaguo la Mungu .Vinginevyo halitokuwapo kabisa.
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hakuna chaguo la MUNGU katika kizazi hiki cha nyoka...wote wanachaguliwa na wanadamu,hata hao viongozi wa dini wenyewe hawachaguliwi na MUNGU sembuse kwenye siasa.
   
 14. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  swadakta!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  SS mi naona yuko fiti kushinda hata JK.......................
   
 15. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #15
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,074
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  alikusikia Kiranga, mi simo!
   
 16. Ndjabu Da Dude

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,857
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Ok. Hata chaguo la "Mungu" tuliyo naye saaivi ni mpenda "uchi" pia (kama ule wa "dokta" Kigoda...)
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Mkuu lazima ujue kuwa kama akimaliza kazi hiyo basi aondoke madarakani. Kama kweli mtu akiingia madarakani kwa ajili hiyo tu, akimaliza hiyo atafanya nini? au ndio ataanza kusafiri kila siku kwenda nje.

  Kingozi amabaye ni chaguo la Mungu huwa anafanya yale ambayo mungu atanataka, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kondoo wake wanapata malisho ya kutosha. Huyo ndio tunayemtaka, so far hatuna.
   
 18. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swali lako ni zuri sana, na la pekee kabisa yafaa ukilipost kwenye thread inayojitegemea ili kuwe na mtiririko mzuri wa mawazo kuhusu Mungu ni nani, asili yake, tabia yake, n.k.
   
 19. Ndjabu Da Dude

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #19
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,857
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Ok.
   
 20. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Ukiwa na mambo yafuatayo unashinda:

  1. Chama kinachokubalika na wapiga kura wengi.
  2. Ndani ya chama hicho wewe unakubalika na wengi.
  3. Fedha ya kutosha kupiga kampeni rasmi na zisizo rasmi
  4. Upepo.

  Haya manne yanatosha kuchaguliwa kuwa Rais wetu 2010. Ukishachaguliwa hata bila yoote yaliyoandikwa sijui maliasili, sijui ukaribu na wananchi, tayari wewe ni chaguo la Mungu. Kwa sababu usingeweza kuchaguliwa bila kuwa chaguo la Mungu.

  CCM wanalijua hili na ndiyo maana mgombea wa CCM ndiye atakayeshinda uchaguzi 2010, kwa hiyo mgombea wa CCM ndiye chaguo la Mungu. Hii ndiyo Tanzania leo.

  Kwa wale mnaotaka kula miaka mitano ijayo ya uongozi, jipendekezeni mapema CCM, acheni longolongo na migogoro ya kijinga ooh ufisadi ooh BOT, vinginevyo umri unakwenda huo hamna mali, hamna chochote. Acheni kusubiri mkono udondoke kama fisi.

  Msiwe wajinga, Kikwete atashinda uchaguzi huu hata Dr Slaa analijua hilo, siyo siri, sasa jipendekezeni mapema ili mfaidi matunda ya uhuru, acheni kusuasua, mtakufa maskini.

  Chadema msitumie ruzuku yenu kugombea urais kwa nguvu, mtapoteza hela bure, tumieni fedha yenu kugombea ubunge, Urais mwachieni Kikwete. Hamtamweza Kikwete nyinyi, Kikwete ni chaguo la Mungu. Kama mnabisha subirini muone.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...