Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
huu sio wakati wa kumpoteza dr slaa kwa sababu ya urais
Wewe una akili sana.
Mimi naona suala sio kushinda pekee, hata kama atashindwa lakini naona ataleta changamoto kubwa kwa JK katika uchaguzi kuliko kiongozi mwingine yeyote katika upunzani, na hata asilimia watakazopata wapinzani katika urais na ubunge zitaongezeka sababu ya changamoto yake. Hatapotea ila upinzani utaimarika. Lipumba, Mbowe wamegombea urais mara kadhaa ,hivyo hawapo bungeni, je tumewapoteza? I dont think so
..........
7. Aliyethibitika wazi kuwa anajali utu wa Watanzania si muigizaji huku anaenda
safari akiacha watanzania wakilipukiwa na mabomu, wakifukiwa na milima,
wakisombwa na mafuriko, wakifa njaa- [/SIZE][/FONT]Anayejali utu si msanii
Hivi mchango alioutoa Dr Slaa na changamoto aliyoileta kwenye bunge letu unalinganisha na changamoto waliyoileta Lipumba na Mbowe kwa kugombea kwao Urais. Tumia hekima yako nzuri uliyonayo upambanue hili.
Changamoto ya kweli ingeletwa na wapinzani kusimamisha mgombea mmoja.
.
nani, slaa, thubutu........................ ni JK kwa kwenda mbele................. rekodi yake ya utendaji inajieleza..................... napendekeza mgombea mwenza awe sophia simba ili amshauri kwa karib zaidi kuhusu uharaka wa kuchukua hatua inapolazimu kufanya maamuzi magumu................................
Hivi ile report iliyosema JK anaongoza kwa 75%
Mbowe 10%
Lipumba 9 %
wameitoa wapi???
'utafiti' umepikwa, ni uwongo wa kufumba macho watanzania kumchagua huyu chaguo la mungu wa mwaka 2010.
tafadhali eleza hilo chaguo la 2010 kama siyo ndugu yako, mchungaji wako au tajiri yako.
2. Aliyethibitika wazi si kwa hisia kuleta maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla wake
si kuiba huku na kupeleke kwa wapiga kura- Maendeleo ya kweli
3. Aliyethibitika kuwa hakuiba pesa za Watanzania ili kununua uongozi- Si mtoa
rushwa wala hakutumia pesa za wizi
Nadhani mkuu huyo mtu hayupo kabisa duniani, labda bado hajazaliwa.
Sijui wewe ni muumini wa Kakobe au vipi. Nashangaa sana unaposhindwa kuelewa kwamba maandiko yanatuagiza tuheshimu walioko kwenye mamlaka kwa kuwa mamlaka zote hutoka kwa Mungu. Sasa wewe unapingana na Mungu unaposema mamlaka yaliyopo siyo chaguo lake? Je wataka kumchagulia Mungu mamlaka unayopendezwa nayo wewe na si yeye? Basi kama umeshaona mamlaka iliyopo haitoki kwa Mungu tueleze wazi ni nani anayetakiwa na Mungu kuwepo uchaguzi ujao kwa maana pengine ameshakushushia Roho wake akuongoze. Tafadhali tujuze usilete porojo hapa ndani ya JF