Chaguo la MUNGU Linalohitaji Mizengwe ya Mwanadamu Kufanikiwa

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,931
71,549
Sijaelewa pale tunaposema "Hili ni Chaguo la MUNGU" lakini ili chaguo hilo litimie inabidi sasa wanadamu watumie njia na mikakati ya siri, vitisho na ghiliba ili kuhakikisha chaguo hilo la MUNGU linatimia.
Jee ni kweli kuwa Mwenyezi MUNGU wa kweli anahitaji wanadamu tutumie nguvu, mikakati, mizengwe na hila kuwadhibiti wale wasiotaka chaguo la MUNGU litimie? Hawa wasiotaka Chaguo la Mungu wana nguvu kiasi gani kupingana na MUNGU hadi ahitaji tumsaidie kuwashughulikia?
Ni chaguo la Mungu kweli au tunatumia jina lake kwa manufaa ya kibinadamu?
 
dini na siasa ni sawa na kuna. mchungaji mmoja alisha wahi kusema matendo ya mungu na shetani yanaendana ila siku mfuatilia sana ili nijue akilikua anamaanisha nini.
 
Ukipata jibu tuoatie,, ingawa pengine 'chaguo la Mungu' tunaweza kuwa limeshafanikiwa humo Dodoma kwa nguvu za kina Bulembo &co
 
Tanzania hakuna viongozi wa dini isipokuwa mmoja..I mean wa kiroho.....wote ni wasaka tonge kwa mgongo wa dini

Yuko mmoja tu ...na huwezi kusikia anaongelea hii mambo ya siasa.....Mwalimu Chriss
Ndugu yangu umeandika vema lakini naomba nikurekebishe kidogo.. Ukisikia mtu au watu wanajiita Viongozi wa Dini, basi tambua kuwa hao si WATUMISHI WA MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI NA VYOTE VIIJAVYO. Bali ni viongozi wa WASLAHI NA MAKINDI BINAFSI YA WASAKA TONGE KWA MANUFAA YAO NA WALE WALIYO WATUMA.. Ndiyo maana utakuta viongizi hao wa dini wako na mwegemeo wa TAASISI FULANI YA KISIASA KWANI WANASHIBA KUPITIA KWAO. Katika Maandiko au kwa wale Wakristo wasomao Biblia, hakuna sehemu utakutana na mstari wa maandiko matakatifu yasemayo VIONGOZI WA DINI bali utakutana na maneno Mtumishi wa Bwana, Mwana wa Mungu, Mtume na Nabii. Si kwamba ilikosewa bali kuna sababu kuu ya kuwaita hivyo kiroho.. sasa basi, wale wote wajiitao viongozi wa dini ni waongoza dini za kidunia kwa maana ya watumwa wa shetani katika kukamilisha agenda ya uraghai.. Mtumishi wa Mungu hana maslahi katika kuogemea siasa kwani yeye mwenyewe kwa mjibu wa maandiko ni mwanasiasa tosha... penye nyeupe atakwambia kuwa hapo ni nyeupe na nyeusi kadhalika atakwambia kuwa hapo ni nyeusi... "..wasiyo wake Mungu Baba mtawatambua kwa Matendo na kauli zao..".
 
Sijaelewa pale tunaposema "Hili ni Chaguo la MUNGU" lakini ili chaguo hilo litimie inabidi sasa wanadamu watumie njia na mikakati ya siri, vitisho na ghiliba ili kuhakikisha chaguo hilo la MUNGU linatimia.
Jee ni kweli kuwa Mwenyezi MUNGU wa kweli anahitaji wanadamu tutumie nguvu, mikakati, mizengwe na hila kuwadhibiti wale wasiotaka chaguo la MUNGU litimie? Hawa wasiotaka Chaguo la Mungu wana nguvu kiasi gani kupingana na MUNGU hadi ahitaji tumsaidie kuwashughulikia?
Ni chaguo la Mungu kweli au tunatumia jina lake kwa manufaa ya kibinadamu?
Chakaza tafadhali sana utatuumiza mbavu wengine mbavu zetu zilishavunjikaga
Eti chaguo la Mungu linalohitaji jitihada MIZENGWE ya wanadamu kufanikiwa ! !
 
Mungu hutenda kupitia wanadamu. Hata Lowassa angechaguliwa na Mungu angetenda kupitia mizengwe ya binadamu. Tatizo ni kwamba hakuna binadamu aliye mkamilifu. Na kuongoza nchi kama yetu hii ya wapenda porojo, wavivu, wasiojituma, wakwepa kodi, mafisadi... siyo kazi rahisi kama unavyodhani. Hata kama tungekupa wewe leo hii ungegundua mapema sana kuwa bila mizengwe ya kibinadamu mambo hayaendi. Watawala wote wanalijua hili.
 
Sijaelewa pale tunaposema "Hili ni Chaguo la MUNGU" lakini ili chaguo hilo litimie inabidi sasa wanadamu watumie njia na mikakati ya siri, vitisho na ghiliba ili kuhakikisha chaguo hilo la MUNGU linatimia.
Jee ni kweli kuwa Mwenyezi MUNGU wa kweli anahitaji wanadamu tutumie nguvu, mikakati, mizengwe na hila kuwadhibiti wale wasiotaka chaguo la MUNGU litimie? Hawa wasiotaka Chaguo la Mungu wana nguvu kiasi gani kupingana na MUNGU hadi ahitaji tumsaidie kuwashughulikia?
Ni chaguo la Mungu kweli au tunatumia jina lake kwa manufaa ya kibinadamu?

Kwenye red; ni kina nani mnaosema "Hili ni Chaguo la Mungu"? Na ni nini mnachokiita "Chaguo la Mungu"?
 
Mungu hutenda kupitia wanadamu. Hata Lowassa angechaguliwa na Mungu angetenda kupitia mizengwe ya binadamu. Tatizo ni kwamba hakuna binadamu aliye mkamilifu. Na kuongoza nchi kama yetu hii ya wapenda porojo, wavivu, wasiojituma, wakwepa kodi, mafisadi... siyo kazi rahisi kama unavyodhani. Hata kama tungekupa wewe leo hii ungegundua mapema sana kuwa bila mizengwe ya kibinadamu mambo hayaendi. Watawala wote wanalijua hili.
Hhhhhhhh huyo itakuwa mungu wa Lumumba ananayetenda kwa mizengwe ya wanadamu
 
Ukisoma isaya 45..1 na kuendelea,Cyrus wa Persian empire..alichaguliwa na MUNGU..japo hakumjua..ili aruhusu ujenzi wa hekalu..alipigwa na Alexander the great..so unaweza chaguliwa kwa kusudi flani..basi.baadae usipokua makini,ukafeli..
 
Mungu hutenda kupitia wanadamu. Hata Lowassa angechaguliwa na Mungu angetenda kupitia mizengwe ya binadamu. Tatizo ni kwamba hakuna binadamu aliye mkamilifu. Na kuongoza nchi kama yetu hii ya wapenda porojo, wavivu, wasiojituma, wakwepa kodi, mafisadi... siyo kazi rahisi kama unavyodhani. Hata kama tungekupa wewe leo hii ungegundua mapema sana kuwa bila mizengwe ya kibinadamu mambo hayaendi. Watawala wote wanalijua hili.
mimi naunga mkono utendaji wa kazi kwa haki, ila siungi mkono kosa la mwingine abebe mzingo mwingine, (kama la wanafunzi) ambalo ni la tcu.
 
Mungu hutenda kupitia wanadamu. Hata Lowassa angechaguliwa na Mungu angetenda kupitia mizengwe ya binadamu. Tatizo ni kwamba hakuna binadamu aliye mkamilifu. Na kuongoza nchi kama yetu hii ya wapenda porojo, wavivu, wasiojituma, wakwepa kodi, mafisadi... siyo kazi rahisi kama unavyodhani. Hata kama tungekupa wewe leo hii ungegundua mapema sana kuwa bila mizengwe ya kibinadamu mambo hayaendi. Watawala wote wanalijua hili.
Mungu sio binadamu hata kama anaonekana na kutenda katika binadamu! Unatakiwa kujua mizengwe ni dhambi hivyo Mungu hahitaji kutumia dhambi ili kufanikisha jambo fulani. Uandishi wako ni kama waandishi wengine hata wa vitabu vya dini ambao falsafa ya uandishi wao imeathirika na mazingira wanayoishi. Mazingira machafu ya Tz (porojo, wavivu, ufisadi, wizi, n.k) yamekuathiri kwa kiwango cha juu hadi kufikiri hakuna jambo jema linaloweza kufanikisha bila mizengwe(dhambi).
 
Nionyeshe kokote kuliko na utawala kamilifu hapa duniani, utawala usio na dhambi, utawala usiodanganya raia ili kutawala. Nionyeshe hata sasa nitafunga virago na kuhamia huko hata iwe Mars!
 
Back
Top Bottom