Chagua mtu sio chama

Chagua mtu sio chama

mzee wa misele

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2015
Posts
366
Reaction score
46
najua saizi tunaelekea uchaguzi mkuu nawahasa watanzania mchague MTU sio chama kumbukeni kwamba MTU ndiye anaeleta maendeleo sio chama chagueni MTU mchapakazi na mpenda maendeleo na mwenye usubutu wa kutoa maamuzi magumu yenye kuleta maendeleo ya nchi asiyekuwa mbinafsi na mwenye upendo na watu wote bila kujali rika la watu, hali waliokuwa nayo watu , nawasilisha
 
Hatutaki kusikia neno ccm pamoja na mvumo wao, cc tunachagua chama chochote kilicho ndan ya ukawa, 2010 mlikuja na story iyo iyo chaguen mtu, hatutak kuckia ccm tena tumechoka
 
Mbona unangatangata maneno? Uchaguzi wa mwaka huu ni Lowasa au Magufuli na CHADEMA/UKAWA au CCM. Sasa unashauri nini?
 
Kama ni kuchagua mtu magufuli anafaa lakini ccm hapana
 
ni kweli hatutaki kusikia kitu ccm hata kama malaika angeshuka toka binguni eti agombee urais kupitia ccm kura hapati
 
Ccm wamebanwa kila kona wanejarbu kusema tuchague MTU na sio chama lakni baadae wamegindua magufli hafahamiki vjijini na watu wa vjijn wao uchagua chama wala sio MTU, kwa maana hiyo ccm wako njiapanda.
 
najua saizi tunaelekea uchaguzi mkuu nawahasa watanzania mchague MTU sio chama kumbukeni kwamba MTU ndiye anaeleta maendeleo sio chama chagueni MTU mchapakazi na mpenda maendeleo na mwenye usubutu wa kutoa maamuzi magumu yenye kuleta maendeleo ya nchi asiyekuwa mbinafsi na mwenye upendo na watu wote bila kujali rika la watu, hali waliokuwa nayo watu , nawasilisha

hakika watu wanachanganya mafile,hivi mtu anatokana na nn?,au ndiyo presha mbona bado dawa inakuja soon!!!,memory zinaanza kusoma ndivyo sivyo? sawa mkuu
 
Binafsi nimeisha fanya maamuzi, awe hata malaika maadam kasimamishwa na ccm sitampa KURA yangu. Uamuzi hu nimeisha ufanya and NO body will change me!
 
hatutaki kusikia neno ccm pamoja na mvumo wao, cc tunachagua chama chochote kilicho ndan ya ukawa, 2010 mlikuja na story iyo iyo chaguen mtu, hatutak kuckia ccm tena tumechoka

sisi hatutaki fisadi anayenunua watu na vyama vyao
 
Uloi nga mâché68;13790085 said:
pumbu zako
Matusi ya nini? Kama ukitukanwa wewe utakubali kweli! Watu humu wamemshupalia Mkapa kuwa ametukana, sasa wewe upo kundi gani. Subiri tarehe 1/9 tuone kama utarudia kutukana namna hii!
 
najua saizi tunaelekea uchaguzi mkuu nawahasa watanzania mchague MTU sio chama kumbukeni kwamba MTU ndiye anaeleta maendeleo sio chama chagueni MTU mchapakazi na mpenda maendeleo na mwenye usubutu wa kutoa maamuzi magumu yenye kuleta maendeleo ya nchi asiyekuwa mbinafsi na mwenye upendo na watu wote bila kujali rika la watu, hali waliokuwa nayo watu , nawasilisha
mzee wa misele, huyo mgombea ambaye hakutokana na chama ni yupi basi? Hebu jaribu kufafanua tafadhali kwani ninavyojua hakuna mgombea binafsi. Kwa kweli napata shida kuelewa ulitaka hasa kusema nini.
 
Last edited by a moderator:
mzee wa misele tupe maoni yako kwa maana hiyo unampendekeza nani?
 
Hiyo dhana ya kusema chagua mtu sio chama, ni dhana ya ujinga na upotoshaji mkubwa sana. Ngoja nifafanue kidogo.

1/Mpaka sasa hapa Tanzania hatuna sheria inayoruhusu mgombea binafsi, hivyo wagombea wote ni lazima watokane na vyama.

2/Kila Chama kina agenda yake ya kutawala, na huwa kinachagua mtu wa kugombea ambaye atakuwa mtiifu kwa chama chake na kutii agenda za chama hicho katika kutawala na sio vinginevyo.

3/Haitatokea hata mara moja mgombea awe juu ya chama anachokiwalisha. Mgombea ni bendera ya Chama wakati wa Uchaguzi. Mgombea ana akisi(Reflect) taswira ya Chama cha siasa, kwa mantiki hiyo, siku zote Chama kitahakikisha kinaleta mgombea mwenye taswira ya 'malaika' ili kuficha taswira yoyote mbaya ya Chama.
 
Mbona mgombea binafsi mlishamkataa kulikoni tena ? Au ndio mnatafuta gea yakutokea ?
 
Thubutu! Mgombea yeyote atakayeshinda atatekeleza ilani ya chama chake na sio mipango yake binafsi. Kwaiyo unapoona umaskini wa nchi hii ni sera za ccm wala co kosa la mtu mmoja mmoja.
 
Back
Top Bottom