Chagua gari Sweetie...

Chagua gari Sweetie...

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,413
Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja
aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.


MZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .


BINTI: Mi naitaka hii


MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe.
Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard


MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki,
gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee


MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako... Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.


MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.


MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.
Cc Nyani Ngabu The Boss Preta NGULI
 
Last edited by a moderator:
Imekaa njema. Mzee kapata alichotaka, binti imekula kwake.
 
Mzee siyo mstaarabu, anawachezea wasichana wa watu, ipo siku watamwagia tindikali.
 
Uwiiii!!!
Bint alijituma na nusu Akijua ameshamiliki Verossa!!!!
 
Mjini akili nguvu kijijini...
Safi sana mzee
 
Huyu Mzee siku nae wadada wakimuingiza kwenye anga zao ndipo atakapojua alichokuwa akikifanya ni ujinga na ni hatari!!
 
Hahahahaah,,,,,mzee huyo ni noma, ila ipo siku naye ataingizwa mjini na hao hao.
 
Back
Top Bottom