Chagua chumba kuokoa Maisha!

Chagua chumba kuokoa Maisha!

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
7,195
Reaction score
21,254
Swali: Kuna vyumba vitatu ambavyo mfungwa analazimika kuchagua kimoja ili kuokoa maisha yake:

1-Chumba cha kwanza: Kimejaa moto mkali unaoungua kila kitu.
2-Chumba cha pili: Kimejaa wauaji wa kukodiwa wenye silaha nzito.
3-Chumba cha tatu: Kimejaa simba ambao hawajala chochote kwa muda wa miaka mitatu.

Tuchangamshe asubuhi hii, mwenye jibu sahihi atapata zawadi.
 
Swali: Kaka na mdogo wake wa kike wana jumla ya umri wa miaka 110. Kaka amemzidi mdogo wake umri wa miaka 100.

Mdogo wa kike ana umri wa miaka mingapi?


(Kamtego: Ukisema ana miaka 10, utakuwa umefeli!)
 
Swali: Racket ya tenisi na mpira wake vina gharama ya jumla ya Dola 1.10 (Tsh 3,100 hivi). Racket inazidi bei ya mpira kwa Dola 1.00.

Je, mpira pekee unagharimu kiasi gani?
 
Swali: Racket ya tenisi na mpira wake vina gharama ya jumla ya Dola 1.10 (Tsh 3,100 hivi). Racket inazidi bei ya mpira kwa Dola 1.00.

Je, mpira pekee unagharimu kiasi gani?
 
Swali: Kama paka 5 wanaweza kukamata panya 5 ndani ya dakika 5...

Je, itachukua paka wangapi kukamata panya 100 ndani ya dakika 100?
 
Swali: Kuna aina fulani ya bakteria ambao wanazaliana kwa mtindo wa kujigawa mara mbili (double) kila baada ya dakika 1.

Ukiweka bakteria mmoja kwenye chupa, chupa hiyo inajaa nzima ndani ya dakika 60 (saa moja).

Je, chupa hiyo ilikuwa nusu (1/2) itakapofika dakika ya ngapi?
 
Back
Top Bottom