Chagua CHADEMA 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chagua CHADEMA 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jafar, Aug 5, 2010.

 1. J

  Jafar JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Usipoteze muda wako umeshaumia kiasi cha kutosha, kataa kuendelea kuumia tena. Yote haya yatawezekana kwa kupiga kura yako na kuchagua CHADEMA.

  Kumbuka Dr. Slaa ni silaha yako ya kupambana na kuleta maendeleo Tanzania. Nchi nyingi zilizokataa siasa za mazoea sasa ziko mbali mfano Zambia, Botswana, Ghana, Malawi n.k. kwa upande mwingine nchi zilizokumbatia siasa za mazoea angalia zilipo mfano Tanzania, Zimbabwe n.k.

  Kataa watu wanaokubali kupokea vyandarua bure kutoka kwa wakora kwa kisingizio cha malaria na kubadirishana na dhahabu yetu.

  Changua CHADEMA 2010
   
 2. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Badili hiyo sahihi yako ili unaowahamasisha waone uko makini na dhamira thabiti. Acha kuwa vuguvugu!
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Naongezea hapo! Kataa watu wanaosahau kuwa tuko karne ya ishirini na moja hata hawakumbuki kuiweka nchi kwenye ramani ya kisayansi na Technologia, kataa watu wanaopenda kuwalaghai watu kwa mipesa haramu wakati wa uchaguzi, kataa watu waioona kero kwa dada zetu kupigwa mimba kila kukicha, kataa watu wanaosahau kuwa 70% ya watz ni masikini wa kutupwa, kataa watu hawa wasiokuwa na vipaumbele kwenye masuala muhimu ya kitaifa kama ( Elimu, Afya, mazingira, Tafiti za kitaalamu, Ubunifu wa kuzalisha mali nk)

  Nachosema watz wenzangu kuwa tupende tusipende mambo mazuri hayaji kirahisi, we need some people to sucrifice their time, families more over their lives. Ukiangalia nchi kama China hawakufika hapo kwa ndoto za kimweli wala kwa kupiga domo, ni kwa vitendo tena serious working.

  SIku moja nikiwa jijini seoul, nikapanda subway nilikuta kuna siti za wazee ambazo ni maalumu kwa ajili yao ikiwa ni heshima kwao kwa kujitolea kuijenga nchi wakati wa miaka ya 1970's. So its the matter of leadership and human resource management. Vibaka kibao hawana kazi, watu kibao wanalia njaa lakini maji kibao sehemu kibao. We can take them and teach them how to do the work. Hao hao watajenga nyumba nzuri, watakuwa wanalima na kila kitu kitakuwepo kwenye makambi yao kama ni soka watacheza, wataangalia EPL na vitu kibao.

  CHAGUA CHADEMA, tuanze mabadiliko. Human Rights ziko sana lakini bila kuvunjwa, hatufiki popote ndugu zangu watz, saizi ni mwendo wa kijeshi jeshi ndo tutaheshimiana.
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Leteni hoja madhubuti ya kwanini watanzania tumchague Dr. Slaa na sio kusema tu tunahitaji mabadiliko (change for its own sake haina maana).

  Watanzania wanahitaji kupima viongozi on the basis of their merits and ability to deliver positive and needed results to the public na sio kuchagua chama au mtu for their own sake!!

  Binafsi nitachagua diwani, mbunge na Rais madhubuti, mwenye vision na anayekerwa na matatizo waliyonayo watanzania na mwenye dawa ya kutatua matatizo hayo kwa kushirikiana na watanzania wengine wazalendo na nchi marafiki bila kujali yyuko chama gani.
   
 5. k

  karisti Member

  #5
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee umesema vyema. Safari hii hebu tubadilike kidogo! CHANGE WE NEED!
  Tunataka watu wenye uchungu na taifa hili, sio blaa blaa tu na maneno matamu kama hadithi halafu
  no action. We need a serious person who will Change the nation from NO to Yes, from poverty to prosperity
  from ubadhirifu wa mali za uma to uadilifu na uzalendo.

  Thats why we need Dr. Slaa to Lead us! Tell your friends, and shout to everybody that
  this term is for SLAAAAAAAAAAAAAA! A WEAPON FOR CHANGE TO PROSPERITY!
   
 6. J

  Jafar JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama unafuatilia siasa neno "mjomba" hapo ni JK. Na dhamira yangu iko wazi kwenye saini yangu. Saini inawaasa wale wapumbavu wachache wachukue maamuzi binafsi.
   
 7. J

  Jafar JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yaani mpaka leo wewe hujapima ukiona mwenyewe basi nyie ndio wale wale. Unasubiri kanga na fulana ili uwambiwe umpigie nani. Pima mwenyewe katika maisha yako ya kila siku halafu amua - usitegemee data za kupikwa zikuamulie mustakabali wa maisha yako. Chagua CHADEMA.
   
 8. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  na mimi naongezea hapo..kataa Serikali ya kidhalimu inayowakumbatia mafisadi wanaofilisi Nchi yetu na kuwaacha Watanzania wengi wakiwa kwenye umaskini uliokithiri
   
 9. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kataa kupokea rushwa za kofia ili uweze kutoa maamuzi sahihi,fuatilia kampeni na usikilize sera na sio sura na kutabasamu kwingi kulikopitiliza,kuwa jasiri kama kamanda vitani. chagua chadema.
   
 10. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "Mjomba najua utapita, watanzania bado wapo usingizini, safari hii kura yangu hutaipata, japo haiwezi kukuzuia lakini nafsi yangu itakuwa na amani kwamba sikushiriki kukusimika"

  Hoja ya Omutwale kama nimemuelewa vizuri ni kwamba unahamasisha watu kuchagua chadema wakati signature yako inaonyesha kuwa kura yako haitaipata mjomba lakini haitamzuia kurudi madarakani, hii inawavunja moyo unaowahamasisha, naomba ibadili ndugu
   
 11. J

  Jafar JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wengi wape
   
 12. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Naongezea,
  Chagua CHADEMA tuondokane na umwenzetu na kulindana kuliko tufikisha hapa
  tulipo!
  Chagua CHADEMA tuondokane na serikali ya kifisadi
  Chagua CHADEMA tuondokane na serikali ya kibabe inayo tisha wafanyakazi wake na
  kuwambia waajiri wwafukuze wakidai haki zao
  Chagua CHADEMA tuondokane na serikali ya kishikaji, akiharibu hapa anahamishiwa
  pale nako akaharibu
  Chagua CHADEMA tumsimike raisi mwenye kuliita koleo kwa jina lake siyo kijiko
  kikubwa (nawajua wezi, wauza unga nawapa muda)
  Chagua CHADEMA tuondokane na serikali inayoona watoto wetu kubakwa na kupewa
  mimba ni kihehele chao
  Chagua CHADEMA tuondokane na serikali inayo husudu 'vigagula' (kwamba atye pinga
  atakufa !!!!!)
  Chagua CHADEMA tusimike raisi mwenye uthubutu
  Chagua CHADEMA tupate kiongozi mwenye kujenga hoja
  Chagua CHADEMA tupate kiongozi anaye jua shida/iumasikini wa watanzania na
  chanzo chake
  Chagua CHADEMA tupate kiongozi anaye jua kujenga hoja na si .... hata pasipo stahili
  Chagua CHADEMA tupate vongozi ........
  Chagua CHADEMA tupate viongozi ........ waweza endelea kwani sababu ni nyiiiiingi
  mno za 'why CHADEMA NOW'
   
Loading...