CHADEMA yazidi kuvuna wanachama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yazidi kuvuna wanachama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by QUALITY, May 28, 2012.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ZAIDI ya wanachama 1000 kutoka vyama mbalimbali wengi wao wakiwamo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamevihama vyama vyao na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
  Mbali na wanachama wa CCM, wengine waliovihama vyama vyao ni kutoka NCCR Mageuzi, TLP na CUF katika mkoa wa Kagera, Mwanza na Mororogo.
  Mkoani Kagera katika wilaya ya Ngara, CHADEMA imezoa wanachama 862 kutoka CCM, NCCR-Mageuzi (104), CUF (83) na TLP (25) katika mwendelezo wa operesheni ya Vua Gamba vaa Gwanda.
  Akizungumza na waandishi wa habari kutoka Ngara jana, mjumbe wa Kamati tendaji ya wilaya ya Ngara ya chama hicho, Simon Malanilo, alisema wanachama hao wapya wamewapata kutoka katika kata sita walizofanya mikutano ya hadhara.
  Alizitaja kata hizo kuwa ni pamoja na Kabanga, Mugoma, Murusagamba, Kasulo, Mrukurazo na Rulenge.
  Malanilo alisema kamati ya utendaji ya Ngara imetumia nafasi ya kuwepo kwa kikao cha wajumbe wa mkutano wa mashauriano wa mkoa wa Kagera uliofanyika Mei 9-10.

  Kutoka mkoani Mwanza, wanachama 97 wa CCM na CUF wilayani Magu, wamerudisha kadi zao na kujiunga na CHADEMA.
  Miongoni mwa viongozi wa CUF waliokihama chama hicho ni katibu wa chama hicho wilaya na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Dominic Bubeshi, ambaye alitangaza juzi kujiunga na chama hicho katika mkutano ulioongozwa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, uliofanyika katika viwanja vya Sabasaba wilayani humo.
  Kada mwingine wa CCM aliyejiunga na CHADEMA ambaye pia aliwahi kugombea udiwani katika kura za maoni mwaka 2010 na kutoa upinzani mkali ni Samuel Moma.
  Nako wilayani Mvomero, Morogoro, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, katibu na wanachama 40 wa CCM katika kijiji cha Kigugu, wilayani Mvomero, Morogoro, wamekihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA.
  Waliokihama chama hicho juzi ni Thomas Maseke (Mwenyekiti), Carlos Lukanga (Katibu wa Tawi la CCM Mlaguzi) na wanachama 40 na kukabidhi kadi za CCM kwa katibu wa CHADEMA wilayani Mvomero, Dismas Ngeresha.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu wa CHADEMA wilayani Mvomero, Ngeresha, alithibitisha kuwapokea wanachama na viongozi hao katika viwanja vya Kijiweni Kigugu wakati wa kampeni ya Vua Gamba vaa Gwanda.
  Alisema Maseke na Carlos kabla ya kujiunga CHADEMA, waliandika barua za kujiuzulu wakiukana uongozi huo ndani ya CCM.
  Kwa upande wake, Maseke alikiri kuihama CCM na kudai anamtumia salamu aliyekuwa diwani wake, Nicholous Waziri, kutafakari, ili maumivu yamtoke.
  Taarifa hii imeandaliwa na Sitta Tuma (Mwanza), Bryceson Mathias (Mvomero) na Mwandishi Wetu (Ngara)

  Source Tanzania Daima ya Mei 23, 2012.

  Nyongeza:
  Mikutano hiyo iliyofanywa kwa stail yake ya timu ya wajumbe kugawanyika katika kata sita na kufanya mikutano yote hiyo kwa mara moja, iliandaliwa na kuratibiwa na kamati tendaji ya wilaya hiyo. Wajumbe walitoka katika majimbo yote kumi ya mkoa wa Kagera. Jioni yake, wajumbe wote walikuwa wamerejea makao makuu ya wilaya ya Ngara ambako nako ulipigwa mkutano mkubwa wa hadhara na kuhutubiwa na wanyeviti wa majimbo yote na wengine toka mkoa wa Mwanza.

  Quality
   
 2. W

  Wangama guy Senior Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  M4C!! Yaani ndo kwanza kumekucha, Magamba wamebanwa pabaya!
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Dar wakiamka Tanzania nzima itakuwa imekombolewa!
  Hakuna watu wagumu na wazito kama waswahili!
   
 4. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 180
  kitaeleweka tu, namhurumia sana nape na jk, wanatia huruma sana! Cdm waachieni hata wanachama wachache msizoe wote jamani!
   
Loading...