CHADEMA yazidi kusambaratisha CCM Ukonga.....

CHADEMA yazidi kusambaratisha CCM Ukonga.....

Uchaguzi ukikaribia matawi yanafunguliwa kwa wingi! Hongera sana, najivunia Kuwa mwanachama hai wa CDM, lakini tatizo baada ya uchaguzi ofisi zinafungungwa na ni nyingi tu hasa mikoani, ukiuliza hakuna pesa ya kuendeshea, Ruzuku hazifiki huko, waambieni wavumilie kidogo balance tuliyokuwa nayo ya ml. 80 tumeagiza card China.

Body without head
CDM kila siku utasikia uchaguzi mi sielewi hata kidogo maana Kama chama lazima kiwe na calendar ya uchaguzi! Yaani nyie CDM mnaendeshwa kwa matukio!

CDM wana jipambanua Kama chama cha demokrasia kumbe wapi! Kuna mambo mengi inabidi mjifunze toka kwa CCM!

Ofisi za CDM ni za muda tu yaani za matukio tu! Yaani ukikaa chini ukatafakari hupati majibu kwa mfano Iramba hawana Mwenyekiti, hata viongozi wa Jumuiya hawana wanataka kumng'oa Mwigulu kwa nguvu toka DSM? Yaani akili zao wanazijua wenyewe! 2015 hamtaamini kitakachotokea tuombe uzima!
 
CDM hamuwezi kuishinda CCM kwa kukaa mitandaoni! CDM Kama chama kina mapungufu mengi sana!

Ofisi zenu Hazina uongozi thabiti, kuanzia ngapi za mikoa, wilaya, Kata hadi matawi! Yaani ni ofisi jina tu lakini Hazina watu! Nyingi zinafunguliwa wakati wa matukio ukitaka kuamini tembelea ofisi za Mkoa wa Singida zinatia huruma!

Pia viongozi wenu wengi hawana program za kujenga chama hadi viongozi wa kitaifa wanapokuja utawakuta busy chopa ikipaa tu ofisi zote zinafungwa!

Jumuiya zenu zipo hoi taabani kwa mfano Singida sijasikia hata ck Moja Jumuiya ndani ya CDM ukifanya mikutano kitu ambacho hakipo!

Hakuna uongozi kwenye matawi wala shina yaani wao M4C ndio chama hivi kwa mipango hii mkiangukia pua mtamlaumu mtu? Yangu macho endeleeni kusutana mitandaoni mtavuna mnachokipanda!
 
Karibuni tangawizi vijana wenzangu nilipoona tu source Tanzania Mbowe nikapitia kijiweni kupata kahawa na tangawizi!
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ukonga kimezidi kujiimarisha kwa kuzindua matawi ya msingi katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, mkakati unaokwenda sambamba na uchaguzi wa viongozi.

Pia chama hicho kimekuwa kikifanya mikutano ya hadhara na kupokea maelfu ya wanachama wapya wengi wao wakitokea CCM.

Uzinduzi huo ambao unafanyika chini ya uratibu wa Katibu wa Jimbo hilo, Juma Mwipopo, lengo ni kukileta chama karibu na wananchi.

Miongoni mwa matawi ya msingi yaliyozinduliwa hivi karibuni ni Tawi la Msingi la Mnarani, Mtaa wa Gurukakwalala na kufanyika pia uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo uliosimamiwa na Katibu wa Jimbo, Mwipopo.

Viongozi waliochaguliwa kuongoza tawi hilo ni pamoja na Bwawa Moses (Mwenyekiti) na Esther Moses (Katibu). Mwakilishi wa Vijana alichaguliwa Salum Mayambe, mwakilishi wa kina mama ni Georgina Jackson na mwakilishi wa wazee ni Deogratius Joram. Vilevile alichaguliwa balozi wa nyumba kumi, Ipyana Noah.

Akitoa maelezo mafupi kabla ya uchaguzi wa viongozi hao, Mwipopo aliwataka wanachama na wapenzi wa CHADEMA kujitokeza hadharani ili chama kiwatambue kuwa wapo, wanakiunga mkono na wanakitumikia kwa uadilifu.

Aidha, Mwipopo alibainisha kuwa lengo la kufungua matawi ya msingi ni kuwatambua wanachama na kuwa na mtandao wa viongozi kuanzia ngazi ya chini na kuwahimiza viongozi waliochaguliwa kutimiza vema wajibu wao kwa kuwatumikia wananchi bila upendeleo.

Akizungumzia kuhusu kukithiri kwa rushwa katika jamii, Mwipopo aliwaonya waliohudhuria katika hafla hiyo kuwachagua viongozi kulingana na sifa zao na si kwa vigezo vya rushwa, urafiki na kufahamiana ili kujitofautisha na vyama vingine vya siasa.

Jimbo la Ukonga kwa sasa ni kati ya majimbo ambayo CHADEMA ina nguvu kubwa na kujirahisishia ushindi katika kiti cha ubunge na viti vya udiwani katika chaguzi zijazo.

Source:Tanzania Daima
Ni wakati muafaka, Bomoa CCM Kabisa, kila sehemu.
 
Back
Top Bottom