CHADEMA yazidi kumeguka...!

CHADEMA yazidi kumeguka...!

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Hii ni zaidi ya kulala na Bundi.

CHADEMA kimepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho Kata ya Mkuza Abdallah Maja kuhama chama hicho na kujiunga na CCM.

Maja pamoja na wanachama wengine wa CHADEMA akiwemo Yusuph Komba walirudisha kadi za Chama hciho kwenye mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala uliofanyika Mkuza Kibondeni wilaya ya kibaha wakati wa ziara yake inayoendelea kwenye mji huo kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama.

Akizungumza mara baada ya kuhamia CCM, Maja alisema kuwa kule Chadema hakuna lolote kwani siasa zake ni za kibabaishaji. "kule hakuna lolote zaidi ya ujanja ambao hautaweza kuleta maendeleo kwa wananchi. Mimi nilipata matatizo lakini walishindwa kunisaidia hadi nikasaidiwa na CCM, nimeona kuwa chama cha ukweli ni Cha Mapinduzi pekee" Alisema Maja.

Source: Majira jumatatu septemba 30, 2013. Ukurasa wa 10:

Baada ya Habari hiyo ya kusisimua napenda kumpa pole ya dhati kabisa Mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw. Freeman Aikaeli Mbowe kwa kufiwa na Ndugu yake Grace Aikaeli Mbowe, ambaye amefariki katika ajali ya Gari iliyotokea eneo la Kabuku Jana.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana Lihimidiwe. Pole mara mbili Mheshimiwa.
 
haishangazi watu wenye akili fupi kukimblia ccm! lakini pia njaa pamoja na ufupi wa akili waliyo jengewa na hiki chama cha kifisadi ndiyo kina fanya wahangaike wali wasijue wanachofanya
 
Hilo ni kama tone tu kati ya wale waliokwisha jitambua!! Kuna kipindi cha mwaka 2011 na 2012 ilikuwa kama mvua ya wanachama kujiunga na CDM!! CDM hatuna hofu yoyote na hao mnaowanunua kwa gharama kubwa!! Tegemeo la CDM ni kuandikisha wapiga kura hasa kwa vijana wengi ndo utaona moto moto moto!!
 
Hii ni zaidi ya kulala na Bundi.
Baada ya Habari hiyo ya kusisimua napenda kumpa pole ya dhati kabisa Mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw. Freeman Aikaeli Mbowe kwa kufiwa na Ndugu yake Grace Aikaeli Mbowe, ambaye amefariki katika ajali ya Gari iliyotokea eneo la Kabuku Jana.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana Lihimidiwe. Pole mara mbili Mheshimiwa.

Hicho kifo ni majibu ya Mungu kwa CCM Bwana alitoa hakutwaa, CCM ndiyo iliyotwaa. Sasa tekelezeni Plan B.

Unaimiss sana Chadema? Kama ulikwenda kujiuza CHADEMA wameshakufukuza. Kwa wewe, Mwigulu Nchemba Atosha lala naye muda wote tuache tulale na bundi wetu.
 
ninauhakika watu kibao watakula sana fedha ya kifisadi lakini kamwe hawatatoa kula kwa wafilisi nchi! na watu wengine hujifanya kujiunga na chama cha kifisadi ili mambo yao yaende poa lakini wala huko hawako, na ukweli wa jambo hil utaonekana mapema sana, na kipindi hiki uchakachuaji wa matokeo utakuwa mgumu sana...maana tumechoka kuchekea nyani
 
Safari inaendelea watabomoka sana mwaka huu mpaka tufike tuendako atabaki mtei,slaa na mbowe kwenye chama siyo vinginevyo.
 
Hii ni zaidi ya kulala na Bundi.

CHADEMA kimepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho Kata ya Mkuza Abdallah Maja kuhama chama hicho na kujiunga na CCM.

Maja pamoja na wanachama wengine wa CHADEMA akiwemo Yusuph Komba walirudisha kadi za Chama hciho kwenye mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala uliofanyika Mkuza Kibondeni wilaya ya kibaha wakati wa ziara yake inayoendelea kwenye mji huo kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama.

Akizungumza mara baada ya kuhamia CCM, Maja alisema kuwa kule Chadema hakuna lolote kwani siasa zake ni za kibabaishaji. "kule hakuna lolote zaidi ya ujanja ambao hautaweza kuleta maendeleo kwa wananchi. Mimi nilipata matatizo lakini walishindwa kunisaidia hadi nikasaidiwa na CCM, nimeona kuwa chama cha ukweli ni Cha Mapinduzi pekee" Alisema Maja.

Source: Majira jumatatu septemba 30, 2013. Ukurasa wa 10:

Baada ya Habari hiyo ya kusisimua napenda kumpa pole ya dhati kabisa Mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw. Freeman Aikaeli Mbowe kwa kufiwa na Ndugu yake Grace Aikaeli Mbowe, ambaye amefariki katika ajali ya Gari iliyotokea eneo la Kabuku Jana.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana Lihimidiwe. Pole mara mbili Mheshimiwa.

Mnh...!
 
ninauhakika watu kibao watakula sana fedha ya kifisadi lakini kamwe hawatatoa kula kwa wafilisi nchi! na watu wengine hujifanya kujiunga na chama cha kifisadi ili mambo yao yaende poa lakini wala huko hawako, na ukweli wa jambo hil utaonekana mapema sana, na kipindi hiki uchakachuaji wa matokeo utakuwa mgumu sana...maana tumechoka kuchekea nyani
Mbona watu wengi sana wamekula fedha za madawa kule chadema lakini wamepuuza wakarudi zao kwenye vyama vyao vya asili.
 
CHADEMA ilishameguka siku nyingi. kinachoendela sasa ni kuporomoka kama yanavyoporomokaga maghorofa ya pale Dar. si Katibu Mkuu alisema kuwa CHADEMA bado hakijawa imara!
 
... we July huyo jamaa ni mchumia tumbo kama wewe, angalia kauli yake eti "nilipata matatizo wakashindwa kunisaidia mpaka nikasaidiwa na ccm" unategemea mtu kama huyu atakaa chadema..!!?? sisi tunasaidia chama sio chama kugawa misaada, kwani imekuwa ccm ? yaani huyu asingetoka mwenyewe tungemtimua kama tulivyokufanya wewe...

...na kwa taarifa tu chadema tumeanza kuingia kwenye mikutano ya chama kwa kulipia kiingilio mlangoni,si chini ya buku tano kila mtu, igeni ccm kama mtapata mjumbe hata mmoja...
 
Hilo ni kama tone tu kati ya wale waliokwisha jitambua!! Kuna kipindi cha mwaka 2011 na 2012 ilikuwa kama mvua ya wanachama kujiunga na CDM!! CDM hatuna hofu yoyote na hao mnaowanunua kwa gharama kubwa!! Tegemeo la CDM ni kuandikisha wapiga kura hasa kwa vijana wengi ndo utaona moto moto moto!!
Haba na hujaza kibaba na polepole ndiyo mwendo.
 
Mbona watu wengi sana wamekula fedha za madawa kule chadema lakini wamepuuza wakarudi zao kwenye vyama vyao vya asili.
nimekuelewa mkuu, maana mi nabisha kwa uzalendo wangu alkin wewe uanauhakika wa buku saba, ushindi wa kwako!
 
Juliana Shonza what is your problem?kufukuzwa kwako CHADEMA ni kutokana na usaliti wako,siyo kweli CHADEMA hamna lolote, lolote lipo mfano
1.CHADEMA imefanikisha General tyre Arusha haikuuzwa kwa maumvi.
2.CHADEMA imerudisha nizamu za uchangiaji wabunge zamani iliwakuwa wanaanza na kuwashukuru wake zao , sasa waziri au mbunge anaenda moja kwa moja kwenye point, unataka CHADEMA ikufanyie nini ndo uone ina lolote, utasubiri sana wewe mwanamke.
 
Hivi Juliana, hicho kitengo cha kuriport habari za wanaohama CDM ndo umepewa wewe?
Hao mbona ndo wameanza tu, wote wliotumwa na MAGAMBA watatoka sana - hasa tutakapokuwa tunazidi kukaribia uchaguzi. CHADEMA kinatakiwa kipewe pongezi na sio pole pale ambapo virusi vinatoka mwilini. Hukuona tulivyoshangilia mlipofukuzwa na Mwampamba?
 
Tunaendelea kushuhudia vifo vya watu wazima kisiasa watapotea wote na aibu itabaki kwa wale waliokuwa nyuma yao.
 
Back
Top Bottom