CHADEMA yaweweseka...

CHADEMA yaweweseka...

watakuja kwa njia moja watatawanyika kwa njia saba,hao ni sisiemu chadema haikamatiki, wajanja wote waliojitambus wanaelewa mambo yanavosonga,hakuna kurudi nyuma haki kieleweke
 
Magazeti mengine utafikiri yanaandikwa na waandishi waliobwia unga kabla hawajashika kalamu. Kichwa cha habari hakina uhusiano kabisa na yaliyomo kwenye habari. Makanjanja.
 
Mimi nikiwaambia chdm imejaa waropokaji mnabisha, siku zote ukishindwa kufuata taratibu utaishia kulalama tu. wenzenu wanafanya maandamano ya kistaarabu, ninyi mnasababisha maafa tukiangalia arusha, singida na sasa morogoro, tunapata picha mbaya kuhusu maandamano ya cdm, na hivyo kwa polisi kuchukua tahadhari kwa wauaji ni sahihi kabisa. haya tuangalie mambo ya katiba na sensa hivi kama mtu unaakili za kutosha unaweza kufananisha na mikutano ya mvt for Chagaland>? Na iweje nyie muwe mnasababisha maafa halafu mumpe raisi kazi ya kuunda mitume isiyokuwa na tija,? haya ndo mapungufu ninayoyaona kwa wanachadema they think too little.
AAAAAAAAAAh! kumbe makuku!....
 
Mimi nikiwaambia chdm imejaa waropokaji mnabisha, siku zote ukishindwa kufuata taratibu utaishia kulalama tu. wenzenu wanafanya maandamano ya kistaarabu, ninyi mnasababisha maafa tukiangalia arusha, singida na sasa morogoro, tunapata picha mbaya kuhusu maandamano ya cdm, na hivyo kwa polisi kuchukua tahadhari kwa wauaji ni sahihi kabisa. haya tuangalie mambo ya katiba na sensa hivi kama mtu unaakili za kutosha unaweza kufananisha na mikutano ya mvt for Chagaland>? Na iweje nyie muwe mnasababisha maafa halafu mumpe raisi kazi ya kuunda mitume isiyokuwa na tija,? haya ndo mapungufu ninayoyaona kwa wanachadema they think too little.
your analysis is just too shallow! certainly you need to go to class again to know the truth.with all this light some people are still in the dark.
 
Wana UAMSHO rudi darasani,vinginevyo utatumiwa saana na CCMizi,hujajua tu kama ushatumiwa,UAMSHO wote hamtakiwi kwa kuwa kwa sasa hamna kazi ya kuwafanyia?,we vuta subira mtatakiwa tena senso ikiisha baada ya kuwa mmeorodheshwa kwa lazima mbali na TANGAZO lenu kuwa msilm yeyote atakae he,,sa,,bi,,w.a ni ''KHAFIRI'' Ww vp? siku zinakwisha ushachukua ukhafiri wako?,
USHAURI:Achaneni na chama cha mabwepande,PANDE ndo ficho lao kunasiku watawaficha huko viongozi wenu bila huruma,hawana urafiki hao zaidi ya kuwatumia na kuwabwaga sasa mmebwagwa cha ajabu mtarudiana tena.
Hakuna ulichoongea hapa zaidi ya kuingiza jazba na itikadi, Pole sana.
 
Acha kutuonyesha upuuzi wako wewe na uwezo wako finyu wa kufikiri. njaa zako unazoziendekeza zitakuua kabla ya muda wako!!!!!!!!
unataka utudanganye kwamba jeshi la polisi linaloua raia wa tanzania wasio na hatia ni wafuasi wa chadema!!!!!una maana kwamba CHADEMA ndio wanatoa amri kwa polisi kuua raia?????!!!!!!!!useless propaganda!!!!shame on you!!!
Nyie ndo mnaficha uovu wenu kwa kusingizia polisi, eti damu za watu ndo ziwafanye muingie ikulu, hakyanani kalumanzila atawavua hadi nguo za ndani lkn kwa umwagaji damu wenu huu mtaishia kumove for chagaland tu.
 
Akili zako finyu ndo zinakufanya uandike uliyoandika hivi katika mauaji yote ya wana CDM yanayotokea nchini yanasababishwa na CDM fikiria kabla ya kunena Polisi na CCM ndo chanzo cha vifo hivyo hakuna maandamano yaliyofanyika katika nchi hii yakawa na vurugu ila utokea vurugu pale tu polisi wanapotumwa na mabwana zako kuzuia maandamano hayo. na unaposema M4C ni movement 4 chagaland hapo ndugu yangu ni kauli ya kukata tamaa na kimbunga kinachowajia na mwaka huu mtakoma.
Kwakweli Chagaland mmeishiwa na sera yaani unamaanisha kimbunga cha mauaji ya watu wasiokuwa na hatia ili muisingizie polisi>.? ndo maana watu wenye busara zao ndani ya chama chenu hawatokei kwenye maandamano yenu halafu mnasema eti wanawasaliti kumbe mipango yenu michafu ya kutaka kuua watu wasio na hatia ili mujipatie umaarufu na kuisingizia polisi kwa kuchafua serikali yetu makini ya C......................C..........................M. Poleeeeeeeeeeeeni saaaaaaaaaaanA
 
Dk Slaa amvutia pumzi Samuel Sitta Send to a friend Thursday, 30 August 2012 21:01 [Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa] Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema kauli iliyotolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ni nzito, hivyo anajipanga kuijibu. Dk Slaa aliliambia gazeti hili jana kuwa asingependa kuzungumzia kauli hiyo sasa kwa kuwa yuko ziarani vijijini, lakini ataitolea tamko wakati mwafaka ukifika.Habari ambazo baadaye gazeti hili lilizitapa zinasema kuwa Dk Slaa huenda akamjibu Sitta leo, atakapokutana na waandishi wa habari mjini Iringa. Dk Slaa mwenyewe jana jioni alithibitisha kwamba atakutana na waandishi wa habari leo mjini Iringa, lakini hakuwa tayari kueleza kama atazungumzia kauli ya Sitta au la. Kauli ya Dk Slaa imekuja baada ya gazeti hili kumtaka azungumzie kauli ya Sitta kuwa muda wa Chadema kutawala nchi bado, kwa kuwa chama hicho hakina viongozi makini wa kufanya kazi za Serikali. Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana Dk Slaa alisema,"Nimemsikia, lakini sijamwelewa. Naomba nipate muda wa kusoma vizuri alichosema, halafu nitamjibu tu." Aliendelea:"Mimi sasa nipo huku Mufindi, sina mawasiliano yoyote ya msingi, naomba nipate muda zaidi wa kujiridhisha maneno yake kabla sijamjibu, nikiwa tayari nitawajulisha (waandishi).” Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza na gazeti hili jana alisema mkutano wa Dk Slaa na waandishi wa habari utalenga kueleza jinsi Chadema kinavyoendesha Operesheni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), baada ya kuzuiwa kwa mikutano yake ya hadhara. “Kwenye mkutano na wanahabari, mambo mengi yanaweza kutokea. Kwa hiyo siwezi kukujibu moja kwa moja kama hilo unaloulizia (kauli ya Sitta) nalo litajibiwa au la,”alisema Makene. Sitta alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM wa wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera juzi, alisema kuna upungufu mwingi katika safu ya uongozi ya Chadema, kutokana na kutokuwa na watu wenye uzoefu wa kufanya kazi za Serikali, badala yake wana baadhi ya watu wenye uzoefu wa kuongoza kumbi za muziki. Sitta alisema ukimwondoa Dk Slaa, hakuna kiongozi mwingine anayeweza kufanya kazi ya kukiongoza na kukifanya chama hicho kikubalike kwa umma. “Hawa jamaa hawana hazina ya viongozi kama tulionayo CCM, ambapo tunaweza kusimamisha wagombea 20 wa urais wenye sifa zinazofanana tofauti na wao wanae Dk Slaa tu ambaye inasemekana aliukimbia upadri,” alisema Siita na kuongeza: “Wote hapa mnasikiaga kwamba Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe ni mjuzi wa disko za usiku, sasa huwezi kulinganisha na CCM hata akitoka mtu mmoja chama chetu hakiwezi kuyumba.” Kuhusu M4C Katika hatua nyingine, Dk Slaa alizungumzia Operesheni inayojulikana kama M4C akisema Chadema imewabwaga polisi, kutokana na chama hicho sasa kubuni mbinu nyingine ya kujiendesha. "Tuko huko Mufindi tunajenga chama, vikao kila wakati," alisema Dk Slaa alipoulizwa yuko wapi na anafanya nini. Dk Slaa alisema CCM na Serikali yake, itajuta kuzuia mikutano ya hadhara ya Chadema kwani baada ya uamuzi huo, chama hicho kimekuja na njia nyingine ya kujijenga maeneo ya vijijini. "Hawa watajuta (CCM na Serikali) kuzuia mikutano yetu. Sisi tumekuja na njia nyingine ya kukijenga chama vijijini," alisema Dk Slaa ambaye hata hivyo, hakubainisha njia gani anayotumia sasa kukijenga chama hicho cha upinzani. Alipoulizwa atamaliza lini ziara yake hiyo ya kukijenga chama kwa njia mbadala, alijibu," Tulipanga kutumia siku 44 katika mikoa mitano, lakini nadhani siku hizo zitaongezeka baada ya mikutano yetu kuzuiwa.” Mwanzoni mwa mwezi huu, Chadema kilianza ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini katika kile wanachokiita Movement for Change (M4C). Hata hivyo, wakiwa mkoani Morogoro, chama hicho kiliingia katika mgongano na polisi katika vurugu zilizosababisha kifo cha mfuasi wake mmoja na majeruhi wawili. Baadaye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema aliipiga marufuku mikutano na maandamano ya chama hicho iliyopangwa kufanyika mkoani Iringa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kupisha Sensa ya Watu na Makazi.
 
Back
Top Bottom