Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,072
CHADEMA YAWATIA SHIME SERENGETI BOYS
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa salaam za heri kwa Vijana wa Timu ya Taifa chini ya miaka 17, Serengeti Boys wanaoiwakilisha nchi yetu kwenye mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana, ambao leo wameingia dimbani kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Timu ya Mali, ambayo ni bingwa mtetezi wa kombe la michuano hiyo.
Tunapenda kuwatia shime vijana hao kuwa wamebeba dhamana kubwa ya taifa letu katika mashindano hayo na matamanio ya Watanzania ambao wangependa kuona jina la nchi yao likiwika na kutamkwa katika mafanikio ya mchezo wa soka barani Afrika na dunia kwa ujumla.
Kutokana na matokeo waliyopata leo ya kutoka sare tasa dhidi ya timu bingwa mtetezi na kwa kuzingatia mwenendo wao katika safari ya kuelekea fainali hizo nchini Gabon, kuanzia kwenye hatua ya mtoano, kisha maandalizi waliyoyapata wakiwa kambini Morocco ambapo walishinda michezo mitano ya kirafiki kati ya saba waliyocheza huku wakitoka sare mmoja na kupoteza mmoja, wakizifunga timu mahiri barani Afrika, Watanzania wamewekeza matumaini yao kwa vijana hao kuwa wataipatia heshima nchi yetu na kumaliza kiu ya muda mrefu ya kutaka kuona timu zao za taifa zinazoshiriki kwenye mashindano ya michezo mbalimbali, zinaliweka jina la nchi yetu katika 'ramani ya michezo' duniani.
Watambue kuwa Watanzania wa kila hali bila kujali tofauti zao zozote, wanafuatilia fainali za mashindano hayo kwa ari kubwa kwa sababu hawatazami tu sura za vijana wa mataifa mengine, bali pia wanafuatilia ushiriki wa vijana wao mahiri, hivyo ushindi wao kwa kila mechi (zinazofuata) na hatimae kufika mbali katika michuano hiyo na kuchukua ubingwa, utakuwa furaha na heshima kubwa kwa Watanzania wote na nchi kwa ujumla.
Mungu ibariki Serengeti Boys
Mungu ibariki Tanzania
Imetolewa Jumatatu, Mei 15, 2017 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA