CHADEMA yawa gumzo Marekani, vua gamba vaa gwanda!!

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,395
92,720
Tawi la CHADEMA Washington DC lazidi kumwaga kadi za uwanachama DMV...!!!


_DSC9521.JPG

Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Kalley Pandukizi akiwa na katibu wachama hicho,Ndugu Libe Mwang'ombe alipotoa kadi rasmi kwa Beautician maarufu na designer wa kiTanzan Linda Bezuidenhout (LB)

Katika miaka ya nyumba Linda aliwahi kusponsor matukio mbali mbali kwenye miaka ya 1990 wengi wao wakimjua kwa Linda Express Nchini Tanzania ambae ambaye hivisasa anajishughulisha na biashara ya nguo za kiume milanovita.com pamoja na zakike ambazo anadesign mwenyewe kwa brand name ya Linda kutoka Atlanta, Georgia Nchini Marekani.


_DSC9526.JPG

Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe akimkabidhi rasmi mwanacham mkareketwa ambae ni mwana mitindo Linda Bezuidenhout (LB) kati ya uwanachama wa chama cha Demokrasia Chadema katika ofisi ya tawi la Tawi la Chama Washington DC.


_DSC9531.JPG

Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Washington DC Mhe. Kalley pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakipata picha ya pamoja na Linda Bezuidenhout Atlanta, Georgia na wanachama wa tawi la chadema Washington DC


_DSC9545.JPG

Viongozi wa tawi la chadema Washington DC wakipata Champagne

_DSC9542.JPG

Linda Bezuidenhout (LB) furaha baada ya kuvua kamba kuvaa gwanda na kuchukua kadi kuwa mwanachama kamili wa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Msikilize kwa makini mwana mitindo mbunifu wa
Linda Bezuidenhout (LB) Aakilonga na Swahilivilla

 
Peoples Power!!!!!!!!!!!!!!! Tunahitaji sana mchango wa watu walioko nje... Waje watupe experience.

Swali la kiaina kwao: Je waTZ nje ya nchi wanaheshimiwa na kuogopwa na wazawa kama sisi tunavyowaogopa hapa nchini?
 
wakati ndio sasa,

  • wa kusema bye,bye CCM
  • wa kuwakataa wezi wa kodi za nchi
  • wa kupinga mafisadi ndani na nje ya nchi
  • wa kuwazomea viongozi wezi
  • wa kuingiza CHADEMA madarakati ili itunuru wananchi kutoka kwenye mikono ya mafisadi
 
Safi sana makamanda,angekuwepo kamanda mkuu mh Mbowe angemwambia huyo dada "Kunja ngumi kamanda,Peoplesssssssssss!" hahahahahahahahaha!
 
Nitapata wapi Gwandas kama za hao makamanda wakuu? nzuri kweli! huyo dada kweli mtu wa mitindo hadi viatu rangi ya Gwanda!
 
You guyz mmenisisimua sana, wewe Linda leta hiyo sample ya gwanda maana la aina yake nataka niwe wa kwanza kutoka nayo hapa bongo kabla hawajaniwahi.
 
You guyz mmenisisimua sana, wewe Linda leta hiyo sample ya gwanda maana la aina yake nataka niwe wa kwanza kutoka nayo hapa bongo kabla hawajaniwahi.
Suzie hakuna wa kukuwahi, hilo Gwanda amedesign yeye mwenyewe Linda na jana yeye ndio mtu wa kwanza kulivaa ndani ya Maryland MD. tuwasiliane kwa inbox nijue nitakuwezesha vipi ulipate Gwanda lako haraka.
 
Last edited by a moderator:
Raha tupu.....! Bado kidogo tutamsikia na Obama naye kavaa gwanda! Sasa sijui kama vasco ataenda tena kumtembelea huko U.S.A...?

Peoples.........
 
Safi sana, we are proud of you guys. Linda mimi penda hilo gwanda tatizo linakuja nikibanwa naanzia kusalula lote au....... Embu ongeza kaubunifu maana hilo ovaroli tamu lakini tukumbuke uvaaji wake na muda

Sent from my BlackBerry 9910 using JamiiForums
 
Peoples Power!!!!!!!!!!!!!!! Tunahitaji sana mchango wa watu walioko nje... Waje watupe experience.

Swali la kiaina kwao: Je waTZ nje ya nchi wanaheshimiwa na kuogopwa na wazawa kama sisi tunavyowaogopa hapa nchini?[/QUOTE]


Mkuu asikudanganye mtu, kwa mtu yeyote aliyeko nje atakuambia ukweli kwamba mataifa mengine yanathamini sana wazawa kuliko wageni. Mimi nina profession muhimu sana, lakini hata hivyo sipewi uzito kama mzawa wa nchi hii. Ukishaitwa immigrant ujue wewe ni kudharaulika tu siku zote. Pamoja na hayo inabidi tuvumilie kuliko kuishi maisha magumu ya tz yanayotokana na sera mbovu za magamba.
 
Matola tutahitaji gwanda kama hilo la Linda kwa ajili ya kinadada kwa bei ya kawaida ambayo mtazania yoyote aweza kuimudu, si lazima zishonwe huko hata hapa kwetu tuna designer wazuri tu.
 
Last edited by a moderator:
Suzie hakuna wa kukuwahi, hilo Gwanda amedesign yeye mwenyewe Linda na jana yeye ndio mtu wa kwanza kulivaa ndani ya Maryland MD. tuwasiliane kwa inbox nijue nitakuwezesha vipi ulipate Gwanda lako haraka.

Sawa, nina email address ya Kalle nitatumia hiyo nashukuru sana, I hope hatatuletea kwa gharama za mafisadi, pia angeongeza kaubunifu kidogo kama alivyosema Josephine maana Mmmmh sijuiiii....... Urembo wataka utashi
 
Last edited by a moderator:
Matola tutahitaji gwanda kama hilo la Linda kwa ajili ya kinadada kwa bei ya kawaida ambayo mtazania yoyote aweza kuimudu, si lazima zishonwe huko hata hapa kwetu tuna designer wazuri tu.
TaiJike sidhani kama kuna designer yeyote wa ndani amekatazwa kudesign Gwanda kwa ajili ya kina Dada, kumbuka kila mtu anataka kuvaa kitu kutokana na uwezo wake kipesa, tofauti ya nguo inakuwa kwenye material ya kitambaa, angalia kwa makini hilo Gwanda la Linda, Dada yeyote anayejiweza kivijisenti angependa Gwanda lenye material hiyo na siyo kama linalovaliwa na wanaume.
 
Last edited by a moderator:
Sawa, nina email address ya Kalle nitatumia hiyo nashukuru sana, I hope hatatuletea kwa gharama za mafisadi, pia angeongeza kaubunifu kidogo kama alivyosema Josephine maana Mmmmh sijuiiii....... Urembo wataka utashi
Kama una Email ile ya lindamali sasa hivi haiko active, ila unaweza kumuinbox hata kwa kupitia uso kitabu.
 
huyu linda ni dada yake na richard yule wa BBA sio? hilo jina la ubini linanifanya niamke hayo
 
Back
Top Bottom