Chadema yaunguruma Nyamongo jioni ya leo!!!

Kinyengeli

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
452
142
Leo tar 07/05/2012 mb wa viti maalum kamanda Ester Matiko amefanya mkutano wa hadhara Nyamongo Tarime kwenye mgodi wa North Mara na kuzungumzia masuala mbalimbali juu ya manyanyaso ya mgodi kwa wananchi na elimu ya uraia kwa wananchi hao. Wananchi hao wameonyesha uvumilivu pamoja na kijimvua kilichokuwa kikinyesha huku makamanda wakiendeleza mapambano na miamvuli. Big up CDM.
 

Attachments

  • IMG0341A.jpg
    IMG0341A.jpg
    11.1 KB · Views: 105
  • IMG0342A.jpg
    IMG0342A.jpg
    8 KB · Views: 107
Nashukuru kwa taarifa mkuu ila kwenye picha inaonyesha ulipiga ukiwa umejificha mvua. Kamanda unatakiwa kwenye manyunyu ukomae na siyo kujificha
 
Vipi hakuna waliojivua gamba huko?
Hongera kamanda kaza mkanda huu ni msako wa nguvu kuelekea ikulu 2015
 
T.2015 CDM MPAKA KIELEWEKE.Halali mtu.Sirikale imeua watz nyamongo na kwenye migod mingne ya madini.We need changes!
 
mbona picha ya pili haieleweki? au hao ni simba?. asante kwa taarifa mkuu.
 
Elimu sahihi na makini ikitolewa, hata panya atainuka na kumfukuza paka maana atajua kuwa kumbe yeye sio kitoweo halali bali ni kwa kuwa ameruhusu fahamu na akili zake zimdanganye kuwa aliumbwa awe kitoweo kwa ajili ya paka. Kwa hili la chama tawala na vyama vinavyoinuka, sio kwamba wao ni paka, bali walijifikiri ni paka, na wakawafanya wengine waamini kuwa wao ni panya. Civic Education pasipo kuchoka, kuwafikia watu wasiofikiwa, kuwaeleza ukweli na mamlaka waliyo nayo ni njia sahihi kwa ukombozi wa pili, wa uhakika na wa amani wa Taifa letu... We shall overcome!!!
 
Naona hii ni twanga kotekote, kweli M4C ni kiboko, hadi JK anaona maruweruwe, kukaa Ikulu inakuwa ishu....
 
Back
Top Bottom