B.G TANTAWI
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 496
- 379
Kuna taarifa za Uhakika na sahihi kuwa Chadema imeamua kutumia mbinu kama zile za Mugabe kule Zimbabwe na Jubilee kule kenya ili kuweza kushinda Uchaguzi mkuu wa 2014 na 2015, Mbinu hizo ambazo mpinzani wake alibweteke baada ya kupata Uwaziri Mkuu zilimsaidia sana Mugabe Kushinda Uchaguzi ulioisha juzi, Hata Odinga anaelezwa kubweteka sana baada ya kupata Uwaziri mkuu, wakati wenzake walikuwa vijijini wakichapa kazi.
Baada ya kuwepo taarifa kuwa chadema haipo vijijini na CCM ikawa inatumia hiyo kama kete yake, sasa Chadema imesambaza vijana wake nchi nzima hasa maeneo ya vijijini ili kuweza kujipenyeza na kupenyeza Chama chao huko vijijini, Taarifa kutoka kwa mmoja wa vijana hao ambaye yeye yupo kanda ya ziwa zinasema kuwa Chadema lazima itashinda uchaguzi wa 2014 na ule wa 2015, amesema "Unajua kwa muda mrefu watu wamekuwa wakisema kuwa chadema haipo vijijini ila ipo tu mjini, sasa tumeamua kuanza kazi mapema na hadi kufikia sasa tumeweza kuvuna wanachama wengi sana.
Taarifa za ndani ya chadema zinathibitisha kuwa kwa sasa wanawatumia pamoja na watu wengine vijana waliomaliza vyuo vikuu ili kuweza kufikisha ujumbe vijijini,
Vile vile, katika kuonyesha kuwa Chadema inafanyia kazi maoni ya watu hasa hapa Jamii forums, mtoa habari huyo amesema, "Unajua Katibu mkuu wetu "akimaanisha Dr. Slaa" ni member wa Jamii Forums kwa hiyo kuna uzi uliwahi kuwekwa JF kuwa kwa sasa Chadema itafute wanachama wengine wapya wa vyama vingine hasa hasa CCM badala ya kuhangaika na mtaji walionao kwa sasa, kwa hiyo habari ile ilimgusa sana Dr. Slaa na kuamua kuwapa majukumu zaidi vijana hawa.
Mbinu nyingine ambayo tayari inafanyiwa kazi na Makao makuu ya Chadema ni ile ya kuteua team maalum ya watu 100 ambao kazi yao kubwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 itakuwa kufuatilia kwa ukaribu Mchakato wa upigaji kura, kukusanya matokeo kwa ustadi mkubwa na kuangalia na kukusanya taarifa na ushahidi wowote kama au ikiwa kuna dalili zozote za uchakachuaji, hii imefanyika kwa sababu imeonekana kuwa wakati wa uchaguzi kila mtu huwa yupo "busy" jimboni kwake.