CHADEMA yatoa tamko baada ya Mbowe kutajwa katika listi ya Makonda

REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,925
14,895
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo February 8 2017 ametangaza kuiachia orodha ya Watu 65 wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya ambapo amemtaja pia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ndani yake.

Dakika chache baada ya kumtaja,CHADEMA Makao makuu Dar es salaam walikutana na Waandishi wa habari na kusema yafuatayo >>> “Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani“

“Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita“

‘Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi… tusingependa kuona viongozi wengine Waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa chama chetu“

Sakata la Mbowe kutajwa na Makonda kuhusika na biashara ya maddawa ya kulevya
Visa vya watu maarufu wengine waliowahi kutuhumiwa au kukamatwa na madawa ya kulevya
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo February 8 2017 ametangaza kuiachia orodha ya Watu 65 wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya ambapo amemtaja pia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ndani yake.

Dakika chache baada ya kumtaja,CHADEMA Makao makuu Dar es salaam walikutana na Waandishi wa habari na kusema yafuatayo >>> “Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani

Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita

Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi… tusingependa kuona viongozi wengine Waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa chama chetu
Dawa imeanza kuwaingia
 
Tuache kelele za ajabu.

Kama hizo taratibu zipo inamaanisha zimevunjwa au siyo?

Mnaonaje ishu ikiisha mkaenda mahakamani? Au ukagoma kwenda kwakua taratibu hazijafuatwa.

Au ukafungua kesi ya defamation baada ya kuwa cleared?

Kutumia ruzuku kwa mambo ya kitoto ni uchimvi. Mngeweza hata kupost FB, IG au Twitter.
 
Naunga mkono juhudi hizi hasa kwa kuanza kushughulikia baadhi ya Mapapa ila hili swala la kuwataja watu hadharani ndo kuna walakini sipendezwi nalo make unaweza ukaishia kumchafua mtu asiehusika. Cadema hii kitu pia inawahusu sana mnatabia ya kutaja taja watu kwa tuhuma za uongo mfano kipindi mnamtaja Lowasa kuwa ni Fisadi huku mkiwa hamna ushahidi mlizingatia utu wake na heshima yake katika jamii? leo hii nyie wenyewe mnaamini kuwa hakuhusika na huo ufisadi hebu mjifunze sasa mjue kabisa what goes around comes around, isiwe tu ikitokea kwenu ndo ionekane mnaonewa huku nyie pia huwaonea watu wengine.
 
Kama MNA kumbukukumbu juu ya kesi iyowahi kutikisa hapa Tanzania ingawa ilikuwa ya kutengeneza, ni ile iyokuwa ikimhusu Rwakatale kwa sasa mbunge na na mwanachama Wa chama cha chadema, akihusishwa na suala LA ugaidi ingawa ilikuja kubainika kuwa ilikuwa ya kutengeneza.

Kilichomkuta kinaweza pia kikawa au kikafanana na hiki kinachoenda kumkuta mwenyekiti Wa chama.

havitofautiani sana believe me. This is African politics
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo February 8 2017 ametangaza kuiachia orodha ya Watu 65 wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya ambapo amemtaja pia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ndani yake.

Dakika chache baada ya kumtaja,CHADEMA Makao makuu Dar es salaam walikutana na Waandishi wa habari na kusema yafuatayo >>> “Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani

Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita

Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi… tusingependa kuona viongozi wengine Waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa chama chetu
Swali la kizushi

Kwani kuthibitishwa kwa tuhuma na kuongelewa kwa tuhuma ni kipi kinaanza?
 
Back
Top Bottom