SI KWELI PreGE2025 CHADEMA yathibitisha kushiriki uchaguzi

SI KWELI PreGE2025 CHADEMA yathibitisha kushiriki uchaguzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kuna pahali nimeona chadema itashiriki uchaguzi je habari ni ya kweli?

CHADEMAJUN26,2025.jpg
CHADEMA26JUN25.jpg
CHADEMA26JUNI2025.jpg

 
Tunachokijua
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kimekuwa kikiendesha ajenda inayojulikana kama 'No reforms, No election' yenye lengo la kuhamasisha na kuchochea kufanyika kwa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na wenye haki ili kuepusha malalamiko yaliyotokana na mapungufu yaliyojitokeza katika chaguzi zilizopita. Kupitia ajenda hiyo mara kwa mara, chama hicho kimekuwa kikisisitiza kuwa bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi.


Taarifa inayosambazwa mtandaoni kuwa CHADEMA itashiriki uchaguzi mkuu 2025

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook na TikTok walichapisha taarifa zilizotumia utambulisho wa Jambo TV na The Chanzo zikinukuu iliyoonekana kuwa taarifa kwa umma ya CHADEMA ikitoa tamko rasmi kuwa itashiriki uchaguzi mkuu 2025.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani Juni 25, 2025 CHADEMA haikutoa tamko lolote la kuthibitisha kushiriki uchaguzi mkuu 2025, bali tamko linalosambazwa mtandaoni ni la kutengenezwa na wapotoshaji.

barua za CHADEMAPia barua yenye tamko hilo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo matumizi ya fonti tofauti na barua za CHADEMA, matumizi ya hati mkolezo isivyostahili yanathibitisha kuwa ni ya kutengenezwa na wapotoshaji.

Vilevile machapisho yaliyotumika kusambaza taarifa hiyo, si ya kweli, ni ya kutengenezwa kwani hayakuchapishwa na vyombo hivyo. (Jambo TV na The Chanzo)​
Hadi No Rwforms No Election

Leo Jumatano, Juni 25,2025 kupitia mtandao, kesi namba 12670/2025 imetajwa mbele ya Mhe. Jaji Kagomba, Mahakama Kuu Dodoma. Kesi imefunguliwa na Raia ni SiSi; Kumbusho Kagine pamoja na Bubelwa Kaiza, wakiwakilishwa na Mawakili wasomi Mpale Kaba Mpoki na Jebra Kambole
 
Back
Top Bottom